Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,479
- 2,877
Wakubwa, hoja zetu ni nzito kweli.Si mtego mgumu...lakini ni mtego mkali...
CCM kwa miaka yote imejitahidi sana kukwepesha na wakati mwingine kuahirisha milongas ya mihimili...
Kuanzia wakati wa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere na mjadala wa Uafrika na Uraia wa Tanzania hadi huu wa mkopo na Tozo wa Rais Samia. Migongano iliepushwa kwa kuzungumza kichama...
Sasa hivi kichama vitu haviendi na visingefika alipofikisha Rais Samia...kukataa msamaha alioomba Ndugai. Samia angeweza kutoa kauli ya kusamehe kama aliyotoa mtangulizi wake kwa waliomkosea wakati ule (mnakumbuka ya Kinana?). Mambo yangeisha kiutu uzima kwa kupiga picha na kunywa chai.
Spika ni mtu mzito sana Kikatiba...Rais ni mzito zaidi..hawapimani. Spika hana hata chipukizi wa kumlinda na mshale..Rais anaamuru majeshi...
Lakiki Samia yuko tayari kuandika historia ya kuwa Rais aliyemlazimisha Spika wa chama chake kujiuzulu kwa jambo la mitazamo midogo yenye kutofautiana kisera? Ni kweli tunataka kumuona Ndugai anatoka lango la Ikulubakitembea anageukageuka nyuma akijifuta jasho?
Kama Rais ni taasisi na Spika ni taasisi kama ilivyo kwa Jaji Mkuu. Tusiingie mtego huu. Wa kutegua ni Samia na si Ndugai.
Hekima itatamalaki? Ya nani?
Ila kwa namna CCM Rais ndiye mkiti wa Chama, katibu mkuu wa chama ni mteule wa Rais bila shaka inafahamika Rais akiamua kurea term ya pili kwa utamaduni wa CCM wataotoa form moja tu, na mchezo mzima unaisha.
Ambacho kinafahamika, Spika Job hana nia ya 2025 labda kama alikuwa mshenga wa mwingine? Je, Job ni mshenga wa nani mpaka hii "homa ya 2025" imempata mapema kiasi hiki?
Nikikumbuka Bunge la Spika Samuel Sitta au Big Sam, likikuwa na joto sana na kama ingekuwa ni enzi ya Big Sam, basi Madam SSH angeteseka sana; maana mzee yule sio tu angetoa kauli ila angeunda Kamati Teule kujua kulikoni chunguni?
Nakubaliana kabisa na ushauri wako, kuwa politics na diplomacy vinaendana, ni kama vile US na Russia wanakaa meza moja ila kila mmoja anakuwa na interest zake.
Ikitokea Executive branch akai-pin down Legislative branch kwa sababu ya "argument" na homa za 2025, bila shaka kama nchi tutakuwa tuna-set precedence ambao sio nzuri.
By the way, Mhe. SSH alitaka watu wafunguke na wapumue, na hoja ya Job mpaka sasa bado haina majibu, kwa kuwa tozo zilipitishwa ili tujenge mashule, mkopo wa 1.3 Tril mbona unafanya kazi za tozo?
So far, tunampongeza mama SSH kwa kukopa ili ku-push madarasa yajengwa haraka ili wanetu wasome, japo nadhani kuna haja ya kuongeza wanalimu na learning materials ili kujifunza kuwe na uwiano mzuri darasani na access ya learning materials ikiwepo.
Mijadala ni afya hasa kama ni mjadala wa wazi, na mikopo ni mizuri kama imelenga kujenga nchi kama ule wa 1.3Tril, suala ambalo ni vema wasaidizi wa madam SSH wakaja mbele, ni kuweka wazi fedha za tozo zimekuwa allocated kufanya nini maana tulipata mkopo usio na riba na tume-solve tatizo ili wanetu wakute kuna vyumba vya madarasa.
Mwisho, wizara ya fedha ndio inakopa kwa niaba ya serikali na Waziri wa kisekta asitake "kutuzuga" kuwa mwananchi hatalipa, ifahamike tu, hatakuja mtu kugonga mlango wa nyumba ila wananchi tutalipa kwa namna moja au nyingine, hivyo basi kwenye threshold ya fursa ya kukopa, tusifikirie tu kuwekeza kwenye majenzi, tukopo ili kukuza uzalishaji ambao return on Investment ni ya haraka, na multiplier effect yake inapimika na inaongeza cash flow.
Tukope ili kuongeza ukwasi TIB, TADB ili tusibaki tuna-import basics kama mafuta ya kula, sukari, mashuka ya hospitali, surgical cotton and bandages ila tuzifanye bank hizi zitukopeshe Watanzania kwa dhamana ya serikali, tuzalishe finished consumable goods snd service za kuuza sokoni, kwa namna hiyo tunaongeza tax base na watu wenye misuli ya ku-service mikopo pale inapo-mature.
Siku njema, tuendelee kujadiliana kwa staha, tusiraruane.