Ni kweli dear halafu hii haina msimu.mikungu pia inatoa majanii mengi tu.
Ni kawaida ya miti kipindi cha kiangazi kupukutisha majani, sidhani kama kuna mti ambao haufanyi hivi.
Ila huo mti mharadari ni kweli unatoa majani mengi na vimatunda vyekundu ambavyo vinachafua sana.
Huyu bonge kwenye picha anayezoa uchafu ndiyo wewe? Unaonekana uko m-cute sana! Hiyo miti kwenye picha ndiyo miharadali? Kuna mtu alinishauri na mimi nipande hiyo hiyo! Lakini kama unayosema kama inapukutisha majani sana basi ni hatari. Huku kwetu kuna miti wanaita Midodoma inakaa mwaka mzima iko green ina kivuli kuzuri sana! Sijawahi kuona majani yake yaliyodondoka!Habari zenu wakuu.
Naomba msaada wa kuelezwa mti mzuri unaoleta kivuli lakini usio chafua mazingira kwa majani/vitunda.
Kwa sasa tuna hiyo miti pichani,ina kivuli na inaleta hewa nzuri ila tunataka tuikate tupande mingine maana hii kwanza inapendwa na popo ambao huharibu mazingira kwa kinyesi chao kwenye kuta za majengo na pia inamwaga majani mengi kiasi kwamba eneo linaonekana kama halisafishwi.
Vile vile nasikia(not sure) haifikishi miaka 10 inakufa.
So wakuu,naomba anayejua mti wowote mzuri wa kivuli hata ukiwa wa matunda anitajie mradi tu usiwe wa kuchafua kwa majani.
Natanguliza shukrani🙏View attachment 2687597View attachment 2687603
Mpera achana nao ule unadondosha majani sana! Kwa mwembe sawa kabisa hata ukidondosha majani unaweza kuyaokota tu!Asante mkuu.
Hata mie niliwaza muembe au mpera ila sikua na uhakika.
Majani ya miti yaliyoanguka pia ni urembo kwenye nyumba. Yanaonyesha uhai kwenye mazingira yako.Sijui unaitwaje ila sidhani kama miti yote inamwaga majani mengi kama hii.Kuna picha nimeweka hapo juu,hayo mafungu ya majani yamejikisanya masaa mawili baada ya eneo kufagiliwa.Upepo ukivuma yanasambaa kila sehemu.
OkayPoa asante mkuu.
Usisahau please[emoji120].
Mamiti ya hovyo sana haya,hata sisi tunayakata
Kivuli chako tu mi hoiiii,njoo pm basi nikuelekeze mti mzuri utakaokufaa
Sawa.Aysee! Hicho kivuli tu,sijui real itakuwaje!
Kuna mada flani aliieta sijui ni Mshana Jr sijui nani inahusu mambo ya miti miti,miti inayotakiwa kupandwa majumbani na mingine isiyotakiwa kupandwa majumbani kwamba ina nuksi na maniaje niaje mengine kibao!! Ukiipata ile utakutana na mengi! Watu walifunguka sana kuhusu mambo ya miti mule! Kama vipi ngoja tumuombe Mshana Jr aje ailete achungulie na kivuli kidogo😎
Usipande hii utajuta.Huyu bonge kwenye picha anayezoa uchafu ndiyo wewe? Unaonekana uko m-cute sana! Hiyo miti kwenye picha ndiyo miharadali? Kuna mtu alinishauri na mimi nipande hiyo hiyo! Lakini kama unayosema kama inapukutisha majani sana basi ni hatari. Huku kwetu kuna miti wanaita Midodoma inakaa mwaka mzima iko green ina kivuli kuzuri sana! Sijawahi kuona majani yake yaliyodondoka!