Mtikila: Hili bunge la katiba limejaa wahuni na washenzi sijawahi kuona toka tupate uhuru

Yeye awezi kusema kitu bila uchunguzi, ukiona ameongea hivyo ujue amefanya uchunguzi wa kina, na ukitaka kujua kwanini amewaita washenzi muulize atakufafanulia, kumbuka huyu ni mtu wa mungu hivyo basi he thinks beyond!
 

we mwalimu wako wa hesabu alikuwa nani?
 
Mtikila ndiyo mhuni namba moja, anafanya siasa za maigizo, ana chama cha siasa ambacho hakijuikani kipo kwa maslahi ya nani, yeye siasa zake ni mahakamani, kama angekuwa mwema, angeungana na wanamapinduzi wa kweli, lakini cha ajabu, mara kadhaa amekuwa akitumika na ccm kutoa kauli zenye utata kwa wanamapinduzi, rejea kauli aliyotoa kuhusiana na bomu lililorushwa kwenye kufunga kampeni za Chadema pale Arusha, waganga njaa tu hawa.
 
Kwa hiyo na yeye ni mmojawapo maana naye yumo miongoni...
 
Mtikila ni zaidi ya CHADEMA!

Mtanisamehe kwani kwenye posho,hakuna tofauti ya wapinzani na chama tawala!

ukiongelea posho usitaje vyama,sema wabunge wote ktk swala la posho wanakuwa mbogo.wakitoka nje wanajifanya ni wapiga kelele kweli
 
hujamalizia usemi WA Mtikila kua
"Haiwezekani 95% ya bunge la katiba liundwe na wanasiasa ambao Tanzania hii hawazidi hata milion Tano. halafu Watanzania walio wengi wawe na 5% tu ya uwakilishi. watanzania wamenyimwa uwakilishi wa kutosha
HIVYO TUTAENDA MAHAKAMANI NA TUTASHIDA! !!"
 
ungeanza kabisa na Abdu Jumbe, maana yeye alianza kudai Tanganyika irudi tangu mwanzoni mwa miaka ya 80's.
 

Mkuu umefunga thread.
 
Katika watu ambao nawaamini ni Mtikila, huyo ni muasisi wa Tanganyika
na naamini wakimsikiliza atatoa mchango sahihi hao wengine ni macho fedha tu

hana lolote hao
 
Kikwete ni mnafiki ndiyo maana hata Lowasa ana hasira naye ni mtu gani anayeshindwa kuheshimu
wananchi? unateua wabunge wa bunge la katiba ambao ni watu wako kwani hakuna walimu nchi hii

mimi naamini angeteu walimu waganga na wakulima bunge lingekuwa halina malalamiko ya wananchi
kikwete ni lazima atapata matatizo baada ya muda wake mtu gani anakuwa na mipango ya chini chini
 
Kama unamkubali Mtikila mwenye chama chenye usajili wa kudumu ingawa wanachama wote alionao hawafiki 150, basi unamatatizo makubwa.

Wengi wetu tunampenda Rev. Mtikila kama mwanaharakati na mpigania haki za binadamu na sio mwanasiasa...ndugu sio wote wanapenda mtu kwa sababu ya mvuto kisiasa kama wewe..
Hivi unajua kama isingekuwa juhudi zake Rev. Mtikila leo hii watanganyika tungekua tunaingia Zanzibar kwa passport...!!
Hivi unajua kama sio Rev. Mtikila leo hii swala la mgombea binafsi lisingekuwepo kwenye rasimu ya katiba...??
Hivi unajua kama sio Rev. Mtikila kupaza sauti ya utanganyika wetu swala la Tanganyika na utanganyika wetu lilikua linaenda kupotea wakati Zanzibar na uzanzibari unaendelea kushamili kwa kasi..
Yapo mengi na mengi Rev. Mtikila ameyapigania for public interest na sio political interest..
Nadhani we humjui vizuri Rev. Mtikila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…