Chariton003
JF-Expert Member
- Jul 18, 2022
- 333
- 905
- Thread starter
- #101
Ahsante kwa kuweka sawa!Wimbo wa taifa hauimbwi ngazi ya vilabu mkuu , unaimbwa kwa timu za taifa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ahsante kwa kuweka sawa!Wimbo wa taifa hauimbwi ngazi ya vilabu mkuu , unaimbwa kwa timu za taifa.
Iko wazi YANGA Ndiyo BINGWA wa CAFCC 2023Naanza kwa kuipongeza timu ya Yanga kwa hatua kubwa waliyoifikia kimpira!
View attachment 2645466
Japo hawakushinda kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na CAF binafsi naamini Yanga ndiye bingwa wa michuano ya CAFCC 2023. Wamecheza soka safi na la kisomi, hongera kwako Nabi na timu yako ya benchi la ufundi, uongozi wa Yanga na mashabiki wote wa Yanga!
Binafsi naamini kushindwa kwa Yanga kuleta kombe nyumbani ni kutokana na stile ya ushabiki wa mpira hapa nchini almaarufu Kama utani wa jadi unaofanywa na Simba na Yanga! Nafikiri umefikia pabaya na kama serikali haitaingilia kati sioni tukifanikiwa kimichezo! Aina hii ya ushabiki imehusisha mpaka wivu wa "kike", uchawi na inaua uzalendo wetu! Hapana lazima viongozi ngazi ya taifa waingilie kati!
Kama si Simba kuisaidia USM kwa namna ilivyoisaidia (sina ushahidi, ni mawazo yangu) hakuna namna yoyote USM angesinda mechi ya fainali ya kwanza iliyochezwa Dar achilia mbali kuchukua kombe hili!
Nilipokuwa natazama mechi ya mchezo wa fainali ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, mashabiki wa Simba walifurahi kuliko hata USM wenyewe Yanga walipofungwa goli la kwanza! Lakini Kama haitoshi, mashabiki hao hao wa Simba waliumia kiasi cha kutokwa machozi pale Yanga ilipofunga goli na huwezi amini walifurahi furaha kuu ajabu pale USM walipofunga goli la pili! Haipaswi kuwa hivi! Chonde sana serikali, ingilieni kati suala hili!
Natamani sana kuona michezo ikileta na kukuza umoja, uzalendo, amani, upendo, furaha nk.
Tusipoangalia, tutashindwa kuishangilia timu yetu ya taifa vizuri kwa kuwa tu mfungaji ni wa Simba au Yanga!
Ni jambo la kushangaza watu wa Kenya, Rwanda na mataifa ya jirani walikuwa wakiishangilia Yanga jana kwa kigezo cha timu yetu inayoiwakilisha Afrika Mashariki eti kuna mitanzania ilikuwa inaiombea mabaya!!! Huu ni ushabiki wa kilofa!
Nimemaliza!
PoleSina shida na mashabiki wa Yanga kuwadhihaki mashabiki wa Simba endapo Yanga ingeshinda na ningewapongeza kwa hilo maana lingeleta changamoto kwa Simba kukazana ili na wao walete kombe!
Binafsi kama ningekuwa rais wa nchi hii ningewasweka rumande wote wanaoshabikia timu pinzani kwenye mechi za kimataifa! Haiwezekani wimbo wa taifa uimbwe kabla ya mechi halafu litokee dude fulani jinga kusapoti timu pinzani! Kwangu huo ungekuwa uhujumu uchumi!
Wimbo wa taifa huimbwa katika mazingira machache muhimu kama vile rais anapotaka kuhutubia taifa na timu za mpira zinaposhiriki mechi za kimataifa! Bila shaka, kwa wakati ule, wachezaji wanaliwakilisha taifa! Wapo kwa niaba ya wananchi na kwa niaba mh rais! Kushindwa ni kumuaibisha rais na ni kuliaibisha taifa! Kama ningekukuta unashabikia rais kuaibishwa lazima ungetafuta nchi ya kwenda!