Mtikila: Kuna CHADEMA MBILI - 'CHADEMA Chumbani' na 'CHADEMA Sebuleni'

Mtikila: Kuna CHADEMA MBILI - 'CHADEMA Chumbani' na 'CHADEMA Sebuleni'

Ukweli nimekuwa nafurahishwa sana na "role" ya CDM kama chama cha upinzani Tanzania ingawa kwangu mie CDM na CCM ni kama mashetani wawili, hivyo basi between the two evils choose the lesser one. Kwa kuwa nilishavutiwa sana na CDM kwa hivi karibuni, mapungufu yanayojitokeza ndani yake hivi sasa ukweli yananifanya tumbo linikate kiasi fulani. Katika jitihada za kujaribu kupata mawazo ya jinsi ya kuepusha mgogoro zaidi kwa kutumia njia ya kidiplomasia nimefanya jitihada binafsi za kuongea na viongozi wa juu kama saba hivi wa pande zinazovutana bila wao kujua natafuta nini (sikufanikiwa kuongea na Mbowe tu). Katika maongezi yangu ambayo ilikuwa ni kama wa kitafiti nimegundua yafuatayo:

1. Ukweli ugomvi mkubwa ni kati ya Mbowe na Zitto (hawa wamesababisha makundi yanayosigishana).
2. Kundi la Mbowe lingependelea Zitto awe nje ya CDM na sio ajirekebishe.
3. Kundi la Zitto, likiongozwa na Zitto mwenyewe linajiona lina mchango mkubwa sana kuisababisha CDM iwe ilipo na hivyo basi iwapo Zitto atatimuliwa atakuwa kaonewa sana.
4.Kundi la Mbowe limebambika kashfa kuwa Zitto ni Msaliti ili kumsababishia aonwe mbaya na asiyefaa ilihali likijua kuwa Zitto kamwe hawezi kuisaliti CDM kwa mapenzi aliyonayo kwayo.
5. Kundi la Zitto linaona akina Mbowe pamoja na kuminya demokrasia zaidi ndani ya CDM, wanatumia rasilimali za CDM isivyo, na kupakaza kuwa akina Mbowe wananufaika zaidi katika rasilimali za CDM kwa kuwanyima haki viongozi wa chini.
6. N.K

Hayo ni baadhi tu ya matokeo ya utafiti wangu usio rasmi kwa jambo hili uliotokana na hao vigogo saba wa CDM niliowahoji.

Baada ya kupata matokeo hayo niliamua pia kuhoji namna ambavyo mgawanyiko huo unaweza kutatuliwa na nikapata baadhi ya majibu kama hivi:

1. Kundi la Mbowe linadai hamna namna ya kumaliza mgogoro huo sababu Zitto hawezi tena fanya kazi na viongozi wa sasa (haaminiki) na wanaamini hawezi kushuka chini, na dawa ni kumtimua au mwenyewe ajitoe CDM.
2. Kundi la Zitto linadai Zitto asafishwe kwanza asiitwe Msaliti na apewe nafasi zaidi ndani ya CDM, hapo mgogoro utaisha.
3. Pande mbili zikutanishwe na kila upande ukiri makosa yake then wale viapo vya kutoangushana, kashifiana na kusalitiana ili wasonge mbele (hili ni pendekezo la mmoja tu kati ya 7 niliowahoji).

Kwa mtazamo wangu, nikaelewa mgogoro huu umefikia pabaya na nikawa nimependekeza njia ya kuzifanya pande mbili zikae na kukigawa CDM, yaani iwepo CHADEMA ASILI na CHADEMA MABADILIKO. Wengi wa viongozi saba niliowachomekea hili waliona kitu hiki hakiwezekani kata kata. Upande wa Mbowe ndiyo ulikuwa na msisitizo zaidi kuwa CDM haiwezi gawanywa kwani kumtimua Zitto ni kazi rahisi kwao na hilo ndilo litamaliza mgogoro.

Kwa kumalizia, mtazamo wangu umekuwa tofauti na hoja hizi na ninawashauri (pande zote) kuwa waangalie uwezekano wa kukigawa CDM kuwa vyama viwili, wagawane rasilimali (kwa kuwa kila upande umechangia upatikanaji wa rasilimali zilizopo). Kwa sisi wanachama na mashabiki tutaona wenyewe ni upande upi twende kati ya CHADEMA ASILI (Ya Mbowe) na CHADEMA MABADILIKO (Ya Zitto).

Mwisho: Ikitokea inakuwa hivyo wewe MwanaCDM mwenzangu utaenda CDM ipi?

Pu m-ba_fu
 
Mimi ninataka CHADEMA ambayo niliifikiria ndo chama makini,chama ambacho niliamini ndo chama cha kumkomboa wananchi kule Geita wanaoishi jirani na Migodi ilihali maisha yao ni duni,CHAMA ambacho kingemfanya kila mwananchi afaidike na raslimali ya ardhi aliyozaliwa.
Kwa haya ninayoyaona kwa viongozi wa juu wa chadema kukitumia chama kujinufaisha wao na familia zao,CHADEMA haifai ila muda wa kujirekebisha wanao
 
kweli chadema wajinga,na wala hamfai,mnatumia ujinga wa CCM kujustfy upuuzi wenu?haina haja ya vyama vingi kama mnafanya yale yale yanayofanywa na CCM

wenzako wakivutaga bangi hukimbilia chooni wewe unakimbilia sebureni pumbavuuuuuuuuuu
 
Mangula Kinana Nape KIkwete KUndi Moja CCM Mtandao MPya
Membe Sitta wayembe Mwandosya CCM Mtndao Kati
Wasra LUkuvi Mkuchika Selia KOmbani CCM Mpito
Sophi Simba Nchimbi MwiguluJana Maamba CCM Masalia haya ndi makn yanayosewa sana mitai a CCM kilakundi eti linaanda mtandao wake ungejaribu kutletea malezo ya hawa hao wanajida kuja na chademambadiriko hawataweza kuvuruga chama kamwe
 
kwa kuwa mbowe hana hela lakini hana njaa, na kwa kuwa zitto hana hela na ana njaa, basi automatically zitto anakuwa inferior kwa mbowe.

pipoz pawa!
 
Mimi ninataka CHADEMA ambayo niliifikiria ndo chama makini,chama ambacho niliamini ndo chama cha kumkomboa wananchi kule Geita wanaoishi jirani na Migodi ilihali maisha yao ni duni,CHAMA ambacho kingemfanya kila mwananchi afaidike na raslimali ya ardhi aliyozaliwa.
Kwa haya ninayoyaona kwa viongozi wa juu wa chadema kukitumia chama kujinufaisha wao na familia zao,CHADEMA haifai ila muda wa kujirekebisha wanao

Ageda ya kikao chenu cha leo hakiwezi kufuta headings kwa mfano gazeti la mtanzania linasema Zitto Kabwe azua vurugu chadema hii n I habari itakayotumiwa na watu kibao kuisakama chadema hapa mtandaoni sio Tanzania kwa hiyo munapoteza muda
 
Aliyeandika wala si mtafiti wa asasi ika abachukulia chama km kampuni nami naona upande wa zitto unafikiri cdm iko kibiashara eti mkishindwa kuelewsna mgawane km hisa za kampuni. Mtafiti hutoa suluhu sio kuendekeza kuvunjika kwa kilichopobja kugawana basi mwandishi huyu atakuwa broker. Naamini mwandishi huyu anaakusi mawazo ya akina zitto. Binafsi ni mdau km hivyo nami niende kudai mchango wsngu hii haipo na haitakuwepo. Cdm iko imara na danage iluyodhaniwa haijawa kinachotokea ji kuhamaki huko ndio inasababisha kutapatapa kwa zitto maana damage control imekuwa kubwa so risk ya chama akiondoka imekuwa ndogo tena kosa kubwa ambalo amefanya na kum fãnya sasa asihurumiwe tena ni hicho kwenda mahakamani big mistake and miscalculations. Mhimu km hajalipwa in few weeks tutaona ukweli utakapodhihiri.bkm statementvyake moja sikubmoja ya kuwa we have to trust institution not people hii inamrudia km alidhani inawadhuru wenzake tu sasa inamrudisha kwao. Basically cdm made a mistake to delay but yes time bado ni sahihi ili tusonge
 
Mchungaji Christopher MTIKILA azidi kupiga msumali wa MOTO katika JENEZA la Chadema mashumbulizi yake yamuelekea Edwin MTEI

"Amemtuhumu mmoja wa wanzilishi na m/kiti wa kwanza wa chadema Edwin MTEI, akidai kuwa ni muasisi wa dhana ya UKABILA na UKANDA katika chama hicho huku m/kiti wa sasa Freeman MBOWE na Katibu wake SLAA wakidaiwa kuboresha mfumo huo KISASA zaidi kwa kuweka NAKSH NAKSH"

Hata kinacho wafukuza Zitto na wenzake ktk Chadema ni matokeo ya kuota mizizi kwa mfumo wa UKABILA na UKANDA ambao hauruhusu mwanachama yoyote kuhoji mapato na matumizi ndai ya chama"

WATANZANIA waelewe Chadema si chama cha siasa na VIONGOZI wake si wanasiasa wa kweli, kwani hawana MAONO wala MALENGO ya kuwakomboa watanzania

KWA UJUMLA NI GENGE LA WALAJI TU!!!

Ndani ya chadema kuna kundi linaitwa "BIG EIGHT " ambalo linaudwa na wazee wa KICHAGA na kiongozi wao mkuu ni Edwin MTEI akisaidiwa na akina Mariale na Ndessamburo,

Hawa ndio wenye chadema yao ambapo moja ya MAJUKUMU yao ni kulinda maslahi ya kichaga ndani ya chama,Kuna Chadema mbili kuna chadema ya CHUMBANI na Chadema ya SEBULENI"

Source gazeti la Umma Tanzania 4/12/2013


---------------------------------


Bora hata chombo kimj ingekuwa linasoma gazeti hilo lnasomwa na mtikila na mwenye nalo otherwise habari ya mtikila anaijua yeye wewe na wenye gazeti ha ha bi chadema huna mlo ndio habari ya mujini
 
utafiti feki,zt yeye ameshajipambanua kama back up ya ccm wewe unasema wanampakazia ulitafiti kuhusu pesazilikuwa zinzenda german?pesa alizokuwa akitumia mamluki wake,ukaribu wake na mtu wa tiss mbana utafiti wako kama wa std 7
 
Mchungaji Christopher MTIKILA azidi kupiga msumali wa MOTO katika JENEZA la Chadema mashumbulizi yake yamuelekea Edwin MTEI

"Amemtuhumu mmoja wa wanzilishi na m/kiti wa kwanza wa chadema Edwin MTEI, akidai kuwa ni muasisi wa dhana ya UKABILA na UKANDA katika chama hicho huku m/kiti wa sasa Freeman MBOWE na Katibu wake SLAA wakidaiwa kuboresha mfumo huo KISASA zaidi kwa kuweka NAKSH NAKSH"

Hata kinacho wafukuza Zitto na wenzake ktk Chadema ni matokeo ya kuota mizizi kwa mfumo wa UKABILA na UKANDA ambao hauruhusu mwanachama yoyote kuhoji mapato na matumizi ndai ya chama"

WATANZANIA waelewe Chadema si chama cha siasa na VIONGOZI wake si wanasiasa wa kweli, kwani hawana MAONO wala MALENGO ya kuwakomboa watanzania

KWA UJUMLA NI GENGE LA WALAJI TU!!!

Ndani ya chadema kuna kundi linaitwa "BIG EIGHT " ambalo linaudwa na wazee wa KICHAGA na kiongozi wao mkuu ni Edwin MTEI akisaidiwa na akina Mariale na Ndessamburo,

Hawa ndio wenye chadema yao ambapo moja ya MAJUKUMU yao ni kulinda maslahi ya kichaga ndani ya chama,Kuna Chadema mbili kuna chadema ya CHUMBANI na Chadema ya SEBULENI"

Source gazeti la Umma Tanzania 4/12/2013


---------------------------------

CHADEMA CHUMBANI ni ya wateule wachache wakati CHADEMA SEBULENI ni wafuata mkumbo akina Lissu
 
MAADILI ya uongozi ni mwenendo au tabia njema inayokubalika na jamii katika kazi ya kuongoza. Kwa kuwa uongozi ni kazi ya kuwaelekeza watu kwenye kujiletea maendeleo yao kwa utashi wa uhuru, haki na usawa; viongozi lazima wazingatie maadili ya uongozi yanayokubaliana na utashi wa utu, heshima ya binadamu na usawa katika matumizi ya rasilimali za nchi katika kufikia malengo ya ujenzi wa jamii ya watu waliyo sawa na huru. Hivi ndivyo ilivyodhaniwa kwenye Azimio la Arusha la 1967 na ndio maana uongozi wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius K. Nyerere na chama cha ukombozi (TANU) uliamua kwa pamoja kuweka maadili na miiko ya uongozi kama sehemu ya Azimio la Arusha (1967). Mabadiliko ya sura ya uongozi tangu uhuru (Desemba 9, 1961) hadi wakati huu umeifanya kada ya uongozi wa siasa Tanzania kuwa kazi ya kipato, kama zilivyo kazi nyingine ambazo baadhi ya watu ndani na au nje ya mfumo wa kada ya uongozi wamekuwa wakipigana vikumbo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi za uongozi kwenye mfumo wa vyama na au wa kushika madaraka ya kuongoza nchi kwenye nafasi zake zote. Maadili ya uongozi kama dhamana inayotoka kwa wananchi yamegeuka na kuwa satwa ya ujasiriamali wa kisiasa. Wanasiasa wenye uoni wa kijasiriamali wanaodhani kwamba uwekezaji kwenye siasa ni wenye kulipa wamechukua nafasi kubwa kwenye mchakato wa siasa na uandaaji wa nafasi za uongozi ndani na au nje ya mfumo wa siasa, jamii na uchumi. Kukosekana kwa maadili ya uongozi kwa sehemu kubwa kumesababishwa na hali angavu ya roho iliyochafuka na kushikwa na uchu unaoongozwa na tamaa ya kishetani katika kutafuta “ukubwa” na mamlaka yenye satwa (nguvu) katika kutawala fursa zote zenye taathira katika mchakato wa maisha ya watu na mazingira. Viongozi wa siasa wamepoteza utu na heshima yao kama binadamu anayehitaji utulivu wa nafsi yenye matumaini juu ya kuwatumikia wengine. Kwa ujumla, kama alivyoandika Sayyid Mujtaba Musawi Lari (1992) kwenye kitabu chake kinachoitwa “Uchunguzi wa Matatizo ya Kimaadili na Kinafsi” binadamu anahitaji kuishi kwa kufuata maadili yaliyokamilika. Lari (1992, ukurasa wa 75) anasema, “mojawapo kati ya misingi na shuruti za maisha ya kijamii na ukamilifu wa kila taifa ni maadili.” Ndio kusema, hata Azimio la Arusha (1967) lilisisitiza sana “maadili” na miiko ya uongozi ambayo ndiyo yaliyokuwa sehemu ya maisha ya viongozi wa TANU (na CCM baina ya miaka ya 1967 hadi 1992). Lari (1992) anaonyesha kwamba kama taifa litakosa maadili basi kuna kila dalili ya taifa hilo kuangamia na au kupoteza mwelekeo wa maisha ya saada kimaanawi, kiroho na kimaada. Kwa kuwa binadamu haishi kwa mkate peke yake; bali, kama kiumbe wa kijamii, lazima afuate njia ya uhuru, haki na usawa katika kuelekea kwenye uchaji Mungu ili kwa uchaji huo ipatikane nafasi ya baraka za kiroho katika kufikia malengo makuu na mhsusi ya kuumbwa kwake katika kufanya dunia mahala pa ustawi wa maisha ya sasa katika kuyaendea maisha ya baadaye. Kwa mtazamo wa uchunguzi wa kisayansi na kwa utumizi wa mantiki ya hoja tunaweza kukubaliana kwamba uongozi (na hususan, uongozi wa siasa) umekosa maadili ya uongozi kwa vile sehemu kubwa ya uongozi wetu na viongozi wengi wamekosa maadili ya uongozi na kuongoza. Mara kadhaa wametokea watu kuukosoa uongozi wa nchi yetu. Japokuwa ukosozi huo huonekana kana kwamba ni chuki binafsi zinazoelekezwa kwa watu binafsi kwenye mfumo wa uongozi kutokana na inda (chuki ya mtu dhidi ya mafanikio ya mwingine). Hata kama, kwa sehemu fulani wapo wanaodhani kwamba ukosefu wa uongozi wenye maadili ya uongozi na ukosozi wake huchukua sura ya chuki binafsi; kuna ukweli wa moja kwa moja na wa kisayansi unaoonekana kwa kushindwa kwa uongozi unaoongoza shughuli za serikali kufika utashi wa uongozi bora. Mwalimu Julius K. Nyerere aliwahi kuandika kitabu juu ya uongozi na hatma ya Tanzania wakati wa mgogoro wa uongozi wa awamu ya pili kipindi cha miaka ya 1990 na 1995. Mwalimu Nyerere alijaribu kuonyesha upungufu uliyojitokeza kwenye sehemu ya pili ya awamu ya pili kutokana na kutelekezwa kwa Azimio la Arusha la 1967 na siasa kugeuzwa “ujasiriamali.” Hata hivyo, ukosozi wa Mwalimu Julius K. Nyerere haukuchukuliwa kwa vile “kitabu chake kilikwishapita, na enzi hiyo ilikuwa na kitabu kingine.” Siasa iliendelea kuwa mwendo mdundo kila kiongozi akitafuta kuwekeza kwenye ujasiriamali wa kisiasa (political entrepreneurship) kwa kuwa ilishaonekana wazi kwamba uongozi wa siasa utachukua nafasi muhimu kwenye miaka ya kuanzia 2005 na kuendelea; hali tunayoishuhudia sasa! Mwaka 2008, kama miaka mitatu tangu kuanza kwa awamu ya nne, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba na yeye (kama mwanafalsafa na mwanasiasa) aliandika hotuba juu ya “ukosefu wa uongozi na hatma ya Tanzania.” Kama ilivyokuwa kwa Mwalimu Nyerere ndivyo ilivyokuwa kwa Profesa Lipumba, ukosozi wake ulionekana pumba na kama kawaida uongozi wa chama tawala uliendelea na mwenendo uleule usiyozingatia mabadiliko ya uongozi wenye tija kwa kuzingatia utashi wa watu na maendeleo yao kwa kuzingatia uongozi wenye maadili yaliyotukuka. Hali tete ya ukosefu wa maadili imeendelea kuishika Tanzania. Hata sasa, hali ya ukosefu wa maadili ya uongozi imechukua sura mbaya zaidi kwa vile viongozi wengi wamepoteza maadili ya utu na heshima ya binadamu imemezwa na shetani anayewaongoza kwenye ufisadi mpevu. Kwa muhtasari, tujaribu kufuatana katika kuangalia matatizo ya kimaadili na kinafsi yanayowakabili viongozi wengi wa Tanzania waliyekabidhiwa dhima ya kuongoza shughuli za serikali ya watu kwa niaba ya wananchi. Katika matatizo ya kimaadili kumi na sita (16) kama yalivyoainishwa na Lari (1992) kwenye kitabu chake; sehemu ya matatizo kumi na moja (11) ya matatizo hayo yanapatikana kwa viongozi wa Tanzania! Hili linaweza kukusitua msomaji; hata hivyo, hiyo ndio hali halisi! Kama tutayachukua matatizo ya kimaadili yanayowakabili vongozi wengi ndani na au nje ya mfumo rasmi wa uongozi wa serikali tunaweza kuona kwamba asilimia 68.75 (kama 69%) ya matatizo aliyoyaorodhesha na kuyachambua Lari (1992) yangalipo. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa! Viongozi wengi ni waongo! Pasipokuwa na chembe ya kuogopa dhambi ya uongo, wengi wa viongozi wamekuwa wakichukua viapo vya uongo na kushindwa kutafakari madhara yake. Uongo wa viongozi wengi, kwa mujibu wa uchunguzi na mantiki, unasababishwa na tamaa au tabia chafu ya mazowea ya kudanganya! Wanatumia uongo kwa vile haijawahi kushuhudiwa viongozi wakiwekwa mtu-kati katika kuthibitisha tabia hii ambayo ndio inayowafanya wananchi wengi kuishi kwa kutegemea uongo kama sehemu ya mila na dasturi kwa vile wanawaona viongozi wao wakishiriki na kunufaika na uongo wa kimaslahi. Viongozi wengi wamekuwa wahaini kwa nchi na watu wake kutokana na uongo! Unafiki, kama ugojwa mbaya wa kimaadili, umewashika viongozi wengi wa Tanzania! Kwa ujumla, kama falsafa ya unafiki ilivyo; viongozi wengi ni wepesi wa kutoa ahadi lakini si watekelezaji. Uongozi wa Tanzania umekuwa hodari wa kutoa ahadi nyingi kuliko uwezo wa utekelezaji wa ahadi hizo kutokana na ufinyu na au matumizi mabaya ya rasilimali. Kutokana na ahadi za kinafiki zinazotolewa na viongozi wa siasa wakati wa kampeni za uchaguzi wananchi wamekuwa wakiwapa ridhaa ya kushika nafasi za uongozi kwa dhana kwamba yale yaliyoahidiwa kwenye ilani za uchaguzi yatafanyiwa kazi Kinyume chake, viongozi wengi wamekuwa wakifanya hiana pamoja na kuchukua ahadi ya kutekeleza ahadi na viapo vyao. Viongozi wengi hawasemi ukweli; isipokuwa husema uongo! Uongo umekuwa sehemu ya maisha ya uongozi wa siasa; na ndio maana wapo baadhi ya wanafalsafa wameshaanza kuiona siasa kuwa “mchezo mchafu.” Sifa nyingine mbaya ya kimaadili waliyonayo viongozi wengi wa siku hizi ni udhalimu. Wengi wa viongozi wa serikali katika ngazi zote wana tabia ya kuwakandamiza wanyonge wanaohitaji huduma kama sehemu ya haki ya wananchi kutoka kwa viongozi (na watendaji) waliyepewa dhamana ya kuwatumikia kwa uhuru, haki na usawa. Hali hii, pamoja na mambo mengine, ndio chanzo cha ufisadi wa kimfumo na wa ndani ya mfumo. Chimbuko la rushwa, hongo, chirimiri, kadhongo, na kuzunguka mbuyu ni kutokana na udhalimu wa moja kwa moja katika kukandamiza uhuru, haki na usawa wa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa mujibu wa utashi wa sheria, kanuni na taratibu za kazi ya kusimamia menejimenti ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Kutokana na hali ya kutokuwepo upendo baina ya viongozi na wananchi, roho mbaya na kinyongo miongoni mwa viongozi na wananchi wanayedhulumiwa huamsha chuki na uadui ndani ya jamii. Kwa kutamani hali ya kukomaa kwa chuki na uadui kwa maslahi ya kibinafsi kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa, kijamii na kiuchumi wamekuwa mstari wa mbele katika kuchochea sintofahamu, songombingo au sokomoko za kisiasa, kijamii na kiuchumi ili kwa hali hiyo wapate kujijenga kisiasa na kuchukua nafasi ya kutawala kwa kutumia matukio! Mchezo huu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa siasa ni wa hatari kwa vile wananchi ---------- kama kondoo wa kafara katika kufikia malengo ya kisiasa! Uchunguzi wa mwandishi (kwenye mazingira ya demokrasia ya siasa za vyama vingi) umegundua kwamba sehemu kubwa ya viongozi wana ugonjwa wa kinafsi wa hamaki! Wengi wa viongozi wa siasa hawana uwezo wa kudhibiti hasira zao; na mara nyingi, viongozi waliyeghadhibika huonyesha hasira hadharani na hata wakati mwingine kushindwa kutumia busara na kuishia kutukana matusi (ya nguoni) au kutoa lugha chafu na kashfa! Hapa ndipo walipofika wengi wa vingozi wengi wanaotegemewa kuwa wakomavu na wenye uwezo wa hali ya juu kwa kudhibiti hamaki! Ifahamike hapa kwamba, “mwanzo wa hasira ni wendawazimu na mwisho wake ni majuto.” Wapo baadhi wa viongozi waliyejikuta wakihamaki na kufanya maamuzi yasiyozingatia uhuru, haki na usawa na kujikuta wakijiingiza kwenye migogoro ya kimaadili. Kwa kuwa viongozi wengi wa Tanzania ni watu wanaopenda sana kuchuma na kulimbikiza mali kama mtaji wa ujasiriamali wa kisiasa; wengi wao, kama wanavyoshuhudiwa siku hizi, wamekuwa na tamaa ya hali ya juu katika kuvuna na kuhifadhi utajiri hususan kwa njia haramu na za kifisadi. Hali hii inawafanya wengi wao kuwa na tabia ya ubahili na kushindwa kuwasaidia wananchi wanaowaongoza katika kujinasua kutokana na umasikini wa kipato. Hakuna kiongozi anayefanyakazi ya kuwatafutia wananchi suluhisho la kudumu la matatizo na au changamoto za hali mbaya ya uchumi. Kama wapo, ambao ni wachache, ni wale wanaowapa wapiga kura wa maeneo yao misaada midogo wanapopatwa na majanga ya asili na au kutoa usaidizi wa elimu, mtibabu au maji pale wanapoombwa kufanya hivyo. Tamaa ya kupenda sana na au kutaka sana ndiyo inayowafanya viongozi wengi kufanya vyovyote na kwa “liwalo na liwe” katika kutafuta uwezo wa hali na mali katika kujenga uwezo wa kutawala mchakato na mfumo wa siasa na upatikanaji wa viongozi ndani ya na au nje ya chama na hatimaye serikalini. Kutokana na sababu za kimaumbile; tamaa ya kupita kiasi katika kutafuta uongozi kwa jinsi yoyote iwayo ndiyo inayowavuta wengi wanaotafuta nafasi za kungia kwenye msongo wa uongozi wa chama (kinachotawala) na ndani ya uongozi wa utendaji wa serikali kuwa kama mbwa-mwitu au tai anayesubiri kurarua! Hata kama, wananchi wenye mamlaka ya kuwapa madaraka viongozi nafasi za kuongoza, wakitumia nafsi yao ya kisheria, viongozi wenye tamaa iliyopitiliza hutumia ushawishi wa nguvu ya fedha zilizochumwa kifisadi kupora nguvu ya kisheria waliyonayow ananchi. Mwenendo huu wa kijamii, kisiasa na kiuchumi ndio unaoifanya Tanzania ya leo iwe kama “shamba la bibi.” Kila mwenye nafasi ya kutamani kushika nafasi ya juu kwenye uongozi wa ndani ya chama kinachotawala na au ndani ya mzingo wa utendaji wa kiserikali katika menejimenti ya uchumi na jamii atatafuta nafasi ya kuvuna mali nyingi na kutafuta umaarufu kwa njia yoyote iwayo alimuradi apate nafasi ya kuwa “bwana mkubwa.” Mchakato wa kutafuta “ukubwa” na “uheshimiwa” umewaroga viongozi wengi wa siasa, jamii na uchumi hadi kutaka wasujudiwe na wananchi masikini! Huu ni ushenzi wa kimaadili uliyopitiliza! Si ajabu kuwakuta vijana wachanga (mabwana wadogo) watoto wa viongozi (vigogo) ndani ya chama na au serikalini wakitafuta utajiri (wa hali na mali) katika kulinda na au kutetea nafasi za wazazi wao ndani na au nje ya mfumo wa uongozi! Baba anarithisha ushenzi wa kimaadili kwa kizazi chake; na mama na yeye anafanya vivyo hivyo, kama baba afanyavyo! Kama chama kinageuzwa kampuni la wenye hisa, na wale wenye hisa nyingi ndio wanakuwa wamiliki wa uongozi kwa jinsi wanavyoweza kununua nafasi za uongozi au kuwanunulia watu wanaowataka kuwa viongozi kwa vile wapendavyo wao (wenye ushawishi wa hali na mali). Uongozi umefanywa sehemu ya kinyang’anyiro cha hila na mizungu ya uharibifu wa kimaadili usiyozingatia uhuru, haki na usawa wa kiakili, kiroho na kimaanawi. Binadamu hakuumbwa aishi kama mnyama wa porini; hata wanyama (wa porini) wamewekewa sheria, kanuni na taritibu za kimambile ambazo shuruti (lazima) wazifuate katika kuyaendea maisha yao kama wanyama, sembuse binadamu?! Sura ya viongozi wengi inaonyesha kwamba wengi wamebobea kwenye uwongo, unafiki, takaburi (kiburi na jeuri), udhalimu, chuki na uadui, hamaki, hiana, ubahili, tamaa, na mabishano. Matatizo haya yote ya kimaadili ndio yanayoufanya uongozi wetu ushindwe kufikia malengo ya usimamizi mzuri wa menejimenti ya rasilimali za Tanzania katika kuendesha mapambano dhidi ya maadui wa taifa ambao ni: umasikini; ujinga; maradhi; na ufisadi. Inawezekana kubadilisha hali ya uongozi wetu; wananchi wanapaswa kuchukua nafasi yao. Uongozi wa kiroho ni wajibu kufundisha kwa uhuru, haki na usawa juu ya dhima ya viongozi kwa wananchi. Kwa jinsi hiyo, tamko la kichungaji lililotolewa tarehe 18 Agosti, 2010 mjini Dodoma na viongozi wa dini lilihitaji usimamizi makini na madhubuti. Kwa ujumla, viongozi wengi wa siasa wamekosa sifa zilizoainishwa na viongozi wa dini, yaani: (1) ucha Mungu; (2) kujali na kuwastahi watu; (3) kupenda haki na kuwajli wanyonge; (4) kuijua na kuitetea Katiba ya nchi; (5) ukweli wa maneno na matendo; (6) kushirikiana na wananchi wote bila ya ubaguzi; (7) uwezo wa kuongoza na upeo mpana; (8) kupenda amani na utulivu; (9) uadilifu; na (10) moyo wa uzalendo na kulipenda tiafa lake! Sifa zote hizi; zaidi ya silimia 60 hazipo! Tuna wajibu wa kutafakari tulipokosea; nasisitiza, tulikosea, na ni wajibu tutafute njia ya uhuru, haki na usawa katika kutafuta ufumbuzi wa uadilifu kama taifa. Hatujachelewa sana; japokuwa tumeshaumia kwa miaka 30 sasa; tujiandae kuleta mapinduzi ya fikra. nchi yoyote dunia uendeshwa na katiba na sheria ubaya ni pale viongozi wanaposhindwa kutumia katiba na sheria zilizopo na kubaki kutafuta njia mbadala ya kuiongoza nchi jambo ambalo linakuwa ni hatari kwa usalama na ustawi wa nchi kwani kila kiongozi anabaki akifikiria kila mawazo yake ndiyo njia sahihi jambo ambalo linakuwa ni kinyume na matarajio ya wananchi, siku za hivi karibu kumeanza kujitokeza chuki pandikizi katika nyanja mbali mbali ambayo ni hatari kwa usalama na ustawi wa nchi, nyanja hizo ni 1. siasa 2. udini 3. ajira 4. ardhi 5. usalama ;maeneo haya tayari imisha wagawa watanzania kimtazamo na hatakuwa na hasira kali dhidi ya viongozi na watawala kwa kushindwa kusimamia katiba na sheria ikiwa na miogozo kamili katika kila jambo ili kupunguza uhasama na chuki hizi zinazoenea kwa kasi, kibaya zaidi ni pale bunge ambalo ndilo lingekuwa suluhu kwa kutunga sheria na kuisimamia serekali ili kuakikisha nchi inakuwa na amani kwa kutunga sheria inayotoa haki na usawa katika kila jambo kwa kila mtu imekuwa ni bunge imekuwa ni bunge la matusi na ubabe na kukosa heshima ya kuitwa bunge tukufu. Uchafu na hatari kwa usalama wa nchi kama bunge inaibua mjadala wa udini jambo ambalo limisha sababisha maafa na hata wengine kushitakiwa alafu wanabaki kukebeiana bila kujadili hoja hiyo kwa makini na kulitafutia suhulu la kudumu kwa kuitungia sheria yenye mtanzamo sawa kwa wote yenye kuridhiwa na pande zote husika,hii tu inawathibishia watanzania ushiriki wa bunge katika kuharibu amani hapa nchini kwa maslai ya wachache wenye manufaa na imani hiyo kutoweka kwa kasi pia wabunge kujadili maswala ya nchi kwa misingi ya vyama vyao na bunge kugeuka uwanja wa fujo na ubabe huku wakisaau majukumu yao tena katika kupitisha bajeti ya serekali jambo ambalo na kila mtanzania hili tu. Inatosha kuonyesha watanzania kwamba hatuna sasbabu ya kuwa na bunge la aina hii wamekuwa ni waribifu wa kodi ya wananchi bure bila wananchi kuwa na manufaa na bunge hilo serekali kushindwa kutoa majibu ya wazi katika malamiko yenye jazba kama ugaidi, udini na migoro ya ardhi nao kuingia katika malumbano na kungana na ubabe hii inasabashi wananchi kuamini malamiko hayo yana ukweli ndiyo maana yana kosa majibu ya kuridhisha kwani mpaka sasa wananchi wamishagawanyika katika misingi ya ukanda, siasa, udini, ndiyo maana wananchi wameaza kungomea rasilimali yanyopatikana katika maeneo yao jambo ambalo ni hatari kwa maslai ya taifa, ulevi wa madaraka na siasa zisizozingatia uhuru, utu, haki na usawa litatufikisha katika maisha yasiyo salama kwa amani ya ya nchi yetu kutoweka , kwani ulevi wa madaraka na siasa azina thamani mbele maisha ya binadamu na haki ya kuishi ni wakati sasa kila mtanzania akatafakari kwa umakini tumetoka wapi? Tupo wapi? Na tunakenda wapi? Naisikitikia nchi yangu kuwa na dalili zote za kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe jambo linalosababiswa na majibu mepesi katika maswali magumu yanayoulizwa na wananchi au maswali hayo kukosa majibu kabisa kitakacho tuokoa ni kuwa na sheria zisizobagua watu kwa makundi yao, dini zao , idikadi zao, kabila zao na ukanda wao, na kueshiwa kwa utu wa watu kwa kila moja wao
 
Ili kuondoa dhana hii ambayo imetawala kwa vichwa vya watz wengi kuwa CDM ni chama cha ukabila, wazo langu naomba MBOWE & SLAA wawapishe watu wengine au mmojawapo aachie ngazi na huyo atae shika nafac ya aliyejiengua km SLAA au MBOWE asiwe MCHANGA, kidogo watz wanaweza kuwaelewa nini mnafanya

sema dhana hii imetawala katika vichwa vya ccm sio watz....then katika maisha huwezi kumsatisfy kila mtu..so mbowe na slaa hata baada ya kuondoka bado ccm watakomaa na udini.
 
kuwatimua akina zitto haimanishi ndio mwisho wa mgogoro cha msingi chadema waangalie ni wapi kuna tatizo,coz walianza akina kaburu na chacha kudai hiki hki wanachokidai akina zitto leo, wakaitwa ni wasaliti wakafukuzwa, leo wamekuja akina zitto na madai yaleyale, jamani wanachadema wenzangu pamoja na kuwa chama kimefanya maamuzi na kinaona maamuzi sahihi ni kuwafukuza lakin warudi nyuma waangalie ni wapi kuna tatizo kwa nini watu wanadai madai yaleyale? leo amkuja zitto amedai kesho atakuja MSIGWA au LISSU JE itakuwaje?
 
well said umetumia hekima, akiri na maarifa ya kutosha kuandika makala yako nimeipenda sana,lakin utashangaa wajinga wanaleta siasa za vyama na kwa hilo......nimependa sana ujumbe wako
 
Mchungaji Christopher MTIKILA azidi kupiga msumali wa MOTO katika JENEZA la Chadema mashumbulizi yake yamuelekea Edwin MTEI

"Amemtuhumu mmoja wa wanzilishi na m/kiti wa kwanza wa chadema Edwin MTEI, akidai kuwa ni muasisi wa dhana ya UKABILA na UKANDA katika chama hicho huku m/kiti wa sasa Freeman MBOWE na Katibu wake SLAA wakidaiwa kuboresha mfumo huo KISASA zaidi kwa kuweka NAKSH NAKSH"

Hata kinacho wafukuza Zitto na wenzake ktk Chadema ni matokeo ya kuota mizizi kwa mfumo wa UKABILA na UKANDA ambao hauruhusu mwanachama yoyote kuhoji mapato na matumizi ndai ya chama"

WATANZANIA waelewe Chadema si chama cha siasa na VIONGOZI wake si wanasiasa wa kweli, kwani hawana MAONO wala MALENGO ya kuwakomboa watanzania

KWA UJUMLA NI GENGE LA WALAJI TU!!!

Ndani ya chadema kuna kundi linaitwa "BIG EIGHT " ambalo linaudwa na wazee wa KICHAGA na kiongozi wao mkuu ni Edwin MTEI akisaidiwa na akina Mariale na Ndessamburo,

Hawa ndio wenye chadema yao ambapo moja ya MAJUKUMU yao ni kulinda maslahi ya kichaga ndani ya chama,Kuna Chadema mbili kuna chadema ya CHUMBANI na Chadema ya SEBULENI"

Source gazeti la Umma Tanzania 4/12/2013


---------------------------------


nitasoma badae
 
Back
Top Bottom