Mtego Aliojitegea Rais Samia, nani atauvunjilia?

Mtego Aliojitegea Rais Samia, nani atauvunjilia?

Wale wabunge wana nafasi nzuri sana kwenye kuamua hili suala, ni either wapige kura ya kutokuwa na imani na Samia au kutokuwa na imani na Ndugai, kwao kuendelea kukaa kimya ni unafiki wasilete habari ya kulinda chama zaidi ya kulinda interests za nchi.

Kuwa na mihimili miwili isiyoelewana ni tatizo, kwa sababu yote hufanya kazi kwa kushirikiana, na kwa namna fulani inategemeana. Naona Samia ameaminiwa kwa kauli yake ya anajenga nchi hataki watu wamharibie, huu kwangu ni usanii tu.

Wakati yeye ndie aliekuwa wa kwanza kuwaambia wanawake wenzie 2025 ni zamu yao, kama alidhani alikuwa anapiga umbea kwenye kikao cha wanawake wenzie ajue wanaume walijua vita ndio imeshatangazwa, sasa apigane asijifiche kwenye kisingizio cha najenga nchi na kutaka kutumbua mawaziri wanaojipanga, anawaonea.
Nani kakwambia mihimili haielewani? Ni job tu na Wala siyo bunge. Tofautisha hilo
 
Si mtego mgumu...lakini ni mtego mkali...
CCM kwa miaka yote imejitahidi sana kukwepesha na wakati mwingine kuahirisha milongas ya mihimili...

Kuanzia wakati wa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere na mjadala wa Uafrika na Uraia wa Tanzania hadi huu wa mkopo na Tozo wa Rais Samia. Migongano iliepushwa kwa kuzungumza kichama...

Sasa hivi kichama vitu haviendi na visingefika alipofikisha Rais Samia...kukataa msamaha alioomba Ndugai. Samia angeweza kutoa kauli ya kusamehe kama aliyotoa mtangulizi wake kwa waliomkosea wakati ule (mnakumbuka ya Kinana?). Mambo yangeisha kiutu uzima kwa kupiga picha na kunywa chai.

Spika ni mtu mzito sana Kikatiba...Rais ni mzito zaidi..hawapimani. Spika hana hata chipukizi wa kumlinda na mshale..Rais anaamuru majeshi...

Lakiki Samia yuko tayari kuandika historia ya kuwa Rais aliyemlazimisha Spika wa chama chake kujiuzulu kwa jambo la mitazamo midogo yenye kutofautiana kisera? Ni kweli tunataka kumuona Ndugai anatoka lango la Ikulubakitembea anageukageuka nyuma akijifuta jasho?

Kama Rais ni taasisi na Spika ni taasisi kama ilivyo kwa Jaji Mkuu. Tusiingie mtego huu. Wa kutegua ni Samia na si Ndugai.

Hekima itatamalaki? Ya nani?

Kama ukimsikiliza mama kwa umakini inaonyesha kuna la zaidi ya kuropoka kule kwa Job!!!Kama Vile mama alikuwa anatafuta kisababu kidogo tu kumkata ngebe Job!!!Sema Job anezingua kuomba msamaha na kulialia kule
 
Hii busara ilitakiwa ianze kwa Supika kwenda kumuona Rais na kumpa dokezo kiuongozi, kwenda public na kuhoji huku ukikebehi "nchi itapigwa mnada" zaidi ya hapo unasema wataamua 2025 mkitaka kuweka wa kukopakopa, huku kulikuwa ni kupungukiwa busara kwa hali ya juu.

Na retaliation yake ndio hii watu msije kumuona Rais amekosea kumjibu public kwasababu yeye aliongea public basi naye acha ajibu public ndio waende huko ndani wakamalizane, hauwezi kuharibu image ya mwenzako yeye akae amekuangalia tuu.
Mkuu nikusifia kwa mawazo mazuri vipi umemaanisha pia kama kuna pahala Rais kajikwaa kwa speech yake amelazimishwa kukosea? Kukosewa na kukosea kujibu kukosewa vyote ni kukosea vipi hii imekaaje? Mama Au Baba kumjibu mtoto kwa vyovyote vile muhimu kudumisha heshima ya nyumba!!!
 
Timu magu mnaumia sana . Mnywe maji mpumzike kiriba cha roho kiwashuke
 
Ndugai kafanya ujinga kuomba msamaha, speaker ni mtu mzito sana

Kitendo chake cha kuomba msamaha kimempa loop hole Bi. Tozo kumdhalilisha
HAPO NDIPO ALIPO KOSEA SANA NDUGAI TENA ILITAKIWA KUTOA MSISITIZO WA KUKATAA MIKOPO MIKUBWA KWA MUDA MFUPI HIVYO INGEMFANYA AONEKANE KUWA NI KWELI ANAONGEA KWA KUANGALIA MASLAI MAPANA YA TAIFA
 
Unaonekana unaongea kishabiki ndugu.

1) Nani kakwambia Mama hawajui maadui zake na idadi yao?? Unamchkulia poa???

2) Yaani wewe hujui kwamba Rais ndio kila kitu ndani ya nchi hii. Kweli hujui hilo?? Unaikumbuka kesi ya uamsho??? Iliishaje???

3) Kwenye kamati kuu watu wa Mama ni wawili tu?? Like seriously? Huoni kama kuna Wazanzibari mpaka huko Njombe na Ilemela??

4) Ndugai ni wa kupuuzwa na hana nguvu yoyote mnayotaka kumpa. Walimtanguliza kikatuni chao slow slow akagonga mwamba chap kwa haraka, na hakuna yeye na genge lake walichoweza kufanya.

5) Nani aliekwambia wenyeviti mikoa sio watu wanaotakiwa kumpa imani Mheshimiwa rais?? Uliwaona Jana Ikulu?? Hivi wewe ulikuwa umekaa kwa upande gani pale??

6) Haya maneno ya watu hawako tayar kuongezwa na mwanamke ni ujinga tu. Huu ni mwaka sasa unamalizika na Mama ndie Rasi wetu

7) Mtu wenu hana namna zaidi ya kuachia ngazi tu. Sio suala la wewe kupenda au kutokupenda. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amir jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama na ni MWENYEKITI WA Chama Cha mapinduzi.
Ni kweli usemacho!!lakini!kuna serekali ndani ya serekali! Kama wewe ni msomaji mzuri wa jf utgundua kuna taasisi ambayo haionekani machoni lakini huamua nani ashike hatamu!!na imeshaamua kuwa mama mwisho 2025!!refer gazeti la uhuru mwandishi wake hakukurupuka alipoandika hatogombea 2025!!Mama akapaniki na kutangaza nia mapema!!na hilo paniki imeendelea hadi leo!!!we ona Mkapa,kijazi,maalim seif,jpm,mfugale,kwandikwa angalizo mlolongo huo unipe majibu!!!Amka usingizi I!!Magamba matatu anasema ajaye ni muislamu mwanamme mwenye misimamo kama JPM!!
 
Acheni kudanganyana! Kwa Tanzania hii, RAIS NDO KILA KITU!! Rais ana maguvu kama yote! Rais ndie Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama! Majaji wote, wanateuliwa na rais! Ingawaje theoretically rais hawezi kumfuta kazi jaji lakini anaweza kumlazimisha ajihudhuru, na anatakiwa awe mbishi kweli kweli ili aweze kugoma!!

Ukitaka kujua nguvu ya rais, go back kwenye sakata la Membe na JPM!! Membe alikuwa na watu kuliko JPM! Membe amehudumu hadi nafasi za juu pale TISS, na kwa maana nyingine, pia alikuwa na watu TISS! Team Msoga YOTE ni watu wa Membe!! Lakini pamoja na sifa zote hizo, bado Membe alishindwa kufurukuta hata mbele ya Rais aliyekuwa anaonekana kama Msukuma Mshamba asiyejua hata kuongea Kiingereza fasaha!

Huyo ndo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Huyo ndie rais ambae aliweza kumzima Edward Lowassa aliyekuwa na maguvu kila kona! Huyo ndo rais aliyeweza kusema "Hii ni zamu ya spika mwanamke" na kuanzia hapo Samwel Sitta akaondolewa kwenye uwanja wake wa kujidai!! Rais wa Tanzania atake tu mwenyewe kutokuwa Mafia. Ukiona watu wanapigania katiba mpya ni pamoja na ku-dilute haya maguvu makubwa ya rais!!
Exactly.

Kuondolewa kwa Assad ni kielelezo cha mwisho kwamba Rais wa Tanzania ni alfa na omega.
 
Kama ukimsikiliza mama kwa umakini inaonyesha kuna la zaidi ya kuropoka kule kwa Job!!!Kama Vile mama alikuwa anatafuta kisababu kidogo tu kumkata ngebe Job!!!Sema Job anezingua kuomba msamaha na kulialia kule
Mama anasema huko walishaanza kusema ni wa mpito..
Mitano tena.
 
Kama Rais ni taasisi na Spika ni taasisi kama ilivyo kwa Jaji Mkuu. Tusiingie mtego huu. Wa kutegua ni Samia na si Ndugai.

Hekima itatamalaki? Ya nani?
Ni mpaka ueleweke mkuu kwa wahusika ili hekima itamalaki. Rais ni muhimu kwetu kama nchi, tusimame naye. Lakini, tuhakikishe aliposimama pako salama. Yatakuwa makosa makubwa kwetu kama tukishangilia kusimama naye wakati ama kwa makusudi ama kwa uzembe wetu tunajua kasimama juu ya "mzinga wa siafu".
 
Ushawahi sikia Samuel Sitta anaomba msamaha kwa mkuu mwenzie wa muhimili! (enzi hizo alikua JK)

Kwa kifupi Job Ndugai kakosea alitakiwa aendelee kuvimba, yeye ni muhimili tofauti, na inashangaza mwanaume gani anakuwa mwepesi mwepesi kuomba msamaha tena kwa she!
TRUE VERY VERY TRUE ,NDUGAI KAFANYA KOSA KUBWA SANA ,tena ndugai kama alijijua yupo hivyo mambo aliyo wafanyia kina ngwajima na mbunge wa ukonga asingetakiwa kuyafanya alikuwa anatoa kauli zidi yao mbovu sana wakati kumbe na yeye anampinga mama ,hivyo mama kagungua ndugai siyo mzima kichwani tena aeleweki tofauti na kina gwaji boi
 
Kosa kuu la kiufundi la Ndugai ni kuomba Msamaha.

Ila Kosa kuu zaidi la kiufundi ni alilofanya Samia kumsema Ndugai kiasi kile, au kwa maana nyingine ni kutangaza vita na adui asiyejua idadi yake.

Samia amedanganywa sana Kuwa Rais ndio Kila kitu, amesahau Bunge likiamua linaweza Kuifanya Serikali isifanikiwe kwa lolote kwa chochote.

Samia anasahau kwenye kamati kuu watu wake wa uhakika ni 2 tu labda na Wazanzibar wenzake, Bado Kwenye mkutano mkuu wa CCM hajui wapo wangapi.

Samia alidokeza Kuwa akina Ndugai walitaka hii serikali iitwe ya Mpito, Kama Ndugai aliamini anaweza kuipeleka hiyo hoja Bungeni basi, Sio wa kupuuzwa hata kidogo.

Hawa wenyeviti mikoa ni watu wasiotakiwa kumpa imani Rais.

Samia anatakiwa ajue Tanzania nzima 80% hawako tayari kuongoza na Rais Mwanamke..

Mwisho nisingependa Ndugai ajiuzulu, ila anoeshe makucha yake sasa
Kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa katiba ya CCM na sheria ya usalama wa taifa Spika akijaribu kufanya chochote dhidi ya Rais ataishia pabaya sana. Nguvu ya mihimili mingine inategemea na mapenzi ya Rais
 
Wewe ile busara ya let us agree to disagree hauitambui kwahiyo ukipishana na kiongozi mwenzako ni unamuanika hadharani.
Ambayo aliyakataa Samia yana msingi wa kikatiba km ukopaji kinyemela na kupelekwa fedha nyingi Zanzibar kinyume na katiba,agree to disagree ni kwenye mambo yasiyovunja katiba tu na siyo haya ya upendeleo
 
Sukuma Gang mtakuwa machoko mwaka huu, Ngojea Samia hawafulumushe mkapambane na Hali zenu wapuuzi nyie,

Mnapima nguvu za Rais,kenge kweli nyinyi
Hiyo siyo nguvu ya sukuma gang huo ni upumbavu wenu wenyewe nguvu ya sukuma gang ipo kwa wananchi na wazalendo waliopo serikalini huyo zuzu ndungai sisi atumtambui hata kidogo ,
 
Hii busara ilitakiwa ianze kwa Supika kwenda kumuona Rais na kumpa dokezo kiuongozi, kwenda public na kuhoji huku ukikebehi "nchi itapigwa mnada" zaidi ya hapo unasema wataamua 2025 mkitaka kuweka wa kukopakopa, huku kulikuwa ni kupungukiwa busara kwa hali ya juu.

Na retaliation yake ndio hii watu msije kumuona Rais amekosea kumjibu public kwasababu yeye aliongea public basi naye acha ajibu public ndio waende huko ndani sawakamalizane, hauwezi kuharibu image ya mwenzako yeye akae amekuangalia tuu.
Hizi busars ndio Huwa zinatuumiza watanzania. Mtu amekupiga hadhari kama ni saizi Yako rudisha hapohapo. Alichofanya Spika ni kumchonganisha rais na wananchi.
 
Back
Top Bottom