Yaani unalinganisha tuhuma za Rais kutaka kusababisha nchi kupigwa mnada, tena tuhuma zilizotolewa hadharani, na tuhuma za kitoto kama za akina Makamba ambazo ziliongelewa behind the scene?! Hivi kama sio uvunjaji privacy uliokuwa unafanywa na Magufuli, wewe na wenzako mngefahamu akina Makamba waliongea nini dhidi yaJPM?Sasa hivi kichama vitu haviendi na visingefika alipofikisha Rais Samia...kukataa msamaha alioomba Ndugai. Samia angeweza kutoa kauli ya kusamehe kama aliyotoa mtangulizi wake kwa waliomkosea wakati ule (mnakumbuka ya Kinana?). Mambo yangeisha kiutu uzima kwa kupiga picha na kunywa chai.
Spika ni mtu mzito sana Kikatiba...Rais ni mzito zaidi..hawapimani. Spika hana hata chipukizi wa kumlinda na mshale..Rais anaamuru majeshi...
Ukweli kabisa, mwanzoni hili suala niliona ujinga lakini jana baada ya kuona video ya Ndugai akizungumzia hilo suala la mikopo, unaona wazi hoja yake was more than issue ya mikopo ambayo hakuwahi hata siku moja kuizungumzia wakati wa JPM ambae alikopa sana!!
Namnukuu Ndugai
"Lakini fikiria, nyinyi ndo wasomi. Kwa mfano Mama juzi ameenda kukopa 1.3 Trillion. Deni. Na tuna majengo hivi sasa, ya madarasa, vituo vya afya, ambavyo yanajengwa, kwa tozo. Hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni, au tubanane banane hapa hapa tujenge wenyewe bila ya madeni haya makubwa makubwa yasiyoeleweka? Ni lini sisi tutafanya wenyewe? And how? Tutembeze bakuli? Ndiyo heshima?
Tukishakopa tunapiga makofi. Sisi wa kukopa kila siku? Tukasema pitisha tozo. Anayetaka, asiyetaka, pitisha tozo. Lazima tuanze kujenga wenyewe. Nani atatufanyia? yuko wapi huyo mjomba? Tukapitisha. Sasa 2025 mtaamua. Mkitoa waliopo, sawa; waje ambao kazi yao itakuwa kwenda kukopa.
Endapo hiyo ndo namna ya ku-run nchi. Hivi sasa deni letu ni 70 Trillion. Hivi nyie si wasomi? Is that healthy? Kuna siku nchi itapigwa mnada hii."
Sasa ukiangalia hiyo nukuu ni kwamba Ndugai karusha mawe yake kwa SSH personally na wala sio kama taasisi! Yaani SSH anaenda kuchukua mikopo isiyoeleweka inayoweza kusababisha nchi kupigwa mnada!
Sasa kwa nafasi ya Speaker, tena mbae u-spika wake umetokana na ubunge wake, nini hapo tafsiri yake kama si kwamba hakubaliani na SSH, tena kwa jambo serious!? Yaani ameonesha hadharani kwamba SSH ni rais wa ovyo! Sasa kama anajua rais ni mtu wa ovyo anayeiweka nchi kwenye rehani, busara si ilikuwa kuachia madaraka ili aendelee kupiga spana?
Ninachokiona kwa Ndugai, he's not happy na SSH, na inawezekana anaona kama SSH amepunguza nguvu aliyokuwa nayo Magu ya kuifanya Dodoma kuwa Capital City ki ukweli ukweli!