Bwana mkubwa tatizo ni nini? msomali au mtutsi? Mmalawi au mjaluo? Si bora hao watutsi tunaopakana nao kuliko wasomali, Je hujui kuwa mwanajeshi Nyirenda aliyepandisha bendera mlima kilimanjaro alikuwa mmalawi? Angalia ramani ya Tanzania, tunapakana na nchi lukuki na raia wa mipakani hata kabla mzungu hajachora hiyo mipaka walikuwa wana move kutoka sehemu moja hadi ingine. Chokochoko dhidi ya watutsi inatokana na dhana potofu inayohubiriwa na watu wa dini fulani kuwa watutsi wana asili ya kiyahudi, na hiyo dini haina mapenzi mema na wayahudi. Vinginevyo, wazee wa Kilosa walitamka hadharani kuwa Mkulo ni mmalawi lakini mkuu wa kaya aliendelea kumpa uwaziri wa fedha hadi kazi ilipomshinda, Wazalendo kama wewe mlikuwa wapi? Mkuu wa ccm ni msomali tena mwindaji wa tembo, mbona uko kimya?? biashara kubwa na raslimali zote za nchi yako haziko mikononi mwa raia, wewe unakasirikia wafugaji wa kinywaranda? hayo ndo mambo ya msingi ambayo unabidi ujiulize mara mbili mbili kuliko hao maskini watutsi ulio nao sua.
Ki historia wanyarwanda na warundi ni wafugaji na wafuagaji wanahama hama kutafuta malisho, wafugaji si wamefika na kufanya vita rufiji na maeneo mbali mbali ya morogoro?? Je huko nako ni wanyarwanda wamechukua ardhi ya tanganyika?Nakumbuka maisha yangu ya utotoni kwenye 1970's huku kwetu maeneo ya Musoma, hawa jamaa walikuwa wanakuja vijijini kuomba kazi ya kuchunga ng'ombe, walikuwa wanaitwa "abha kanga" kwa kilugha chetu, mshahara wao ulikuwa ni maziwa, akishakamua anajipimia kiasi cha maziwa anachotaka. Watu wa maeneo ya ukanda huu hawa ni ndugu zetu, hata lugha tunazoongea zina maneno mengi yanayofanana, majina ya watu, maeneo na vitongoji vinafanana kwa kiasi fulani, tumekuwa nao pamoja kabla ya kuwajua wazaramo au wandengeleko, Huko nyumba ukanda huu watu wahakuwa wapenzi wa RTD, walikuwa wana tune radio rwanda kigali, kupata miziki ya uhakika, sikinde sijui ngoma ya ukae yalikuwa ya huko daslam