Mtikila: Hili bunge la katiba limejaa wahuni na washenzi sijawahi kuona toka tupate uhuru

Mtikila: Hili bunge la katiba limejaa wahuni na washenzi sijawahi kuona toka tupate uhuru

Mtikila, huko sasa utakomaa, maana uko katikati yao. Yaani mtu kati, kama hutapata kichaa sijui?
 
Huyu jamaa ni ngangari kinoma ,anatumia uhuru wake vilivyo ,na ndio hivyo tumeanza kuona malimbwende ya Bunge la katiba na bado .
 
Wengi humpuuza Mtikila,bila kuangalia mantiki ya mambo anayoyaibua na kusimamia!
 
Wajumbe ni wahuni ina maana na yeye mwenyewe Mtikila au alisema wahuni kasoro yeye
 
MTIKILA huwa haeleweki, pia ni mtu anae penda sana kesi. Akikoswa kesi ama ya kushitaki au kushitakiwa huwa hana raha kama mlevi kukosa pombe. Kwa hili amekosea, unaposema wajumbe wa baraza la katiba ni wahuni na washenzi, unakuwa umemtukana pia rais alie wateua hawa watu.

We unasoma kwa kigugumizi nini? Tayari amemtukana kwa kusema kuwa na aliyewatua naye ni mhuni! Rudia kusoma tena! Issue ni kwamba tumfanyeje kwa kumtukana MTUKUFU RAIS?
 
Kama unamkubali Mtikila mwenye chama chenye usajili wa kudumu ingawa wanachama wote alionao hawafiki 150, basi unamatatizo makubwa.

Hakuna haja ya kuwa na kundi kubwa la wanafiki wanaojifanya watetezi kumbe wachumia matumbo.... Kheri Jemedari Mtikila
 
Kama unamkubali Mtikila mwenye chama chenye usajili wa kudumu ingawa wanachama wote alionao hawafiki 150, basi unamatatizo makubwa.

Siamini sana kigezo cha wingi wa wanachama, ni mojawapo lakini hakitoshi. kuna vyama vina wanachama wengi lakini wengi wao ni wavivu tu, tangu wameingia hawapata muda wa kujiuuliza kwa nini wapo pale walipo...
 
Walau Mtikila amethubutu kuyasema yote. Hilo ni bunge la kihuni na hakuna kitu pale wala maamuzi yenye afya kwa taifa yatakayofikiwa. Kwa tunaojua tunajua maamuzi yatakuwa ni viini macho tu.

Prof Shivji na wasomi wengi tu wasionunulika walishalibaisnisha hili. Bunge hili halipaswi kutokana na vyama bali wajumbe wake wawe ni WaTanzania tu. Leo bunge lile lina sura ya vyama na wengi wakiwa ni watu kutoka chama tawala.

Ukweli tumeshindwa hata kujifunza kwa wenzetu kutoka nchi jirani ya Kenya kwani walau wao wamethubutu. Pamoja na vurugu zao zilizotokea na kupoteza maisha ya watu lakini walau wametufundisha somo ambalo sisi bado tunasua sua kujitendea haki pasipo kutanguliza hila na ubinafsi.

Hivi umeona wapi mtu mmoja akaamka asubuhi akateuwa watu zaidi ya 600 kwa utashi wake na jinsi alivyojisikia mwenyewe na wakawapa haki watanzania zaidi ya 45 millioni?

Wabunge wa BLK walipaswa kuchaguliwa na wananchi wenyewe bila sura ya vyama na si kuteuliwa kihuni na mtu mhuni mwenye nia kuwatendea watu uhuni.
 
Christopher Mtikila amesema ukweli ambao watanzania tunaogopa kuusikia.Tujivalishe UZALENDO Rais wetu amepotoka kwa kutuchagulia hao wawakilishi ambao kama hata kumchagua kiongozi tu wa muda mfupi wanahongwa na wanakubali kuhongwa,ni aibu ya mwaka.

Na hao waliohongwa na aliyehonga walitakiwa kutolewa mara moja kwenye hilo bunge maana siyo tu wahuni bali wezi wa haki zetu za msingi na hawafai hatakuitwa waheshimiwa.Hakuna tusi la kuwapa watu hawa ila kwenye jamii hata ya panya hawafai kuwepo.
 
Kama unamkubali Mtikila mwenye chama chenye usajili wa kudumu ingawa wanachama wote alionao hawafiki 150, basi unamatatizo makubwa.

Mtikila ni kichwa. Ukimsikiliza kwa makini jamaa huwa ana hoja na misimamo isiyoyumba.

Katika kesi zake zote ambazo amewahi kuishtaki JAMHURI Mahakamani kupinga baadhi ya sheria za kihuni ikiwemo ya mgombea binafsi hajawahi kushindwa. Fuatilia utakubaliana na ukweli huo.

Katika hili la kuhusu KATIBA MPYA na BUNGE LAKE bado Mtikila anaonekana kuwa na hoja ya msingi. Ameshasema kuwa yeye anaenda kufumua Bunge hili na kubatilisha uhuni wote kwa kutaka Tanganyika iundwe kwanza ndipo Katiba ya JMT ishughulikiwe. Kama Bunge hili litakataa hoja yake ameapa kwenda kwenye Mahakama ya kimataifa kudai haki ya Watanganyika.

Chezea Mtikila wewe!!
 
Mchungaji anayo point ya msingi. Kwanza Tanganyika irudi ndipo katiba ya JMT itafutwe.
 
Huyu jamaa akiikosa Tanganyika ndani ya Bunge lazima akimbie kabla ya muda.
 
Kama kawaida yenu vijana wa ccm kwa kurupuka bila hata kutumia akili, yeye kasema anamkubali mtikila na sio chama,, shiiit mbona mnakuwa na vichwa nazi jamani???. Hata kama ni wazito kuelewa ila sasa mnavuka mipaka ya wazito kuelewa..
asante mkuu wabongo ndo tulivyo
 
Genius Mtikila; nakubaliana na mawazo yake kabisa. wajumbe wengi katika bunge hili hawajui hata kama wapo pale kufanya nini. lipo kundi linalosubiri kuonyesha utaalamu wao wa kisheria, lakini lipo kundi vilevile linabeba mitazamo ya vyama na lipo kundi ambalo linataka kutumia nafasi hiyo kutaka kufahamika. sioni kundi lililo beba mawazo ya mwananchi kama wapo ni wachache sana. HAPO NDIPO NINAPOPATA MASHAKA YA KUPATIKANA KATIBA BORA . Wabunge Wahuni kwa ajili ya jambo kubwa la kitaifa. nachoka kabisa.
 
da yani kwa hili mtikila we nishujaa wangu mimi baada ya kugundua hivyo siitaji katiba mpya kwa sababu naamini haitakua na tofauti na hii ya sasa labda rangi ya nje badala ya zambalau inaweza ikawa ya kijani au njano,we katiba iandikwa na chenge,lowasa,wasila,mwigulu,kigwangala,ndugai unategemea nini?
 
Back
Top Bottom