Wale wabunge wana nafasi nzuri sana kwenye kuamua hili suala, ni either wapige kura ya kutokuwa na imani na Samia au kutokuwa na imani na Ndugai, kwao kuendelea kukaa kimya ni unafiki wasilete habari ya kulinda chama zaidi ya kulinda interests za nchi.
Kuwa na mihimili miwili isiyoelewana ni tatizo, kwa sababu yote hufanya kazi kwa kushirikiana, na kwa namna fulani inategemeana. Naona Samia ameaminiwa kwa kauli yake ya anajenga nchi hataki watu wamharibie, huu kwangu ni usanii tu.
Wakati yeye ndie aliekuwa wa kwanza kuwaambia wanawake wenzie 2025 ni zamu yao, kama alidhani alikuwa anapiga umbea kwenye kikao cha wanawake wenzie ajue wanaume walijua vita ndio imeshatangazwa, sasa apigane asijifiche kwenye kisingizio cha najenga nchi na kutaka kutumbua mawaziri wanaojipanga, anawaonea.