Ni kweli mkoramaji ni mzuri ila sasa mpaka uje utoe kivuli cha kueleweka sio leo. Unaeza subiri 5 years bado kivuli kinasua sua.
Kuna mtu kashauri mstafeli, ila kwa mimi sijawahi kuona mstafeli wenye kivuli. Hua inanyooka tu kwenda juu. Pia mimi mistafeli niliikata baada ya kuniletea ule ugonjwa wa wadudu weupe ambao nahangaika nao hadi leo.
Ushauri wangu tafuta miashoki dume. Hakikisha ni dume maana jike ndio ile hunyooka na kurefuka sana. Miashoki dume inaangusha majani kidogo sana, haina matunda, ina kivuli kizuri, na haichukui muda sana kuota.