Mtoto aliyesaidiwa na Rais Samia aanza matibabu ya Kibingwa MOI

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
214
Mtoto Nicholaus Nkinga (9) ambaye changamoto yake ya matibabu ya mguu iliyomgusa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameanza rasmi kupata matibabu ya kibingwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Jijini Dar es Salaam.

Mtoto huyo mwenye changamoto ya kuvunjika mguu wa kushoto alipokuwa akicheza mpira Mwaka Mmoja na Miezi Sita iliyopita katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, amepokelewa leo Januari 05, 2026 katika taasisi ya MOI na kuanza matibabu akiwa ameambatana na mama yake mzazi.

Mama wa mtoto huyo Bi. Lucia Kawawa ameipongeza Taasisi ya MOI kwa mapokezi mazuri huku akimshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa wa upendo na huruma na kugharamia matibabu ya mwanae.

"Ninamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo na huruma... Mtoto wangu sasa ameanza matibabu jambo amabalo sikuwa na uwezo wa kulitelekeza peke yangu" amesema Bi. Lucia

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema taasisi hiyo imempokea mtoto huyo na tayari madaktari bingwa bobezi wameanza taratibu zote za uchunguzi na matibabu kulingana na hali yake.

“Tumempokea mtoto Nicholous na ameanza matibabu, tunamshukuru Mhe: Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuibua mtoto huyu na kumleta hapa MOI, madaktari bingwa wanaendelea na matibabu…najua watu wenye changamoto za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu wapo wengi kwenye jamii yetu” amesema Dkt. Mpoki na kuongeza kuwa

“Wale wenye changamoto hizo wanaweza kuwasiliana nasi kwa namba ya simu 0733803104, ukipiga namba hii itapokelewa na mtoa huduma kwa wateja ambaye utamweleza tatizo lako na kisha taasisi itaangalia namna ya kukusaidida”

Pia Dkt. Mpoki amesema kuwa katika jitihada za taasisi kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi amesema hivi karibuni madaktari bingwa bobezi wataweka kambi maalum ya matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mara.

"Natoa wito kwa wananchi wenye changamoto za mifupa, ubongo mgongo na mishipa ya fahamu kujitokeza kwa ajili ya kupatiwa matibu wakati wa kambi hiyo" amesema Dkt. Mpoki

Naye, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga Bi. Swaiba Chemchem amemshukuru Rais Samia kwa moyo wa upendo na huruma kwa wenye uhitaji na kufanikisha safari ya matibabu ya mtoto huyo.

IMG-20260105-WA0093.jpg
IMG-20260105-WA0069.jpg
IMG-20260105-WA0074.jpg
 
Hivi mnajua kwamba serikali imeifungia JamiiForums, nyie kama taasisi ya serikali kuja kutoa hii taarifa hapa ni uvunjaji wa sheria
Hawa ni wahalifu na wavunjifu wa sheria tu
 
Hivi Samia ni mtaalamu wa mifupa? 🤣
Uchawa bhana
 
Muuaji wa watanganyika anaanza kujikosha Kwa kusaidia mtoto kutibiwa Kwa Kodi za watanganyika.Pamoja na kusaidia lakini ajue tarehe 12/1/2026 MAANDAMANO YAPO PALEPALE YA KUMWONDOA MADARAKANI NDULI MAMA.
 
Nikipiga hiyo namba matibabu yatakuwa bure kwa hisani ama? moi
 
Hata km ndo ivyo mauji aliyofanya huyu bi chura 29oct hayafutiki na atupe ndg zetu tuwazike

wako wap ndg zetui?
 
Mtoto Nicholaus Nkinga (9) ambaye changamoto yake ya matibabu ya mguu iliyomgusa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameanza rasmi kupata matibabu ya kibingwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Jijini Dar es Salaam.

Mtoto huyo mwenye changamoto ya kuvunjika mguu wa kushoto alipokuwa akicheza mpira Mwaka Mmoja na Miezi Sita iliyopita katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, amepokelewa leo Januari 05, 2026 katika taasisi ya MOI na kuanza matibabu akiwa ameambatana na mama yake mzazi.

Mama wa mtoto huyo Bi. Lucia Kawawa ameipongeza Taasisi ya MOI kwa mapokezi mazuri huku akimshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa wa upendo na huruma na kugharamia matibabu ya mwanae.

"Ninamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo na huruma... Mtoto wangu sasa ameanza matibabu jambo amabalo sikuwa na uwezo wa kulitelekeza peke yangu" amesema Bi. Lucia

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema taasisi hiyo imempokea mtoto huyo na tayari madaktari bingwa bobezi wameanza taratibu zote za uchunguzi na matibabu kulingana na hali yake.

“Tumempokea mtoto Nicholous na ameanza matibabu, tunamshukuru Mhe: Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuibua mtoto huyu na kumleta hapa MOI, madaktari bingwa wanaendelea na matibabu…najua watu wenye changamoto za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu wapo wengi kwenye jamii yetu” amesema Dkt. Mpoki na kuongeza kuwa

“Wale wenye changamoto hizo wanaweza kuwasiliana nasi kwa namba ya simu 0733803104, ukipiga namba hii itapokelewa na mtoa huduma kwa wateja ambaye utamweleza tatizo lako na kisha taasisi itaangalia namna ya kukusaidida”

Pia Dkt. Mpoki amesema kuwa katika jitihada za taasisi kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi amesema hivi karibuni madaktari bingwa bobezi wataweka kambi maalum ya matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mara.

"Natoa wito kwa wananchi wenye changamoto za mifupa, ubongo mgongo na mishipa ya fahamu kujitokeza kwa ajili ya kupatiwa matibu wakati wa kambi hiyo" amesema Dkt. Mpoki

Naye, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga Bi. Swaiba Chemchem amemshukuru Rais Samia kwa moyo wa upendo na huruma kwa wenye uhitaji na kufanikisha safari ya matibabu ya mtoto huyo.

View attachment 3525646View attachment 3525647View attachment 3525648
Tanzania inawatto kama Hawa wangapi husemi? Wamrsaidiwa to wangapi husemi? Alimsaidia kama raisi au kama Samia husemi?
 
Back
Top Bottom