Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Si mtego mgumu...lakini ni mtego mkali... CCM kwa miaka yote imejitahidi sana kukwepesha na wakati mwingine kuahirisha milongas ya mihimili.
Kuanzia wakati wa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere na mjadala wa Uafrika na Uraia wa Tanzania hadi huu wa mkopo na Tozo wa Rais Samia. Migongano iliepushwa kwa kuzungumza kichama.
Sasa hivi kichama vitu haviendi na visingefika alipofikisha Rais Samia, kukataa msamaha alioomba Ndugai. Samia angeweza kutoa kauli ya kusamehe kama aliyotoa mtangulizi wake kwa waliomkosea wakati ule (mnakumbuka ya Kinana?). Mambo yangeisha kiutu uzima kwa kupiga picha na kunywa chai.
Spika ni mtu mzito sana Kikatiba...Rais ni mzito zaidi..hawapimani. Spika hana hata chipukizi wa kumlinda na mshale..Rais anaamuru majeshi.
Lakiki Samia yuko tayari kuandika historia ya kuwa Rais aliyemlazimisha Spika wa chama chake kujiuzulu kwa jambo la mitazamo midogo yenye kutofautiana kisera? Ni kweli tunataka kumuona Ndugai anatoka lango la Ikulubakitembea anageukageuka nyuma akijifuta jasho?
Kama Rais ni taasisi na Spika ni taasisi kama ilivyo kwa Jaji Mkuu. Tusiingie mtego huu. Wa kutegua ni Samia na si Ndugai.
Hekima itatamalaki? Ya nani?