Je, Adamu na Hawa walikula tunda gani?
(Wengine husema ni tunda la ndoa)
Magonjwa, dhiki, mahangaiko ya maisha na kifo ni matokeo ya dhambi waliyoifanya wazazi wetu adamu na eva katika bustani ya edeni. Biblia hielezea dhambi hiyo kuwa ni kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya uliokuwa katikati ya bustani hiyo. Wasomaji wengi wa biblia hutofautiana juu ya nini hasa kilikuwa tunda hilo, wengine wakisema ni tendo la ndoa. Mwanateolojia titus amigu anachambua utata huo akijibu swali la bw. Goti chiwambo wa s.l.p. 911 songea juu ya suala hilo.
Ufalme wa kiakili ndilo tunda aliloonyeshwa Eva na Shetani kichwani na moyonimwake. Basi Eva alipofikiria juu ya manufaa ya ujuvi au ufalme huu wa kiakili moyo wake ulitamani akaona wafaa kuliwa kwa vile ulipendeza kiakili.
Hapo akaendelea na hatua ya kuchuma tunda kile hicho ni kitendo gani? Hicho ni kitendo cha kuupokea uzuri na ujuvi huo au uzuri wa ufalme huo wa kiakili moyoni au nafsini yaani kulileta nafsini ndiko kulichuma na kulikumbatia moyoni ndiko kulila.
Hivyo basi tangu kuliona tunda lile hadi kulichuma na kulila, mambo au vitendo vyote vinetendeka kiakili hazikuwa habari za tunda lenye kugusia kama papai , chungwa au ndimu, Tuendelee mbele.
Baada ya kulila mwenyewe, Eva alimsimulia Adam juu ya suala hilo la kiakili pevu la ufalme na madaraka kamili ya kiakili.
Huko kumsimulia Adam habari hiyo ndiko kunakoitwa ''KUMPA ADAM TUNDA'' Naye adamu kwa upande wake alipoelewa na kutia moyoni habari hiyo ya ufalme au mamalaka kamili ya kiakili ndiko kunasemwa ''NAE AKALA" .
Kwa kifupi ndugu maluli hilo tunda si tunda kama tunda ila ni zao la mti wa kiakili yaani akili peve kabisa ambalo ni ule ufalme wa kiakili au mamalka kamili ya kiakili.
Kuliona tunda ni kule kubaini uzuri wa tunda lile la kiakili na kulichuma ni kule kuhamishia ufalme huo wa kiakili kwenye moyo binafsi.
Kulila tunda hilo ni kule kuweka moyoni au akilini ufalme huo wa kiakili na kumpa Adam ni huko kumsimulia Adam habari za ufalme huu wa kiakili na kula kwa Adam ni huko kulipokea yeye binafsi neno hilo na kuliweka pia moyoni au nafsini mwake.
Ndugu Kanyoto watu wengine hung'ang'ania tafsiri kwamba tunda lililoliwa ni ''TENDO LA NDOA'' HII NI TAFSIRI POTOFU .Fikiria hoja au mambo matatu ambayo sasa ninataka kukuambia.
(I)Ashakum si matusi Eva alichumaje tunda ambalo liko mwilini mwake mwenyewe? Kuchuma maana yake ni kutwaa kitu toka mahali kilipotundikwa na kuleta mahali pengine. Eva asingeweza kwa mwili wake mwenyewe
Aidha alikulaje tunda hilo kabla ya kumshirikisha Adam hali yeye ni jinsia moja pakee yake? TUSIENDE KWENYE MATUSI hakuna heko wala misingi yoyote ya kimaendeleo.
(II) Fikiria viungo vya uzazi utavielezeaje kama ni mti wa ujuvi wa mema na mabaya? Mbona ahera picha hiyo ingekuwa ya kichwa cha binadamu ambacho kinaweza kutambua mema na mabaya.
(III) Zaidi ya vichekesho hivyo vyote, tendo la ndoa kati ya Adamu na Eva vilisharuhusiwa kwao kama tunavyosoma katika Mwanzo 1:28. Yaani walipata ruhusa ya kufanya kitendo hicho hata kabla ya dhambi yao katika sura ya 3:6-7; wanapoonekana wana kosa.
Wao walifunganishwa ndoa na Mungu mwenyewe pale aliposema katika sura 1:28. "Zaeni Mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha, "Jiulize tu; ndugu Kanyoto. Jiulize kidogo tu. Wangezaaje bila kuruhusiwa na tendo la ndoa?
Basi walisharuhusiwa, hivyo kulifanya kusingekuwa haramu ya laana kubwa kama waliyopewa.
Basi ni wazi tunda halikuwa tendo la ndoa maana ilishakuwa halali kwao kama bibi na bwana. Basi walifanya kitu kingine, ndicho kuchuma na kula tunda ambalo nimekwisha kulieleza; NI ULE UFALME NA MADARAKA YA KIAKILI ili wawe huru zaidi au sawa na Mungu mwenyewe.
Ndipo hao watu walitambuana kuwa ni watu wawili wa jinsia tofauti. Mwandishi hafichi; ila anasema, japokuwa walikuwa uchi, hawakuona haya yoyote. Hilo lisome kwenye Mwanzo 2:25; sura ambayo imetangulia hiyo ya 3 inayosimulia dhambi ya kula tunda lililokatazwa.
Nimalize jibu kwa Angalia; nakufahamu tafsiri ya kwamba Adamu na Eva walifanya tendo la ndoa hali ambayo inachochewa na maelezo kwamba waliona haya; wakashona majani na kujifanyia nguo.
Tafsiri hii iache kwani si sahihi kwa sababu haioani na maelezo yaliyotangulia; na zaidi ya hayo, inapotoshwa sababu ya akina Adamu na Eva kuona haya na kujifanyia nyuo za majani.
Ukweli ni kwamba kutokana na kuvunja uhusiano wao na Mungu, usawa ulikuwapo kati yao ulivurungika pia. Kwa hiyo wakaona tofauti ya kijinsia kwa kiwango cha juu hali yao kuwa wadogo sana mbele ya Mungu, wanaionja kwa kipimo kingine sasa.
Basi wanajisikia uchi wao kwa wao ndio maana wanajifanyia nguo za majani; na wanajisikia uchi mwingine mbele ya Mungu. Yaani kukosa heshima na hadhi mbele yake Mungu mwenye haki na mapendo na ndipo wanajificha kati ya miti ya bustani.
Ndugu Kanyoto; hilo liwe wazi kuwa mkosefu hujisikia uchi mbele ya Mungu na watu.
Mkosefu yeyote hujisikia kisaikolojia yuko uchi mbele ya wengine wasio na hatia.
Fikiria inakuwaje baada ya mtu kushikwa wizi au mtu kwa mtu mwingine. Unaona mtu yule anaonja kabisa kwamba bila shaka watu wengine wote wanamfahamu na yeye kihadhi, ameshuka; amekuwa mtupu; hana kitu cha kumhifadhi.
Kumbe tukirudi tena katika tatizo hilo la Adamu na Eva, hapo kabla uhusiano wao haujavurugwa; ule uhusiano na Mungu. Wao walionja usawa kamili kati yao ndiyo maana Adamu hakujisikia vibaya kuwa na jinsia nyingine tofauti palepale au Eva ndivyo alivyoweza kuhimili kujisikia vizuri mbele ya Adamu bila ya kujihifadhi kwa nguo yoyote.
Kwa sababu hiyo, hawakuoneana haya na kuhitaji nguo yoyote. Lakini baada ya uhusiano wao kuvurugwa, wanaonja tofauti zao kwa sababu ya ubinafsi na kwa sababu ya kuteremka hadhi na jitihada za kujirejeshea usawa kati yao; zinakuwa ndiko kujishonea nguo zilizolingana na majani; lakini wapi walishakuwa wamechelewa.
Mtengano kati ya Adamu na Eva kueleza unajidhihirisha katika jibu la Adamu na ksema kwa ubaguzi, na kwa kumtenga mkewe kwa kusema, "ni huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nani, ndiye aliyenipa matunda ya mti huo; nikala."
Maana yake, Adamu anamuona Eva sasa kama mtu tu; aliyeletwa pale; si mwenzi wake mshirika. Basi, uchi wa akina Adamu na Eva ndiyo hayo yanayoendela mpaka leo tunapobaguana kijinsia pale ambapo wanaume, watoto wa Adam wanapoendelea kuwaona wanawake kama watu walioletwa na kama watu ambao wamepewa tu wewe pamoja nao lakini si wenzi wao halisi,
Haya ndugu Kanyoto tusitamani ufalme wa kiakili au madaraka halisi ya kiakili bila kumruhusu atutawale kwa enzi yake madhara yake ni makubwa kwa sasa hivi , wanaume na wanawake sisi tu sawa kwa asili yetu na kwa sababu hiyo hakuna sababu ya kubaguana .