Mtoto alichelewa kulia baada ya kuzaliwa na anapitia changamoto kazaa, naomba ushauri wa kitabibu

Mtoto alichelewa kulia baada ya kuzaliwa na anapitia changamoto kazaa, naomba ushauri wa kitabibu

Idrisa1510

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2018
Posts
276
Reaction score
444
Mimi si mtaalam wa masuala ya afya, frstborn wangu amepatwa na changamoto na mimi ni mzazi mpya (baba mpya).

Tarehe 11 mwezi huu wa 9 ndio alizaliwa. Njia ya uzazi ilikua ni ya kawaida japo iliambatana na changamoto nyingi kutokana na mke wangu ndio alikua napata uzazi kwa mara ya kwanza.

Baada ya kuzaliwa, mtoto hakulia (kutoa sauti). Jitihada za watoa huduma ziliendelea ikiwa ni pamoja na kumuweka mtoto kwenye oxygen, na baada ya muda zaidi ya nusu saa hatimae mtoto aliweza kulia.

Baada ya hapo, mtoto hali yake sio nzuri na anapitia mambo yafuatayo:

1. Amewahi kutetemeka mguu na mkono wavkulia na kushtuka-shtuka. Hapa watoa huduma walisema ni degedege na alichomwa sindano iliyomlaza 12 hours (saa 11 jioni mpaka saa 11 alfajiri)

2. Kunyongonyea au kukosa nguvu. Hana uchangamfu kama wa watoto wengine

3. Hanyonyi na akinyonya anavuta mara chache kwa udhaifu kisha anaacha.
Hapa inalazimu maziwa kukamuliwa pembeni na kunyesha kwa kijiko. Kwa njia hii analamba lamba kidogo kwa uchache mno.

4. Muda mwingi amesinzia, hali lii, na akilia basi inakua kwa sauti ya chini sana.

5. Rangi ya ngozi imekua ya bluu na kama kufifia. Sijui ni kutobolewa tobolewa mwili kuingiza masindano au la.

HATUA WALIZOCHUKUA WATOA HUDUMA

1. Mama na mtoto bado wamelazwa kituo cha afya mpaka sasa kwa ajili ya uangalizi wa kitabibu.

2. Wamempima kiwango cha sukari mtoto na wanasema sukari iko chini sana. Kwahiyo siku zote hizi Amekua akiongezewa sukari kupitia mishipa ya damu (mwanzo alichomwa mkono wa kulia lakini baadae wakahamishia mguuni kulia)

NB:
Taarifa zote nazipata nikiwa mbali, maana mzazi na mimi tuko mikoa tofauti.

NAOMBA WATOA HUDUMA ZA AFYA MNIPE JAPO ABC ZA INSHU HII, maana naambiwa mengi ninapouliza kwa jamiii inayonizunguka
 
kwanza pole kwa changamoto, pili jitahidi ukawe karibu nae hata kwa wiki moja ili hayo unayoyadikia ukayashuhudie..

mengine ni ya wataalam wa tiba fanya ukamkutanishe na manguli wa tiba zacwatoto.
 
kwanza pole kwa changamoto, pili jitahidi ukawe karibu nae hata kwa wiki moja ili hayo unayoyadikia ukayashuhudie..

mengine ni ya wataalam wa tiba fanya ukamkutanishe na manguli wa tiba zacwatoto.
Kibaruani huku ni ngumu kuondoka, na pia Hali za kiuchimi kutoka nilipo mpaka kule ni ghali mno.

Nilitamani kuwafanyia mchakato aende hospital yenye madaktari bingwa wa watoto lakini bado hajaruhusiwa kutoka kwa Hali yake
 
jitahidi kama hayupo katika level ya hospital ya mkoa au ya rufaa.. fanya utaratibu upate rufaa hata kwakuforce ila kama uwezo upo.
 
Back
Top Bottom