Mtihani wa usaili wa Tax Officer (TRA) wavuja

Hahahahah usicheze na hii system ya ajira bongo! Kilichompata jamaa ni kibaya sana kwa mtu kufanyiwa ila kwa status jamaa anaonekana tu ni mtoto wa mkulima yani!Wamemchukulia mkolomije tu maana hana mtu anamjua 😅😅😅 wakamfanyia u borne town!

Sasa kama huna link hata na mtu mmoja mzito unatoboaje kwenye huo msala? Maana kimsingi hapo ulitembea waya tu kutoka juu 😅😅😅 “kwanini dogo mumemfelisha mtihani bila sababu? Nahitaji apewe hio nafasi mara moja kabla sijaja huko ofisini na pia nitawasiliana na mama pale ikulu nimueleze hizi tabia zenu za viburi”
 
Ndio mbinu hizo ikibidi ulokote desa😅😅😅
 
Na dhamira ya kufanya analog ni kuwa kuna fungu linapigwa na wote watakaochaguliwa kusimamia zoezi hilo!😅 Allowance ya nauli,kula na malazi 😅😅😅 hivyo wamewagueza wasaka ajira kama mradi wao!
Si wanatakiwa wasahiliwe ama wasaka fursa Kama mie nimetokea kigoma kuja dar nilipwe gharama zangu i.e nauli malazi na msosi? Mana Kuna kampuni wanaojielewa wanafanyaga ivyo?

Binafsi I know value ya muda wa mtu.
Kuna mud Fulani nilikuwa nafanya finishing ya house ,kigae,rangi,gypsum board naita fundi Kama watatu kwa kila ishu so nafanya comparisons.
Ila nilikuwa nawatoa nauli zao walizotumia.aliyekuja na boda yake nampatia ya mafuta.
Namwambiaje huu ni usahili so usipochaguliwe usije ukasononeka.
Mana I felt it too!! So I never wanted someone to feel it how I felt it
 
Kuna utofauti kati ya kufanya mambo kwa adabu na kufanya mambo hovyo bila kujali
Na aliyefanya bila kujali ni huyo aliyepewa pepa halafu baada ya mthni akausambaza, kama n mimi ningepewa hilo pepa hata demu wangu nisingempa
 
Hii nchi kama baba yako alikuwa mzembe miaka hio ya 70 hakusoma akashika nafasi nzuri serikalini au akafanya mabiashara na kujiwekeza sana ujue inakula kwako mazima as a child!

The Struggle is fuckkin real,kitaa kinasulubu kiroho mbaya!
Nakazia..
Ila watakuja hapa watakwambia pambana[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nakazia..
Ila watakuja hapa watakwambia pambana[emoji23][emoji23][emoji23]
Kupambana sio sifa bali unatakiwa ufanikiwe 😅 kwanini upambane wakati rasilimali zote zipo wazi kwako! Una right connections unapambana vipi sasa wakati mambo yanajiseti tu!

Kupambana sio jambo rahisi kwa hali ya sasa ya maisha!
 
Ndio mbinu hizo ikibidi ulokote desa😅😅😅
kaka maisha n mapambano magumu yanayohitaji ukatili na fitina inapobidi, hapo utumishi kama una mwanao yeye ndio mshika password ya kuingia kwenye kisanduku cha marks ukishindwa kuingia oral interview basi milele utalalamika kama Manara. yaani kumwambia tu "oyaa wee nina 10% ebu iongeze ifike 60%"
 
Nami pia ni muhanga wa iyo tume ya ajira,mwezi wa tano nilikuwa hapo dodoma mwajiri alikuwa ni Tanesco,nilichokutana nacho sintakuja tena kuaribu hela yangu kwenda saili zao,yaani nimefika ndani kuna kuna watu walikuwa wameingia na majibu kabisa kwani majibu unajibia kwenye karatasi za rimu ambazo hazina chata yoyote,mie nabaki kufikiria jinsi ya kujibu kuna mtu anatoa karatasi lake anabandika juu ya meza kisha anatulia anaanza kuwachora tu nyie mnaosumbua ubongo,nikavulimia kutoka nje nakutana na jamaa nilisoma nae chuo anacheka anaanza kuniambia paper nawe ulipata nabaki kushangaa tu.
kiukweli kabisa utumishi wanazingua sana tena sana,Mungu atusaidie tu kutuweka hai na kututendea haki yeye sie tutokao familia za kimasikini
 
Mkuu utateseka sana na hizi Biashara Kichaa ,tafuta shughuli nyingine mkuuu

Utapoteza muda bure mkuuu.
Mambo ya Utumishi ni miyeyusho tupu Mkuuu.

Check sasa umepoteza 200K kwa mambo ya kijazebend

Mimi nishaachaga hizo Biashara

Naomba alafuu nikiitwa siendi hataaa
 

Hahahah ila mwanangu unachekesha kichizi katikati ya majonzi Hahahah,yule mwana akikaa vibaya hata barabarani watamuondoa tu.

Kuna comment iliandikwa kwny huo uzi ‘Oyaa huyo jamaa aachane na hio nafasi la sivyo watambakia kesi huko kazini akienda’ mwamba nae akajibu ‘kufungwa jela sio tatizo ninachotaka mimi ni nafasi ya hio kazi tu,jela iko kwa ajili ya watu’ Hahahah.
 
Kweli maisha hayana huruma kabisa na mtu ina maana kuna mahala lazma utatumia ukatili maisha ni vita 😅..

Ukiwa na right connections maisha yanakuwa mepesi kama unyoya wa njiwa 😅 utafelije na mgawa marks ni mwanao!
 
😅😅😅😅😅😅😅 jamaa anajifanya kamanda kuliko hata Waziri! We imagine waziri mwenyewe kasanda unafikiri kuna force kubwa kiasi gani behind that maana ujumbe umeshaenea hapo!

Ni utekelezaji ila Waziri na genge lake wameichunia wanampiga kalenda tu za kwenda na kurudi!

Kitakachofuata atalimwa barua tu moja akiendelea kung’aa ng’aa sharubu ofisini kwa watu atasema na keko 😅! Umafia tu ndio last option dogo atapotea bora achune tu.
 
Unawainjoy tu 😅
 
Kweli maisha hayana huruma kabisa na mtu ina maana kuna mahala lazma utatumia ukatili maisha ni vita 😅..

Ukiwa na right connections maisha yanakuwa mepesi kama unyoya wa njiwa 😅 utafelije na mgawa marks ni mwanao!
mimi interview yangu ya 1 nilifika hapo sina connection yyte, nikiwa maeneo nimekula kasuti kangu uchwara likaja kundi la watu. lile kundi likawa linasema like "swali fulani na fulani tayari bado fulani, hints za maswali matatu yote yaliganda kichwani nikawageukia nikawakazia macho wakaogopa wakasepa. mzee nilienda kukesha na hints 3 kesho kwenye pepa maswali yote niliyakuta nikatia above 80 huko. maajabu kwenye oral zile sura sikuziona hata moja, nikamkumbuka mwana fa aliwahi kusema "unaweza kulala na bi harusi na usiwe bwana harusi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…