MTEGO; "Babe ukitaka tudumu kwenye haya mahusiano/ ndoa yetu basi kila mtu abakie na simu yake"

MTEGO; "Babe ukitaka tudumu kwenye haya mahusiano/ ndoa yetu basi kila mtu abakie na simu yake"

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,185
Reaction score
37,239
Habari za muda huu wazalendo wenzangu poleni na mihangaiko, harakati na purukushani za kuhakikisha mkono unakwenda kinywani.

Bila shaka hiyo sio kauli ngeni miongo mwa wanaojiita wapendanao ni kauli ambayo imekaa kibusara au kwenye kheri.

Hii kauli imevikwa muonekano wa hekima lakini ndani yake ina ushetani mkubwa wa matendo...

Mimi binafsi lishawahi kunikuta "Jambo" baada ya kuibeba kauli hii kwa jinsi inavyoonekana na so uhalisia wake.

Hii kauli ni kichaka cha waovu wanaotumia simu kama bunge la kuendeshea vikao vyao vyenye nia ovu.

Ni kauli inayoweka ulinzi wa mtu mwovu kufanya uovu kwa uhuru.

Chonde chonde mwenza wako anapohubiri sana kauli hii unatakiwa ufungue jicho la tatu kuyaona usiyoyatarajia.

"NZI WASIOTAKA USHAURI HUZIKWA NA MIZOGA"
 
"Ukitaka ndoa idumu" hiyo kauli mtu anaweza kula makofi, jukumu la kuifanya ndoa idumu ni la wanandoa wote sio mmoja, sasa huyo anayesema ukitaka idumu anakuwa na maana yeye hayuko kwenye nafasi ya kudumisha hiyo ndoa, kama ndivyo hafai kukaa kwenye ndoa.
 
Ukiona mtu kafikia hatua ya kukuambia hivi ujue ameshajua huna kauli juu yake au hata ukimuacha Hana Cha kupoteza.
Yaan mtu asipokuwa na hofu ya kukupoteza hukuambia lolote analojisikia
 
"Ukitaka ndoa idumu" hiyo kauli mtu anaweza kula makofi, jukumu la kuifanya ndoa idumu ni la wanandoa wote sio mmoja, sasa huyo anayesema ukitaka idumu anakuwa na maana yeye hayuko kwenye nafasi ya kudumisha hiyo ndoa, kama ndivyo hafai kukaa kwenye ndoa.
Kweli watu wanaoa kwa bahati mbaya
 
Back
Top Bottom