Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Okay.Ni kweli mkoramaji ni mzuri ila sasa mpaka uje utoe kivuli cha kueleweka sio leo. Unaeza subiri 5 years bado kivuli kinasua sua.
Kuna mtu kashauri mstafeli, ila kwa mimi sijawahi kuona mstafeli wenye kivuli. Hua inanyooka tu kwenda juu. Pia mimi mistafeli niliikata baada ya kuniletea ule ugonjwa wa wadudu weupe ambao nahangaika nao hadi leo.
Ushauri wangu tafuta miashoki dume. Hakikisha ni dume maana jike ndio ile hunyooka na kurefuka sana. Miashoki dume inaangusha majani kidogo sana, haina matunda, ina kivuli kizuri, na haichukui muda sana kuota.
Ndio.Okay.
Ukimuambia muuza miti anipe muashoki dume ataelewa tu mkuu?
Kweli hii miti popo wanaipenda ni miti poriinapendwa na popo
Miti tunayoiita Midodoma ni kama hii kwenye picha, bahati mbaya nimepiga usiku sina hakika kama inaonekana vizuri. Lakini kikubwa unachopaswa kuangalia ni hiyo morphology ya canopy cover maana ndicho kivuli chenyewe. Hapo ina kama miaka mitatu!Ndo huo hapo?
Sijawahi kuuona.View attachment 2688263