Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Hivi mmeiona hii video ya tukio la mauaji yaliyotokea Jumamosi iliyopita kwenye duka la Boxer huko eShowe, KwaZulu-Natal? Inatisha sana! Jamaa mmoja (33) aliyekuwa mfanyakazi wa duka hilo aliwaua kwa kuwamiminia risasi mameneja watatu wa kike ofisini kwao baada ya kufukuzwa kazi kwenye kikao cha nidhamu.
Wahanga ni akina mama watatu: Thembeka (Meneja Mkuu), Lulama (Bakery), na Thandiwe (Utawala). Mashuhuda wanasema jamaa aliwazibia njia, akawafungia ndani, akawamiminia risasi za kutosha, akabadilisha kabisa na "magazine" nyingine akawaongeza risasi kisha kukimbia. Polisi (SAPS) bado wanamtafuta mpaka sasa.
Naona huko mitandaoni Wasouth wanalaumu duka la Boxer na kuuliza: Mtu mkatili hivi aliingiaje kwenye mfumo wa ajira wa duka kubwa namna hii?
Binafsi naona Wasouth wanajisahaulisha ukweli halsi.
Haya ni madhara ya moja kwa moja ya mihemko yao ya kiuchumi na kijamii. Miezi michache nyuma kulikuwa na wimbi la propaganda kali za kisiasa zilizolenga kuwafukuza wafanyakazi wote wageni kwenye biashara za ndani. Ili kulinda biashara zao zisiaribiwe, maduka na viwanda vikafuta kazi wageni wote kwa mkupuo.
Sasa soko la ajira limekumbwa na uhaba mkubwa wa nguvu kazi tena wa ghafla.
Biashara nyingi sasa hivi zinapumulia mipira; zinapambana kubaki wazi lakini hazina watu wa kuaminika wa kufanya kazi. Ili mradi tu duka liendelee kufanya kazi, waajiri wanakurupuka kuajiri mtu yeyote bila hata kufanya "background checks" za tabia au usaili wa kina.
Wanajikuta wanachukua watu wenye rekodi za uhalifu, msongo wa mawazo, na roho za kikatili kama huyu muuaji.
Hili ni janga linathibitisha jinsi sera za kufuata mihemko na kutafuta umaarufu wa muda mfupi zinavyoumiza jamii. Unapofukuza wageni kwa pupa bila maandalizi, unajaza nafasi zao kwa kushusha vigezo vya usalama, na mwisho wa siku watu wasio na hatia ndio wanaolipa kwa damu zao.
Mungu azilaze roho za mama wa watu kwa amani.
MailGuardian