Mtindo mpya wa rushwa wa kubomoa na kujenga Hospitali ya Taifa Muhimbili

Mtindo mpya wa rushwa wa kubomoa na kujenga Hospitali ya Taifa Muhimbili

Kumeingia mtindo mpya wa kujitafutia miradi. Sasa mkurugenzi wa Muhimbili anataka kuanzisha mradi wa upigaji eti Muhimbili ibomolewe na kujegwa upya wakati kuna vijana hawana hata mabweni ya kulala.

Kwani kuna tatizo gani ya maeneo ya kujenga mpaka wakabomoe hospitali! Kwaninj basi pasibakie kufanywa chuo cha afya na waongeze wanafunzi kwenye sehemu nyingine muhimu! Wenzetu wana hospital mpaka za makontena eti sisi tunalalamika majengo ni ya kizamani! Wakati tunategemea misaada kwenye dawa na chanjo.

Mtindo huu vilevile upo kwenye viwanja vya mpira na Zanzibar nako wanafanya haya.

View attachment 2714027
Toa upumbavu wako hapa
 
NASHAURI WASIBOMOE,NI HERI KUONDOA HAYO MASHULE HAPO JIRANI,NA KUONGEZA MAJENGO MAPYA YA HOSPITALI,PRESENTABLE.
kiasi cha fedha kikaboreshe pugu sec,na kuipanua,ikiwepo kuipa heshima kubwa ya "Mwl.Jkn sec n high school".
Majengo ya Mwanzo yamechoka hata ukiyaacha sio salama Wala sio compatible na Mifumo mipya ya ujenzi wa Kisasa unaoendana na hali ya Sasa.

Usipoyabomoa yatabaki yawe yanafanya kazi gani? Hata NHC inabomoa majengo ya zamani na kujenga mapya.
 
Logically jamaa kaeleza mazingira ya rushwa hapo. Kwamba hakuna hoja ya kubomoa jengo na kujenga upya kwa sababu huko kwenye nchi zilizoendelea kuna hospitali ziko hadi kwenye makontena na watu wanapata huduma vizuri kabisa na maisha yanaendelea.

Mtoa mada anaona kwamba kitendo cha kuanzisha mradi wa ujenzi upya wa hospitali kwa kigezo cha majengo yamechoka hakina mashiko kwa sababu majengo sio tatizo, tatizo ni huduma.

Mtoa mada anaenda mbali zaidi anashangaa watu ambao mnategemea misaada hadi ya dawa za asprin, mnaanzisha miradi isiyo na tija.

Kwa mtazamo wangu, mtoa mada ana hoja ingawa sio nzito sana ila asikilizwe.
Hahahahaha
 
Nasikitika kwamba barsbara nyingi za upanga ni za vumbi na zina mavumbi na mashino hatari hatari...na hapo ni Karibu na CITY centre...
Maghorofa yake yanaficha mengi....hiv kwa nini wasitengeneza barabara qualitu na sidewalks upanga nzima...

Bado kuna nyaya za Tanesco zilizofungwa ovyo ovyo Dar city centre nzima...

Kusema ukweli Dar inasikitisha sana...city council sijui wanafanya nini....hadi kutumia Billion 71 kujenga magufuli stendi...wakati wangejenga stendi simple kama ile wanayojengwa mwemge ya billion 10...na billion 61 zikajenga na kumodify barabara za citu centre kwa kuziwekea sidewalks na mitaro...

NB..barabara nyingi za upanda ni dirt roads 90%...
We jamaa ile stendi ya Magufulu unataka ujenge kwa bilion 10?
 
Kumeingia mtindo mpya wa kujitafutia miradi. Sasa mkurugenzi wa Muhimbili anataka kuanzisha mradi wa upigaji eti Muhimbili ibomolewe na kujegwa upya wakati kuna vijana hawana hata mabweni ya kulala.

Kwani kuna tatizo gani ya maeneo ya kujenga mpaka wakabomoe hospitali! Kwaninj basi pasibakie kufanywa chuo cha afya na waongeze wanafunzi kwenye sehemu nyingine muhimu! Wenzetu wana hospital mpaka za makontena eti sisi tunalalamika majengo ni ya kizamani! Wakati tunategemea misaada kwenye dawa na chanjo.

Mtindo huu vilevile upo kwenye viwanja vya mpira na Zanzibar nako wanafanya haya.

View attachment 2714027
Mkuu acha unaa Nchi hii upigaj muhimu wala huwez fungwa magereza, so acha tule!!
 
Ebu elezea rushwa inafanyika vipi hapo?
Pesa inapigwa kwenye manunuzi, bila mradi huwezi kuiba,tengeneza mradi wa jengo, kila bidhaa itakayotumika, bei ongeza Mara mbili, ukisema unahitaji mifuko 200 ya saruji, unatumia 80 tu, mingine ni chakula!!
Serikalini, peni ya 200,hunuliwa kwa tsh 2000Tsh.
 
kwa hiyo kama wajengo yamechoka yaachwe tu?

Nyie malalamiko fc mna shida sana vichwani mwenu
Majengo yote yamechoka pamoja? Na kwa nini yamechoka? Lini umeyafanyia ukarabati? Na unadhani hayo mapya hayatahitaji ukarabati?

Amandla...
 
Badala ya kubomoa wakajenge sehemu nyingine kisasa🤔 kwanini ubomoe sehemu ambayo inaweza kutumika kwa shughuli nyingine. Kuna shule mbili pale kubwa zaidi ya Tatu kuanzia Tambaza mpaka Azania watoto hawana mabweni ya kutosha kwanini wasikarabati ikawa shule na hospitali ikajegwe sehemu nyingine?
Ndugu yangu unajua muda mwingine nawaza kuwa huenda tuliharakisha sana kupata uhuru. Tungesubiri tupate uhuru mwk 1990 au 2000 nina uhakika kuna mambo mengi ya maana tungekuwa tumeshafanyiwa na wakoloni wetu. Sisi kichwani hakuna kitu NDIO MAANA BARABARA INAJENGWA LEO HALAFU MWAKANI INABOMOLEWA ILI KUONGEZA UPANA NA MADARAJA. Nina uhakika sio muda mrefu Stand ya Magufuli Mbezi itabomolewa, na baadhi ya barabara za mwendo kasi zitabomolewa kwa madai ya kuhamisha au kuboresha.

Ninaamini serikali zetu zingekuwa makini ungekuta DSM sehemu zenye huduma za kibiasha na soko kubwa sio kariakoo tu. PIA INASHANGAZA KUONA SASAHIVI SOKO LA KARIAKOO LIMEONGEZEWA MAJENGO YA GHOROFA za mabilioni ya fedha. Ninaona KULIKO KUONGEZA UKUBWA WA HILO SOKO NI KWANINI WASINGETAFUTA ENEO LINGINE NJE YA MJI NA KUJENGA SOKO LENYE HADHI KAMA VILE BUNJU AU KIBAMBA. YAANI WAO WANAONA SAWA WATU WOTE KUKIMBILIA KARIAKOO halafu wanashangaa kuona foleni za magari

Actually Tanzania we don't have intelligent planners.
 
Hiyo hela wangejenga hospital nyingine mpya
Mloganzila kule wana eneo kubwa sana..kwa nini wasiendeleze kule.

Kwa nini wasitanue huduma mikoani kama mwenzao alivyoanza na hospital za rufaa mtwara, dodoma, mbeya, Mara na geita.
 
Logically jamaa kaeleza mazingira ya rushwa hapo. Kwamba hakuna hoja ya kubomoa jengo na kujenga upya kwa sababu huko kwenye nchi zilizoendelea kuna hospitali ziko hadi kwenye makontena na watu wanapata huduma vizuri kabisa na maisha yanaendelea.

Mtoa mada anaona kwamba kitendo cha kuanzisha mradi wa ujenzi upya wa hospitali kwa kigezo cha majengo yamechoka hakina mashiko kwa sababu majengo sio tatizo, tatizo ni huduma.

Mtoa mada anaenda mbali zaidi anashangaa watu ambao mnategemea misaada hadi ya dawa za asprin, mnaanzisha miradi isiyo na tija.

Kwa mtazamo wangu, mtoa mada ana hoja ingawa sio nzito sana ila asikilizwe.
Umeongea vizuri ila kusema hoja sio nzito umeharibu
 
aliyemweka huyu mkurugenzi ndio anajua, nilimsikia anataka kukopa milioni 600 kujengwa parking. Mloganzila Ina eneo kubwa sana kwanini hizo pesa wasiwekeze kule. Mashine nyingi za vipimo hazifanyi Kazi kwanini wasitumie hizo pesa kukarabati hizo mashine na kukimbilia kubomoa majengo na kujengwa upya.
 
Logically jamaa kaeleza mazingira ya rushwa hapo. Kwamba hakuna hoja ya kubomoa jengo na kujenga upya kwa sababu huko kwenye nchi zilizoendelea kuna hospitali ziko hadi kwenye makontena na watu wanapata huduma vizuri kabisa na maisha yanaendelea.

Mtoa mada anaona kwamba kitendo cha kuanzisha mradi wa ujenzi upya wa hospitali kwa kigezo cha majengo yamechoka hakina mashiko kwa sababu majengo sio tatizo, tatizo ni huduma.

Mtoa mada anaenda mbali zaidi anashangaa watu ambao mnategemea misaada hadi ya dawa za asprin, mnaanzisha miradi isiyo na tija.

Kwa mtazamo wangu, mtoa mada ana hoja ingawa sio nzito sana ila asikilizwe.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] naona unachambua riwaya
 
Back
Top Bottom