Mti waliokatazwa Adamu na Hawa kula ulikuwa mti gani?

Mti waliokatazwa Adamu na Hawa kula ulikuwa mti gani?

Ufunuo 2:7b Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.

Mungu aliwapa chaguo la kutii ama kutokutii, kwa kuweka Mti wa Mema na Mabaya, kama tujuavyo zao la mti ni tunda, tunda la mti walilo kula ( halikua tunda lenye kumpendeza Mungu) halikua tunda tunda la Roho bali tunda la yulemuasi wa Mungu. Ni somo pana sanahili
 
sasa jiulize tunda gani walikula ?

Ujue kwenye hilo suala la tunda kila mtu ana tafsiri yake lakini hakuna ambaye ana uhakika sana kilikuwa ni kitu gani walifanya... Ila labda nikukumbushe kitu kwenye mafundisho tunaambiwa kuwa kwenye lile shamba kulikuwa na miti ya aina mbalimbali mfano mti wa uzima(ambao INASEMEKANA wangewahi kuula hata baada ya kutolewa shambani kwa UTOVU wa nidhamu bado wangeweza kuishi mpaka sasa na vizazi vyao pia) na ule waliokula(waliokatazwa) uliwafanya wagundue wapo uchi(hapa tunaweza kusema walikula mti wa ufahamu wa mema/mabaya)....

Mie kwa mtizamo wangu mwenyewe ninaweza kusema kuwa ni mpaka mtu aweze kufunuliwa na roho mtakatifu ndipo anaweza kupata ufahamu ulikuwa ni mti gani vinginevyo wengi wetu tutaishia kukisia kisia tu mambo kwa kuwa hakuna mwenye uhakika kabisa kwenye hili jambo....
 
Ngoja nianze maombi nifunuliwe mimi ..sasa je jamii itakubaliana na mimi
 
Mi kwa ufahamu wangu mimi naona Mwenyezi Mungu aliamua kuwapa mtihani wa kutokula tunda kwenye huo mti ili awapime kwa imani kama viumbe wake wanamtii...
 
Yani mtaandika mpaka basi but kulijua tunda msahau,huwa halieleweki ni lipi hasa.
 
Kwa hiyo mnaamini kitu ambacho hata hamkijui, maana sijaona consensus kwenye hiyo ishu, wengine wanasema ni tunda la kawaida, wengine wanasema ni ngono, wengine wanasema ni figure of speech kwamba walipewa tu choice ya kuchagua kumtii Mungu au kutomtii. Which is which?
 
Mungu nimwema leo nimepata majibu kwamaswaliyangu yamuda mrefu.
 
Kila mtu anajibu lake wapo wanaosema ni apple sababu ya utamu wake ukienda mbeya (uyole na inyara) wanaona inaweza kuwa ni mikusu sababu ni mitamu balaaa ukienda njombeh wanadai ni peazi...dodoma wanasema zabibu.......kazi kupata jibu.
kule kwetu lushoto wanasema ni "komamanga"kiswahili sijui wanalitaje hilo tunda.
 
kama kweli waliruhusiwa kabla kwanii watoto walianza kupatikana baada ya tunda kuliwa?
 
inasemekana hata mtoto wa kwanza mwenye jina la kaini hakua mtoto halali wa adam na ndio maana alikua na roho mbaya na ndio kizazi kilichoendelea mpaka leo
 
inasemekana hata mtoto wa kwanza mwenye jina la kaini hakua mtoto halali wa adam na ndio maana alikua na roho mbaya na ndio kizazi kilichoendelea mpaka leo
Mama weeeee... Alikua mtoto wa nani..!?
 
Back
Top Bottom