Mtazamo wangu kuhusu siasa za Tanzania na Rais Magufuli

Be blessed
 
Hivi nikuulize mkuu, mfano Dr. Sengondo Mvungi (Mungu amrehemu huko aliko) Alivamiwa akapigwa na kuporwa vitu vyake kama 💻 na vingine, Je yeye ni marehemu ni ushirikiano upi aliouonyesha hadi watesi wake wakapatikana na sheria ikachukua mkondo wake au marehemu RPC BALO wa Mwanza? We vp?
 
Hukumuona yule mbunge viti maalum alipeleka msaada shuleni wakamkatalia kisa mpinzani? We vp?
 
Mpaka hpo tumejua upande wako
 
Unaandika sana, too wordy!!

Unajaribu kuwa neutral ili uuze hoja yako umeshindwa!!

Be brief and to the point!!

Mwenzio mwanaharakati huru alianza hivi hivi sasa hivi hata hajielewi!!

Amekuwa kichekesho cha taifa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Hongera kwa kukiri kuwa Serikali iliyoko madarakani inatumia vizuri kodi za wananchi kuboresha huduma za kijamii pale upouliza Kwani huduma bora kwa hao watu wa vijijini zinaletwa na ccm au ni kutokana na kodi za wananchi?.

Je, upinzani unajivunia nini, katika miaka 4 ya utawala wa Serikali iliyoko madarakani, cha kuwaambia wananchi, wapiga kura. Au wataendeleza ngonjera zao za madai ya Demokrasia, Tume Huru ya Uchaguzi, Haki bila kuwajibika, na Uhuru usio na mipaka. Naamini hawatawaambia wapiga kura, kwenye majukwaa ya siasa, ukweli kuwa wamekuwa wakitumia Demokrasia, Haki na Uhuru uliopo kufikisha madai hayo ndani na nje ya mipaka ya nchi hii.
 

Acha kunilisha maneno, wapi nimesema serikali inatumia vizuri kodi za wananchi? Kuna kutoa huduma za jamii kutokana na kodi za wananchi, lakini kutumia vizuri kodi za wananchi kutoa huduma ni jambo jingine.

Kwani Nyerere alipoenda kudai uhuru huko UNO alikuwa amejenga madaraja mangapi, na barabara ngapi za kuwaonyesha wananchi hadi atake kupewa uhuru? Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani.
 

Nimekuelewa sasa kuwa viongozi wa upinzani, siyo wanachama wao, wanadai/tafuta uhuru wa kutawala na siyo maendeleo ya watu!
 
Uongozi wa nchi hauna majaribio. Hata vile, kwa maneno na matendo ya viongozi wa upinzani, ni dhahiri hawajawa tayari kuongoza nchi. Japo wanaongoza katika baadhi ya Halmashauri na Majimbo ya uchaguzi, hawajaonesha utofauti wa mabadiliko, zaidi ya hali kuendelea kuwa mbaya.
 
Umeandika makala ndefu yenye maudhui mbili tu.
Yakwanza kumsifia Bw Yule. Hata kwa maovu ya wazi aliowatendea Wapinzani wake ndani ya chama na nje ya chama chake.
Pili ni kujaribu kumchafua Mh Lissu aliyekwenda nje kupigania uhai wake uliokuwa uondolewe na eti wasiojulikana ingawa hata ww mwenyewe unawajua fika.

Kwasasa Watz sio wale uliokuwa ukiwafikiria enzi zile za zidumu fikra za mwenyekiti. Wana muomko mkubwa na pia wanajitambua. Usihangaike kutumia propaganda zako mfu ktk kujenga hoja kwenye mioyo ya Watz wa sasa. Usuwafanye Watz majuha kwakuwa unaemsujudia kakamata mpini. Wakati wowote huo mpini unaweza kuvunjika au kumponyoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasema Rais Magufuli hawajui waliompiga Mh Lissu risasi. Unasema ni Mh Lissu ndiye aliyekataa kutoa ushirikiano kwa Polisi. Je Lissu alipokuwa Hosp Nairobi nchini Kenye kuna Polisi waliokwenda kumuona kwa lengo la kumhoji?? Je nini kiliwapata Wabunge wenzake toka chama tawala??
Nani alizuia fedha za matibabu kwa Mh Lissu??

Unaetaka kumsafisha hasafishiki kwa propaganda zako hizi. Usikimbilie kupindisha ukweli juu ya shambulio lile kwani hata unaejaribu kumsafisha alishakiri mwenyewe kuwa Watz sio Wajinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wakati Lowasa alipotimkia Chadema ninyi mlikaa kimya? Je unayakumbuka maneno ya Polepole?? Lowasa hivi sasa yuko huko kwenu kama kweli ni fisadi mtimueni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuelewa sasa kuwa viongozi wa upinzani, siyo wanachama wao, wanadai/tafuta uhuru wa kutawala na siyo maendeleo ya watu!

Unaongea utoto gani mwengeso, ni nani atatawala bila kuleta maendeleo yoyote? Hata wakoloni walitutawala lakini kuna maendeleo walileta.
 
Kwa hiyo nchi nzima tufuate tu hisia za watu kama hizi zako?

Tulipopata uhuru Tanganyika tulikuwa nao viongozi wenye uzoefu wa kuendesha serikali; mbali hata ya kutokuwa na watumishi wenye sifa za kufanya kazi maofisini?
 
Nimepitia hoja za wachangiaji pamoja na majibu ya mleta mada katika hoja hizo,nimegundua yafuatayo!
1.Michango yote ambayo mleta mada ameweka alama ya "like" ni zile zinazoshambulia upinzani au kumtetea JPM!
2.Kuna hoja moja ambayo mleta mada ameiweka ambayo ni Tundu Lissu kuichafua Tanzania!Lakini hajaeleza ni kwa vipi Tundu Lissu anaichafua nchi,lakini pia sioni uhusiano waowote kati ya hoja ya ushoga aliyoishikia bango na kuchafua nchi!Hakuna alipoonesha Tundu Lissu anachafua nchi zaidi ya kurejea ushoga!
3.Mleta mada anajaribu kujificha kwenye kivuli cha kutokuwa na Chama ili kujenga hoja zake,lakini ukisoma hoja zake anashindwa kuficha mahaba yake kwa serikali ya JPM!Anasifu hatua ya JPM katika sakata la akina Lugola kuwa linaonesha JPM anavyoheshimu mamlaka ya bunge kwenye maamuzi!Lakini anasahau mambo ambayo JPM anafanya bila kulishirikisha Bunge!JPM amelaumiwa sana kwa kutumia fedha kinyume na bajeti,ndio kisa hata cha 1.5 trilion CAG alizosema hajui ziliko maana CAG hukagua miradi kulingana na bajeti ilivyopitishwa na bunge,sasa kama kuna miradi nje ya bajeti hiyo CAG hana mkono wa kuikagua!Hapa ndiko kulizaa bunge kuitwa dhaifu baada ya kuonekana halina meno!
Sasa kisa tu cha kesi ya kina Lugola,mleta mada kajitia boriti kwenye macho yake!Hii inadhihirisha mahaba ya wazi kwa JPM!
4.Mleta mada kashindwa kueleza nini chanzo cha chuki!Katika zama kama hizi ambacho watawala wanaona upinzani ni kama Corona na unapaswa kutokomezwa,kweli anashindwa kujua chanzo cha chuki!Manyanyaso wanayopitia wapinzani,mleta mada kashindwa kuona ndio chanzo cha chuki iliyopo!

Nawasilisha!
 
Unaongea utoto gani mwengeso, ni nani atatawala bila kuleta maendeleo yoyote? Hata wakoloni walitutawala lakini kuna maendeleo walileta.
Yaani nawashangaa wapinzani kwa tafsiri yao ya maendeleo kuwa ni wao kuwa madarakani! Du!

Kama viongozi wa upinzani wameshindwa kuonesha umma wa wapiga kura matumizi mazuri ya ruzuku, demokrasia ndani ya vyama vyao, na udhibiti wa lugha wanayotumia kufikisha ujumbe wao, hakika bado ni wanasiasa uchwara.
 
Wakuamua nani apewe ridhaa ni wananchi wapiga kura,so wakati wa uchaguzi wataenda kuuza sera zao ni nini watafanya na wakiaminiwa wanachaguliwa!Huo mtazamo ni wako wewe kada wa lumumba!
 
CCm ndio chama cha magufuli na ndio sababu ya uharo wote huu Tanzania na kwa taarifa yako ccm imejengwa kwa misingi ya rushwa wizi na uuwaji hii ndio CCM sasa kama wataka kumsifu msifu tu na pia CCM ujuwe huu ni mwaka wa 60 kutawala Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…