Mtindo mpya wa rushwa wa kubomoa na kujenga Hospitali ya Taifa Muhimbili

Mtindo mpya wa rushwa wa kubomoa na kujenga Hospitali ya Taifa Muhimbili

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Kumeingia mtindo mpya wa kujitafutia miradi. Sasa mkurugenzi wa Muhimbili anataka kuanzisha mradi wa upigaji eti Muhimbili ibomolewe na kujegwa upya wakati kuna vijana hawana hata mabweni ya kulala.

Kwani kuna tatizo gani ya maeneo ya kujenga mpaka wakabomoe hospitali! Kwanini basi pasibakie kufanywa chuo cha afya na waongeze wanafunzi kwenye sehemu nyingine muhimu! Wenzetu wana hospital mpaka za makontena eti sisi tunalalamika majengo ni ya kizamani! Wakati tunategemea misaada kwenye dawa na chanjo.

Mtindo huu vilevile upo kwenye viwanja vya mpira na Zanzibar nako wanafanya haya.

A200DAED-8183-47DF-9DA7-C8CCD9EFEBEE.jpeg

Pia soma: RC Chalamila: Hospitali ya Muhimbili itabomolewa yote na kujengwa upya kwa msaada wa Korea Kusini alipokwenda Rais Samia
 
Mkurugenzi wa Muhimbili kushindwa vibaya.

Muhimbili si hospitali ya umma tena, wengi wa wagonjwa kushindwa kutibiwa kwa kushindwa kulipia huduma.

Kwa lugha ingine badala ya pesa kuwekeza ktk kutoa huduma nzuri wanawekeza ktk malengo.

Kwa ufupi serikali imeshindwa ktk kila huduma
 
Muhimbili ilikosewa kwa majengo mengi kuongezewa bila kufuata maelekezo ya wataalamu, hivyo ardhi nyingi imememezwa na huu ujenzi holela na kuharibu mandhari na maeneo ya maegesho.

Maendeleo yeyote yatakayofuata au kufanyika hapo, ni vizuri wawahusishe wataalamu wa usanifu majengo. Au waanze upya sehemu nyingine.

Ni sawa sawa na Uwanja wa Taifa inakuwa na viwanja viwili sehemu moja. Wakati wilaya zingine hakuna kitu au kuna sehemu nyingine kiwanja hicho kingefaa. Ikiwa wataalamu wangetumika. Mfano uwanja wa Uhuru ungebaki hapo, na uwanja wa Mkapa ukawa Kigamboni au sehemu nyingine.

Kule Chuo cha Muhimbili kumekuwa kuchafu sana au ndio majengo yamechakaa, biashara kila sehemu, kuko giza giza ambao ni dalili ya uchafu au kuwa na watu wengi sehemu ni ndogo.

Jingine wangefuata utaalamu ilikuwa ni kutumia ile ile plan ya Sewahaji, Kibasila, na Mwaisela ile lakini wangeenda juu, yaani wangeongeza ghorofa au kuwa na vunja jengo moja na kuweka jipya la ghorofa wanazoona zinafaa kwa mipango ya baadaye, kama 10, 14, n.k.
 
Muhimbili ilikosewa Kwa majengo mengi kuongezewa bila kufuata maelekezo ya wataalamu hivyo Ardhi nyingi imememezwa na huu ujenzi holes na kuharibu mandhari na maeneo ya maegesho .
Maendeleo yeyote yatakayo taka kufanyika hapo ni vizuri wawahusishe wataalamu WA Usanifu majengo , . Au waanze upya sehemu nyingine . Ni Sawa Sawa na uwanja WA Taifa inakuwa na viwanja viwili sehemu moja . Wakati Wilaya zingine hakuna kitu au kuna sehemu nyingine kiwanja hicho kingefaa. Ikiwa wataalamu wangetumika . Mfano uwanja WA Uhuru unge Baki hapo, na WA mkapa ukawa Kigamboni au sehemu nyingine.
Kule Chuo cha Muhimbili kumekuwa kuchafu Sana au ndio majengo yame chaka , biashara kila sehemu , kuko Giza Giza ambao ni dalili ya uchafu au kuwa kama watu ni wengi sehemu ni ndogo.
Jingine wangefuata utaalamu ilikuwa ni kutumia Ile Ile plan ya sewahaji, kibasila na Ile nyingine imenitoka kidogo lakini wange enda juu , yaani wangeongeza ghorofs au kuwa Wana vunja jengo moja na kuweka jipya la ghorofa wanazoona zinafaa Kwa Mipango ya baadae. 10, 14 n.k

Badala ya kubomoa wakajenge sehemu nyingine kisasa🤔 kwanini ubomoe sehemu ambayo inaweza kutumika kwa shughuli nyingine. Kuna shule mbili pale kubwa zaidi ya Tatu kuanzia Tambaza mpaka Azania watoto hawana mabweni ya kutosha kwanini wasikarabati ikawa shule na hospitali ikajegwe sehemu nyingine?
 
Ebu elezea rushwa inafanyika vipi hapo?
Logically jamaa kaeleza mazingira ya rushwa hapo. Kwamba hakuna hoja ya kubomoa jengo na kujenga upya kwa sababu huko kwenye nchi zilizoendelea kuna hospitali ziko hadi kwenye makontena na watu wanapata huduma vizuri kabisa na maisha yanaendelea.

Mtoa mada anaona kwamba kitendo cha kuanzisha mradi wa ujenzi upya wa hospitali kwa kigezo cha majengo yamechoka hakina mashiko kwa sababu majengo sio tatizo, tatizo ni huduma.

Mtoa mada anaenda mbali zaidi anashangaa watu ambao mnategemea misaada hadi ya dawa za asprin, mnaanzisha miradi isiyo na tija.

Kwa mtazamo wangu, mtoa mada ana hoja ingawa sio nzito sana ila asikilizwe.
 
kwa hiyo kama wajengo yamechoka yaachwe tu?

Nyie malalamiko fc mna shida sana vichwani mwenu
 
Badala ya kubomoa wakajenge sehemu nyingine kisasa🤔 kwanini ubomoe sehemu ambayo inaweza kutumika kwa shughuli nyingine. Kuna shule mbili pale kubwa zaidi ya Tatu kuanzia Tambaza mpaka Azania watoto hawana mabweni ya kutosha kwanini wasikarabati ikawa shule na hospitali ikajegwe sehemu nyingine?
Leo umeanzisha mada yenye kueleweka vizuri, pamoja na kuingiza mambo ya ruhwa ambayo huna ushahidi juu yake.

Mimi ningependekeza hizo shule mbili, zihame, eneo lote la upande huo kuanzia Morogoro road liwe eneo la Chuo kukuu, pamoja na Hospitali.

Ikilazimu, watu wafidiwe wahame baadhi ya maeneo kuelekea upande wa Mashariki, kuelekea barabara ya Umoja wa Mataifa.
 
Back
Top Bottom