Mtemi Ng'wanamalundi (Mwanamalundi) - Yesu wa Afrika?

Tatizo unadhani ujio wa Bwana Yesu duniani ulikuwa kufanya miujiza tu.

1 Yohana 4:10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.

1 Yohana 2:2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.



Nimekumegea kidogo tu hapo.Ila fahamu Tito 2:11-14 "Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema."
 
OSIRIS....
Read about him.
 
Jamani ndugu hakuna mtu anacho hicho kitabu aki scan ukirushe hapa???

Mmenikumbusha kipindi ndo naanza kujua kusoma nilikisoma hicho kitabu cha[h=1]Mwanamalundi:mtu maarufu katika historia ya Usukumani[/h]
 
Sitaki kunfananisha mtu mwenye nguvu za kiganga na Bwana Yesu. Ng'wana malundi unaijua vizuri historia yake? Je unajua alipewa nguvu zake na mwanamke? Hebu nenda usukumani kwanza kamjue Ng'wanamalundi kisha uje hapa ukiwa kamili

Na huyo "nguvu" Yesu zake alipata wapi?
 

Yale yale, porojo za masimulizi za mababu wa kiyahudi!
 

Yale yale! Vitabu vya masimulizi ya mababu wa kiyahudi!
 

Hiyo sehemu balaa ukifika Magu lazima uijue tu!

Ila kwa kweli sungusungu walikuwa noma. Kuna ujambaz ulifanyika kwetu miaka ya 80 mwishoni wa kuteka basim, kuwaibia abria na kuwabaka abiria wanawake, fimbo zilitembea, basi kuna jamaa mmoja alipatikana mpaka akawtaja wahusika wenzake na jina la jambazi mmoja nalikumbuka hadi leo: Ng'wana Makolobela!
 

Kakolo = Kakondoo!
 
Ukienda Tabora baada ya Kipalapala kuna jiwe moja ambalo hulia kama ngoma. Nadhani ndio mahali ambapo watemi wa kinyamwezi huwa wanaskimikwa u-temi. Ni kweli kule Sengerema kuna jiwe lenye nyayo za Ng'wanamalundi pamoja na mbwa wake. Tulienda kuliona jiwe hilo zamani sana nakumbuka ni miaka ya 1980's. kwa sasa sijui kama bado lipo. Kaburi la Ngw'anamalundi kwa ninavyofahamu liko wilaya ya Kwimba, maeneo ya Ngudu ingawa binafsi bado sijafika kuliona.

Ukitaka kupata historia na maajabu ya watu wa Usukumani tembelea Bujora Museum. Ina mengi ya kusisimua sana.
 

Jitambulishe kama wewe ndiwe chenge, mnyantuzu mlozi wa bunge!
 

viliwahi kuwepo tena kwenye library za shule za msingi miaka ya 70 na early 80s.
 
Huwezi kumfananisha BWANA YESU na mwanamalundi kwani Yesu Kristo ni MUNGU ila alikuja ulimwenguni akiwa na umbo la kibinadamu kuwafundisha wanadamu na kufisha umbo la kibinadamu kwa ajili ya dhambi za wanadamu nikiwemo mimi labda swali kama liko kwamba ni kwa vipi yesu ni Mungu haya hapa: 1..... Wafilipi 2:5-11 hapa tunapata maelezo jinsi Yesu alivyojifanya mwanadamu na ktk mstari wa 11 tunaambiwa kuwa kila ulimi wapaswa kukiri kuwa Yesu Kristo ni BWANA imeandikwa kwa herufi kubwa na kama una biblia ya union version ya kiswahili nenda kabisa kule mwanzoni uone maana ya BWANA inapoandikwa kwa herufi kubwa bila shaka utakuta kuwa hilo ni jina takatifu yaani JEHOVA kama linavyoitwa kwa kiyaudi. 2.....sababu ya pili kuwa Yesu ni Mungu soma Isaya 9:6 " kwa ajili yetu mtoto amezaliwa.............. Ataitwa mshauri wa ajabu,[MUNGU MKUU], BABA WA MILELE, mfalme wa amani. 3....sababu ya tatu angalia 1timotheo 3:16 "bila shaka siri ya utauwa (uchamungu) ni kuu,Mungu alijidhirisha ktk mwili...... Akaönekana na malaika,akaubiriwa ktk mataifa......" 4.....sababu ya nne tazama sisi wanadamu tunapokufa tunaamini ya kuwa Mungu ndiye anatoa roho zetu lakini tazama Yesu aliitoa roho yake mwenyewe Yohana 19:30 takiriaani bibli nzima pamoja na histori yake ilishuudia ujio wa Yesu kristo katika mwili lakini ni umoja pamoja na Baba, na Roho mtakatifu uwezi kutenganisha nafsi hizi 3 tazama 1 Yohana 5:7-8 CONCLUSION: KAMA UNAAMINI KUWA MUNGU (YESU) ALIKUUMBA NA BAADAE KUJITOA KUKUOKOA BURE HUWEZI KUMLINGANISHA NA HUYO MWANAMALUNDI AMBAYE AMEOZA KABURINI AKISUBIRI YESU ARUDI NA APATE UJIRA KADIRI YA MATENDO YAKE. WITO: Matendo ya mitume 4:12 "wokovu haupatikani kwa mwingine, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu litupaso sisi kuokolewa kwalo isipokuwa Jina la YESU" JE UNAKUBALI KUMPOKEA YESU KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WAKO? Kama jibu ni ndiyo basi Mungu azidi kubariki na weka uamuzi wako hapa watu wasipotoke na huyo mwana (mtotomalundi)
 
Jitambulishe kama wewe ndiwe chenge, mnyantuzu mlozi wa bunge!
Hahahaha Mkuu mi nashida na kitabu kinachoelezea historia ya huyu gwiji wa kisukuma. Huyo Chenge mi hata sijawahi kuonana naye uso kwa uso!!
 
Yale yale, porojo za masimulizi za mababu wa kiyahudi!
Ahsante mkuu kwa comment nzuri. Niliwahi kufanya kazi na wayahudi, pamoja na kuamini kuwa wayahudi wamebarikiwa, lakini ni wachawi mbaya. Kuna kipindi walikuwa wanakuja na hirizi kujaribu kwa mmoja wa wafanyakazi, ambaye ataisikia inapumua basi anakaa nayo.
 
Mkuu haya yote unayajua kwa sababu wenzetu waliwahi wakaandika na kutunza kumbukumbu, lakini kwa vile sisi akina MWANAMALUNDI hawakuweza kuwa documented na kupewa heshima za kuwa na wafuasi kama ilivyokuwa huko ulaya na sehemu zinginezo, basi tunaamini moja kwa moja kuwa Bwana Yesu ndiye aliyekuja ulimwenguni kututangania utukufu wa aliye juu mbinguni. Hilo mimi sina shaka nalo, tatizo linakuja namna historia za hawa akina Mwanamalundi kufanana kimatendo na bwana Yesu kristo, je huoni kuwa Mungu alikuwa na lengo lake katika kila pembe ya dunia pengine kuwa na mwakilishi wake?
 

Wa-Ukenyenge,

Yaani ukijaribu kuwaelewesha watu kwamba biblia ni masimulizi tu ya hadithi na mapokeo ya mababu wa kiyahudi kwa vizazi vyao, sidhani kama kuna watu watakuelewa. Yaani kwao biblia ni NENO la Mungu. The same applies to Quran. Ni kwamba jamii hizo waliweza tu kuweka katika maandishi masimulizi hayo na kwa vile historia imemnyima mtu mweusi kusambaza tamaduni na imani zake kwa jamii nyingine basi kwa wengine nguvu na masimulizi ya weusi ni uchawi na urozi na ushirikina!

Ni ajabu zaidi mpaka kwa weusi sis wenyewe kuamini hivyo!
 

Nimeipenda hii. Big up.
 

Perfect! safi sana. natamani ningekuwa ni mimi nimeiandika hii.
 

Ibambasi,

Hapo umeongea. na ikumbukwe kuwa hawa watu brown 'wazungu' madhumuni yao makuu kuleta dini ilikuwa ni kutupumbaza ili watutawale KIURAHISI, ndiyo maana walifanya kila linalowezekana kuzifutilia mbali mila zetu na desturi zetu kwa KUTUJAZA WOGA wakituhubiria na wakisema kama tutaendelea kuzifuata basi tutegemee kukumbana huko mbeleni na moto wa 'moto wa milele'.

Ibambasi,
Kumbukumbu zilikuwepo lakini hawa wamishionari waliwarubuni wazee wetu wazichome motto na kuzisahau, ndiyo maana zilizobaki ni zile ambazo hawakuweza kuzifutilia mbali kama nyayo za hao magwiji kwenye milima.

Hawa viumbe wa brown walifanikiwa sana, athari zake mpaka leo hii zinajionesha. utamsikia 'mbongo' eti anakwambia huo ni ustaarabu. mimi ninasema huu siyo ustaarabu bali ni ugonjwa uliopandikizwa wa inferiority complex
 
Reactions: amu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…