hivi huyu ni mchungaji wa nn vile!!!??
wa siasa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hivi huyu ni mchungaji wa nn vile!!!??
Bunge la kutaka tu potsho kubwa badala ya kuangalia kilichowapeleka kujadili. Huyo mbunge aliyetoa hoja hafai kabisa kuwa mbunge wa nchi hii. Nasema kwa sababu yeye anataka kubomoa badala ya kujenga.Hizo 300000 kwa siku kwa mda wa siku 30 ni millionaire 18,000,000. Hii ni sawa na mshahara wa mtu wa sh.300,000 kwa mwezi kwa mda wa miaka 5. KAMA MSHA
HARA WA MTU MMOJA KWA MIAKA MITANO ANAPEWA MBUNGE POSHO KWA MIEZI MIWILI TU AMBAYO NI MILIONI 90 KWA MWEZI HALAFU BADO ANALALAMIKA KUWA NI KIDOGO. JE, HUYU NI WA KUJENGA AMA KUBOMOA? HAFAI KUWA MBUNGE KABISA.
Mtikila ni zaidi ya CHADEMA!
Mtanisamehe kwani kwenye posho,hakuna tofauti ya wapinzani na chama tawala!
ungeanza kabisa na Abdu Jumbe, maana yeye alianza kudai Tanganyika irudi tangu mwanzoni mwa miaka ya 80's.Namkumbuka huyu REV. MTIKILA katika miaka ya tisini alikuwa anadai KATIBA na TANGANYIKA irudishwe, watu wengi walidhania ni chizi kutokana na lugha yake. Leo yale mawazo yake ndiyo yanapiganiwa na wengi. Huyu jamaa huwa ni MTAIFA sana, ila bahati mbaya watu wengi hawamuelewi. nakumbuka alishaipeleka serikali mahakamani akidai mgombea binafsi, alivyoshinda ile kesi PINDA akampotezea. Leo hii tunapigania mgombea BINAFSI.
Walau Mtikila amethubutu kuyasema yote. Hilo ni bunge la kihuni na hakuna kitu pale wala maamuzi yenye afya kwa taifa yatakayofikiwa. Kwa tunaojua tunajua maamuzi yatakuwa ni viini macho tu.
Prof Shivji na wasomi wengi tu wasionunulika walishalibaisnisha hili. Bunge hili halipaswi kutokana na vyama bali wajumbe wake wawe ni WaTanzania tu. Leo bunge lile lina sura ya vyama na wengi wakiwa ni watu kutoka chama tawala.
Ukweli tumeshindwa hata kujifunza kwa wenzetu kutoka nchi jirani ya Kenya kwani walau wao wamethubutu. Pamoja na vurugu zao zilizotokea na kupoteza maisha ya watu lakini walau wametufundisha somo ambalo sisi bado tunasua sua kujitendea haki pasipo kutanguliza hila na ubinafsi.
Hivi umeona wapi mtu mmoja akaamka asubuhi akateuwa watu zaidi ya 600 kwa utashi wake na jinsi alivyojisikia mwenyewe na wakawapa haki watanzania zaidi ya 45 millioni?
Wabunge wa BLK walipaswa kuchaguliwa na wananchi wenyewe bila sura ya vyama na si kuteuliwa kihuni na mtu mhuni mwenye nia kuwatendea watu uhuni.
Kama unamkubali Mtikila mwenye chama chenye usajili wa kudumu ingawa wanachama wote alionao hawafiki 150, basi unamatatizo makubwa.
Kama wajumbe wa hilo bunge ni wahuni na washenzi basi ina maana na yeye mwenyewe ni mhuni na mshenzi.