Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Na: Dr. Zack, Mtaalam wa Masuala ya Uchumi Duniani
01.10.2026
Kuzinduliwa kwa mradi wa Dangote wa US$16 bilioni huko Lamu, Kenya, jana si habari ndogo kwa Afrika Mashariki. Refinery hiyo imepangwa kuwa na uwezo wa kuchakata mapipa 700,000 ya mafuta kwa siku, ikiambatana na mtambo wa umeme wa MW 1,000, pamoja na uzalishaji wa mbolea na kemikali. Kenya inatarajia mradi huo kuunda zaidi ya ajira 60,000 katika kile kinachoelezwa kuwa uwekezaji mkubwa wa viwanda katika ukanda huu. Dangote pia ameweka mezani uwezekano wa serikali za nchi za Afrika Mashariki kushikilia kwa pamoja hadi asilimia 30 ya mradi huo.
Lakini Tanzania nayo haikukaa na kuangalia Lamu ikiondoka na fursa. Mpango wa Tanga Regional Energy Hub unaounganisha Tanzania, Uganda na Vitol Bahrain unalenga kuwekeza zaidi ya US$20 bilioni katika mfumo mpana wa nishati unaojumuisha refinery, matanki ya kuhifadhi mafuta, jetty ya kupokea mafuta ghafi, miundombinu ya baharini, biashara na usambazaji wa bidhaa za mafuta, pamoja na bomba la bidhaa za mafuta linalounganisha Tanga na Uganda. Serikali ya Tanzania imesema utekelezaji wake unalenga kuongeza ajira, local content, ujuzi wa wataalamu wazawa na biashara ya nishati. Muhimu zaidi, Tanga haianzi kutoka sifuri: inajengwa juu ya EACOP yenye urefu wa takribani kilomita 1,443, inayounganisha maeneo ya mafuta ya Uganda na Tanga, na yenye uwezo uliopangwa wa kusafirisha hadi mapipa 230,000 kwa siku.
Hapa ndipo tofauti ya kimkakati inapoonekana. Lamu inaleta refinery kubwa sana na inaweza kuwa kituo muhimu cha mafuta kwa Kenya na nchi jirani. Tanga, kwa upande mwingine, inalenga kujenga mfumo mzima wa corridor ya nishati unaounganisha mafuta ghafi ya Uganda, Bandari ya Tanga, storage, refining, pipeline ya bidhaa, biashara na masoko ya Tanzania, Uganda na nchi nyingine za ndani ya Afrika Mashariki. Uganda yenyewe inaendelea na refinery yake ya Hoima yenye uwezo wa mapipa 60,000 kwa siku, na serikali hizo mbili zinasema Hoima na Tanga zitakamilishana badala ya kushindana. Hii ina maana Tanzania inaweza kutengeneza mnyororo ambao thamani yake haishii kwenye kiwanda, bali unaendelea kwenye usafirishaji, bandari, maghala, biashara, huduma za kitaalamu, viwanda vinavyotumia bidhaa za petroli na ajira.
Kwa Mtanzania, hiyo ndiyo sehemu muhimu ya kuangalia. Kila pipa la mafuta linalopita kwenye miundombinu ya Tanzania linaweza kuunda shughuli za kiuchumi katika bandari, trucking, engineering, insurance, banking, warehousing, logistics, catering, construction na huduma nyingine. Na refinery inapozalisha ndani ya ukanda, thamani haishii kwenye kuuza mafuta ghafi nje na kununua bidhaa zilizokwisha chakatwa. Tanzania inaweza kuwa sehemu ya mnyororo wa thamani. Serikali tayari imeweka wazi kuwa Tanga Energy Hub inalenga kuongeza ushiriki wa wazawa kupitia local content na kujenga uwezo wa wataalamu wa ndani.
Hata hivyo, hapa ndipo tunapaswa kuwa wakweli kwenye namba. US$20 bilioni za Tanga si US$20 bilioni ambazo tayari zimewekwa benki kwa ajili ya refinery. Ni makadirio ya uwekezaji wa energy hub nzima, na bado kuna vipengele vinahitaji feasibility studies, financing arrangements na final investment decisions. Kwa upande wa Lamu, US$16 bilioni ni thamani ya mradi mkubwa wa refinery na complex yake, lakini pia una changamoto zake, ikiwemo masuala ya ardhi na kesi za kisheria zilizoripotiwa kabla na baada ya uzinduzi. Kwa hiyo, ushindani wa Tanga na Lamu haupaswi kupimwa kwa ukubwa wa headline pekee. Unapaswa kupimwa kwa swali moja: ni mfumo gani utakaobakiza thamani zaidi ndani ya uchumi wa Afrika Mashariki, na kila nchi itapata sehemu gani ya thamani hiyo?
Na hapo Tanzania ina sababu ya kujiamini. Hatuna haja ya kupigana na Kenya kwa kelele wala kujaribu kuiga Lamu kwa kila kitu. Tanzania ina EACOP, Bandari ya Tanga, eneo la kimkakati kwenye Bahari ya Hindi, ardhi, masoko yanayounganisha Tanzania na nchi za ndani, na uzoefu wa kuendesha miradi mikubwa ya miundombinu ya kikanda. Kinachotakiwa sasa ni kuunganisha rasilimali hizi kuwa corridor moja yenye ushindani, yenye refinery, storage, logistics, pipeline, petrochemicals, manufacturing na biashara ya kikanda. Hapo ndipo Tanga inaweza kuwa zaidi ya bandari ya kupitisha mafuta. Inaweza kuwa lango la thamani ya mafuta ya Afrika Mashariki.
Kwa hiyo, Tanzania tunapaswa kusimama kwenye maslahi ya Watanzania. Hii si vita ya kumchukia Dangote, Kenya au Lamu. Ni ushindani wa kiuchumi ambao unatakiwa kutufanya tufanye kazi kwa kasi zaidi, tujenge miundombinu kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha Watanzania wanakuwa washiriki wa kweli, si watazamaji wa uwekezaji mkubwa unaopita mbele yao. Tanga ikianza kusimama kama Energy Hub, fursa zitakuwa kubwa kuliko ajira za kiwandani pekee: zitakuwa kwenye usafirishaji, uhandisi, biashara, logistics, viwanda, huduma, teknolojia na supply chains nzima. Kwa hiyo Watanzania waanze kujiandaa sasa. Mradi ukianza Tanga, tusije tukawa watu wa kusubiri ajira; tuwe wafanyabiashara, suppliers, engineers, transporters, investors na wataalamu watakaokamata nafasi zao ndani ya corridor mpya ya biashara ya Afrika Mashariki.