Walimu siku zote wako nafasi nzuri ya kuwa na nidhamu, na ndivyo wanavyofundishwa ili kwa nidhamu hiyo wawalee na kuwakuza vyema watoto wetu. Asingeweza kujibu mapigo kama ambavyo wewe ungefanya. Pengine angejibu ungesikia kapigwa risasi maana OCD bila shaka alikuwa na bastola kiunoni, na habari ingekuwa "Mwalimu apigwa risasi alipomshambulia OCD" na hadithi nyingine nyingi za kumchafua. Nadhani hapo tuangalie uhalali wa OCD kumpiga eti kwa kosa la kutoonyesha Strong Room ambayo HAIPO na sio mwalimu Mkuu aliyepaswa kuijenga ni Serikali ya Halmashauri yake iliyotakiwa kuweka mambo yote muhimu katika shule hiyo. Sasa OCD anapomshambulia Mwalimu kumjeruhi na hadi kumchania nguo, kweli huo sio Unyanyasaji????? POLE SANA MWALIMU, POLENI SANA WALIMU WOTE. Imenikumbusha machungu ya Mwalimu aliyechapwa bakora mbele ya wanafunzi wake na Mkuu wa Wilaya maeneo ya Kagera.