Mtego Aliojitegea Rais Samia, nani atauvunjilia?

Mtego Aliojitegea Rais Samia, nani atauvunjilia?

Si mtego mgumu...lakini ni mtego mkali...
CCM kwa miaka yote imejitahidi sana kukwepesha na wakati mwingine kuahirisha milongas ya mihimili...

Kuanzia wakati wa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere na mjadala wa Uafrika na Uraia wa Tanzania hadi huu wa mkopo na Tozo wa Rais Samia. Migongano iliepushwa kwa kuzungumza kichama...

Sasa hivi kichama vitu haviendi na visingefika alipofikisha Rais Samia...kukataa msamaha alioomba Ndugai. Samia angeweza kutoa kauli ya kusamehe kama aliyotoa mtangulizi wake kwa waliomkosea wakati ule (mnakumbuka ya Kinana?). Mambo yangeisha kiutu uzima kwa kupiga picha na kunywa chai.

Spika ni mtu mzito sana Kikatiba...Rais ni mzito zaidi..hawapimani. Spika hana hata chipukizi wa kumlinda na mshale..Rais anaamuru majeshi...

Lakiki Samia yuko tayari kuandika historia ya kuwa Rais aliyemlazimisha Spika wa chama chake kujiuzulu kwa jambo la mitazamo midogo yenye kutofautiana kisera? Ni kweli tunataka kumuona Ndugai anatoka lango la Ikulubakitembea anageukageuka nyuma akijifuta jasho?

Kama Rais ni taasisi na Spika ni taasisi kama ilivyo kwa Jaji Mkuu. Tusiingie mtego huu. Wa kutegua ni Samia na si Ndugai.

Hekima itatamalaki? Ya nani?
Atoke TU kwenye Lile lango huku akifuta jasho Hanna nanna, wanaolichelewesha taifa ni pamoja na hiyo🤔.
 
Hii busara ilitakiwa ianze kwa Supika kwenda kumuona Rais na kumpa dokezo kiuongozi, kwenda public na kuhoji huku ukikebehi "nchi itapigwa mnada" zaidi ya hapo unasema wataamua 2025 mkitaka kuweka wa kukopakopa, huku kulikuwa ni kupungukiwa busara kwa hali ya juu.

Na retaliation yake ndio hii watu msije kumuona Rais amekosea kumjibu public kwasababu yeye aliongea public basi naye acha ajibu public ndio waende huko ndani wakamalizane, hauwezi kuharibu image ya mwenzako yeye akae amekuangalia tuu.

Huu ni mkakati wa maadui wa Samia, walianza kwakumuwekea matarakimu ya ajabu kuhusu foreign reserves za nchi ili tu aonekane kituko mbele ya umma wa waTanzania na hilo walifanikiwa kwani kosa halikusahihishwa kabla ya speech kusomwa but the damage had already been done. Ndio Ikaja hii ya Ndugai kuzungumzia mikopo na tozo , yote hiyo ikielekezwa kudiscredit credibility ya Rais kuwa hajali maisha ya wananchi kwa kubariki tozo na kukopa kopa hivyo!!

Haya yote yamepangwa ili kumdhoofisha asifanikiwe na agenda yake ya maendeleo towards uchaguzi mkuu kwani wao wana ajenda yao; it is up to Samia to act decisively kwa kuonesha kuwa sio kweli kuwa yeye ni Rais wa wananwake na sio wa wanaume!!! Kuna hiyo hoja kuwa yeye anadhani anaweza kuchaguliwa kwa kuwajali wanawake tu na kuwasideline wanaume!!! She should be in apposition to address these serious allegations through her actions.
 
Si mtego mgumu...lakini ni mtego mkali...
CCM kwa miaka yote imejitahidi sana kukwepesha na wakati mwingine kuahirisha milongas ya mihimili...

Kuanzia wakati wa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere na mjadala wa Uafrika na Uraia wa Tanzania hadi huu wa mkopo na Tozo wa Rais Samia. Migongano iliepushwa kwa kuzungumza kichama...

Sasa hivi kichama vitu haviendi na visingefika alipofikisha Rais Samia...kukataa msamaha alioomba Ndugai. Samia angeweza kutoa kauli ya kusamehe kama aliyotoa mtangulizi wake kwa waliomkosea wakati ule (mnakumbuka ya Kinana?). Mambo yangeisha kiutu uzima kwa kupiga picha na kunywa chai.

Spika ni mtu mzito sana Kikatiba...Rais ni mzito zaidi..hawapimani. Spika hana hata chipukizi wa kumlinda na mshale..Rais anaamuru majeshi...

Lakiki Samia yuko tayari kuandika historia ya kuwa Rais aliyemlazimisha Spika wa chama chake kujiuzulu kwa jambo la mitazamo midogo yenye kutofautiana kisera? Ni kweli tunataka kumuona Ndugai anatoka lango la Ikulubakitembea anageukageuka nyuma akijifuta jasho?

Kama Rais ni taasisi na Spika ni taasisi kama ilivyo kwa Jaji Mkuu. Tusiingie mtego huu. Wa kutegua ni Samia na si Ndugai.

Hekima itatamalaki? Ya nani?

Ya Ndugai yalikuwa maoni yake ambayo kila mtu ana haki yake.

Yakajibiwa kwa marungu na kumpelekea Ndugai kuomba yaliyopita yasiwe ndwele.

Maombi ya Ndugai yametupwa kwa kejeli.

Tulipo sasa ni hapa:

Msamaha kubutuliwa, Ndugai aungwe mkono

Aluta Continua.

Vita ni vita, Mura!
 
Ngoja nivute katiba ya 1977 ilifanyiwa marekebisho.
Nichukue na rasimu ya katiba ya Warioba.
Halafu nione nani ni nani ,wakati gani na wapi?

Huu mchezo kila mmoja acheze kwa tahadhari. La sivyo Jeshi linaweza kuichukua nchi kwa muda kidogo mambo yakilekebika.
Nani ajuaye kuwa bunge la ccm ambalo linahisi kuna uzanzibari lita vote kukasa imani na Ndugai?

Huu mtego mama asije kuingizwa king halafu kete zake zikaliwa zote.
Maana ili amle kirahisi awe na wabunge watakao mshabikia mama Tanganyika walio wengi ambao wanaridhishwa na mgawo wa Tozo za simu za Tz bara kugawiwa visiwani.
Labda atangaze fasta kulivunja bunge na baraza la mawaziri.
Lkn hii yooote mama ya nini, ninavyomdhania ni mwelevu na angekaa kumyaaa akaendelea kuchapa kazi wale wa kuongea na fever zao za 2025 mwisho wangekaa kimya. Maana mtoto mdogo halali na hela mkononi.
Nani alimwambia aje kujibishana nao? Walitosha aliowandaa akina Gavana wa benki na wengine wamujibu kwa capacity zao.

Dalili za kutochomoka 2025 zimeanza kuonekana. Genge la ccm B linazidi. Uzuri alikumbuka ule wimbo "tuna imani na ...... oya oyaaa oyaaa" na UNAFIKI ukiwa mwingi. AMEKUMBUKA sasa AELEWE.

Job amejipangaje na sala yake ya KITUBIO? Ajue Intel Sec wa kila kada wanamlia rada wametumwa .
Tunataka Royal people kwa Country sio wachumia tumbo na walamba viatu
 
Wakati ndugai anashinikiza asad atoke kisa tu alihoji matumizi ya fedha za matibabu mlishangalia, nionavyo mimi ndugai ana mengi aliliyoyafanya hadi kufikia kwenye tozo na mikopo, maana mama alisema eti rais wa mpito aliyekuwa anaratibu haya ni nan? Kimsingi rais kashaonesha kwamba hamtaki ndugai na huyo jiwe alikuwa anasamehe anawataka asiowataka alikuwa anafurusha na wengine hadi leo hawajulikana walipo. Hivyo hapa ndugai avune alichopanda
 
Ile kazi wale wenyeviti wa CCM mikoa walipewa ndio maana jana wakaitwa ikulu kupongezwa kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Hapo ukiangalia vizuri utaona Samia binafsi ameshaanza kujipanga kwa 2025, ila hataki wengine wajipange, akiulizwa anakimbilia najenga nchi, huu ni uongo anacheza na akili za wajinga.

Sasa nawashauri wote waanze kujipanga kwa 2025 hii nchi haina haja ya kuwa na Rais, inaweza kujiendea tu, kila siku tunalia umasikini, hakuna maji safi na salama, hawa miaka yote hawajui wanachofanya bora wapigane tu niangalie vita yao.
Msitudanganye huku Machui tulip Sisi tunakunywa maji safi na salama na yatapatikana muda wote.

Wananchi tunayaona matunda ya serikali yetu njema.
 
Si Tetesi, kuna vitu unaweza kusema tetesi lakini hili la spika kusimama na kuonyesha madhaifu ya Rais wazi wazi kwa uchambuzi ni wazi hali si shwari
CCM ktk uchaguzi wa ndani wa 2017 iliingiza madodoki ya kutosha ili kuweka mazingira ya team za ushindi...

Kisha madodoki hayo mkaja kuwaita WAJUMBE NUKSI walipovunja rekodi ya rushwa kwenye teuzi za ndani ya chama kuelekea uchafuzi mkuu 2020.

Jobo na wenzake hawakustahili hata kuwa wabunge kwa sababu hawana merits za kushika nafasi hizo.

Kikubwa ni kwamba, nchi imekosa muelekeo inayumba kwa sababu tumetengeneza TABAKA la watawala.

Mimi sioni tija kwenye huu mtanange lakini kwa mujibu wa Katiba yetu ya Nchi, ni wazi Spika amebugi step
 
Kaka hakuna mhimili wenye absolute powers zaidi ya serikali, Jaji Mkuu anateuliwa na Rais, akiamua kumvua wadhifa anaweza wakati wowote, pia Spika anapendekezwa na chama chini ya mwenyekiti ambaye ni Rais, kumbuka pia hoja yaweza kutolewa na wabunge ambao wengi ni ccm na mara zote wako loyal kwa chama na mwenyekiti. So wakiamua spika ang'oke ni dkk.Nguvu ya Rais katika nchi hii ni kubwa sana, ndio maana kipindi cha mwendazake hakuna aliyefungua mdomo.
 
That's what happens when you mess with women, na ndo maana wenye akili zao hawataki "ugomvi" na wanawake hata kama wanajua wana uwezo wa kuwatandika makofi. Tena kama wanawake wenyewe ndo wa pwani, ndo kabisa! Hawa watu hawana simile!
 
Si mtego mgumu...lakini ni mtego mkali...
CCM kwa miaka yote imejitahidi sana kukwepesha na wakati mwingine kuahirisha milongas ya mihimili...

Kuanzia wakati wa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere na mjadala wa Uafrika na Uraia wa Tanzania hadi huu wa mkopo na Tozo wa Rais Samia. Migongano iliepushwa kwa kuzungumza kichama...

Sasa hivi kichama vitu haviendi na visingefika alipofikisha Rais Samia...kukataa msamaha alioomba Ndugai. Samia angeweza kutoa kauli ya kusamehe kama aliyotoa mtangulizi wake kwa waliomkosea wakati ule (mnakumbuka ya Kinana?). Mambo yangeisha kiutu uzima kwa kupiga picha na kunywa chai.

Spika ni mtu mzito sana Kikatiba...Rais ni mzito zaidi..hawapimani. Spika hana hata chipukizi wa kumlinda na mshale..Rais anaamuru majeshi...

Lakiki Samia yuko tayari kuandika historia ya kuwa Rais aliyemlazimisha Spika wa chama chake kujiuzulu kwa jambo la mitazamo midogo yenye kutofautiana kisera? Ni kweli tunataka kumuona Ndugai anatoka lango la Ikulubakitembea anageukageuka nyuma akijifuta jasho?

Kama Rais ni taasisi na Spika ni taasisi kama ilivyo kwa Jaji Mkuu. Tusiingie mtego huu. Wa kutegua ni Samia na si Ndugai.

Hekima itatamalaki? Ya nani?
Sukuma gang kubalini kuwa hamna chenu
 
Kosa kuu la kiufundi la Ndugai ni kuomba Msamaha.

Ila Kosa kuu zaidi la kiufundi ni alilofanya Samia kumsema Ndugai kiasi kile, au kwa maana nyingine ni kutangaza vita na adui asiyejua idadi yake.

Samia amedanganywa sana Kuwa Rais ndio Kila kitu, amesahau Bunge likiamua linaweza Kuifanya Serikali isifanikiwe kwa lolote kwa chochote.

Samia anasahau kwenye kamati kuu watu wake wa uhakika ni 2 tu labda na Wazanzibar wenzake, Bado Kwenye mkutano mkuu wa CCM hajui wapo wangapi.
Acheni kudanganyana! Kwa Tanzania hii, RAIS NDO KILA KITU!! Rais ana maguvu kama yote! Rais ndie Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama! Majaji wote, wanateuliwa na rais! Ingawaje theoretically rais hawezi kumfuta kazi jaji lakini anaweza kumlazimisha ajihudhuru, na anatakiwa awe mbishi kweli kweli ili aweze kugoma!!

Ukitaka kujua nguvu ya rais, go back kwenye sakata la Membe na JPM!! Membe alikuwa na watu kuliko JPM! Membe amehudumu hadi nafasi za juu pale TISS, na kwa maana nyingine, pia alikuwa na watu TISS! Team Msoga YOTE ni watu wa Membe!! Lakini pamoja na sifa zote hizo, bado Membe alishindwa kufurukuta hata mbele ya Rais aliyekuwa anaonekana kama Msukuma Mshamba asiyejua hata kuongea Kiingereza fasaha!

Huyo ndo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Huyo ndie rais ambae aliweza kumzima Edward Lowassa aliyekuwa na maguvu kila kona! Huyo ndo rais aliyeweza kusema "Hii ni zamu ya spika mwanamke" na kuanzia hapo Samwel Sitta akaondolewa kwenye uwanja wake wa kujidai!! Rais wa Tanzania atake tu mwenyewe kutokuwa Mafia. Ukiona watu wanapigania katiba mpya ni pamoja na ku-dilute haya maguvu makubwa ya rais!!
 
Back
Top Bottom