Mtoto ana mwaka na miezi 7 na mama yake ana ujauzito ila afya ya mtoto kama inazorota

CAMANGA

Member
Joined
May 14, 2023
Posts
72
Reaction score
299
Wazazi wenzangu naombeni msaada hapo niweze kuvuka kama Kuna sayansi yoyote nisaidieni nitumie

Mtoto anaharisha, nimeenda hospital wamempa oral lakini naona hali yake kiafya inaporomoka, kula amepoteza hamu ya kula hali, muda mwingine unakuwa unashindwa ununue nini Ili ale

Nitumie mbinu gani mtoto arudi hali yake ya mwanzo
 
Pole...hilo janga liliwahi kunikuta...
Njia pekee ya kumnusuru huyo mtoto wa mwaka na miezi 7 ni kumuachisha kunyonya..

Maziwa ya mama yake si salama tena kwa sababu mwili wa mama umeshabadilika mfumo wake kwa sababu ya ujauzito...

Tena hali hiyo kama mtoto ni mdogo sana anaweza kushindwa kutembea...

Muachisheni huyo mtoto nyonyo haraka sana mumpe virutubisho mbadala.
 
Weka wazi mimba ni miezi mingapi
Fanya hivi
Muachishe mtoto kunyonya maziwa ya Mama
Muweke mbali na mama ake na asilale nae
Muanzishie lishe maalumu uji wa ulezi hakikisha unaweka mbegu za maboga maziwa ya ng,ombe wa kienyeji ya kimasai kabisa kama kuna shangazi au mama ake mdogo alale nae mtoto
Kama mimba changa unashauriwa itoe kama huna uwezo wa kuhudumia huyu ambaye keshakuwepi
 
Mkuu jaribu kwenda hospitali tofauti, hio hospital uliyokwenda akapewa oral alipimwa?
Inabidi apimwe kuanzia damu, choo n.k...
Nenda hospital acha njia za mkato, hata ukimpatia dawa za kuongeza hamu ya kula bado hujatibu tatizo...

Endelea kutembelea vituo vya afya tofauti..
 
Pole...hilo janga liliwahi kunikuta...
Njia pekee ya kumnusuru huyo mtoto wa mwaka na miezi 7 ni kumuachisha kunyonya..

Maziwa ya mama yake si salama tena kwa sababu mwili wa mama umeshabadilika mfumo wake kwa sababu ya ujauzito...

Tena hali hiyo kama mtoto ni mdogo sana anaweza kushindwa kutembea...

Muachisheni huyo mtoto nyonyo haraka sana mumpe virutubisho mbadala.
Mkuu kunyonya ashaacha mimba mama Ake amepata baada ya mtoto kuachishwa kunyonya na anatembea vizuri tu, hali yake imebadilika wiki moja hii
 
Weka wazi mimba ni miezi mingapi
Fanya hivi
Muachishe mtoto kunyonya maziwa ya Mama
Muweke mbali na mama ake na asilale nae
Muanzishie lishe maalumu uji wa ulezi hakikisha unaweka mbegu za maboga maziwa ya ng,ombe wa kienyeji ya kimasai kabisa kama kuna shangazi au mama ake mdogo alale nae mtoto
Kama mimba changa unashauriwa itoe kama huna uwezo wa kuhudumia huyu ambaye keshakuwepi
Mimba alipata baada ya kuacha kunyonya mkuu ,mtoto anatembea na alikuwa vizuri tu hali ime change hili wiki ,dogo analia Lia tu na kula hataki
 
Wazazi wenzangu naombeni msaada hapo niweze kuvuka kama Kuna sayansi yoyote nisaidieni nitumie

Mtoto anaharisha, nimeenda hospital wamempa oral lakini naona hali yake kiafya inaporomoka, kula amepoteza hamu ya kula hali, muda mwingine unakuwa unashindwa ununue nini Ili ale

Nitumie mbinu gani mtoto arudi hali yake ya mwanzo
Msilale naye kitanda kimoja.
Zingatieni lishe bora na zaidi ongezeni UPENDO kwake.
 
Pole...hilo janga liliwahi kunikuta...
Njia pekee ya kumnusuru huyo mtoto wa mwaka na miezi 7 ni kumuachisha kunyonya..

Maziwa ya mama yake si salama tena kwa sababu mwili wa mama umeshabadilika mfumo wake kwa sababu ya ujauzito...

Tena hali hiyo kama mtoto ni mdogo sana anaweza kushindwa kutembea...

Muachisheni huyo mtoto nyonyo haraka sana mumpe virutubisho mbadala.
Uongo! Kitu hujui acha kukiongelea’ hakuna uhusiano na mimba na maziwa ya mama. Sema uangalizi wa mama kwa mtoto umepungua. Baba ashike hatamu kumnusulu
 
Wazazi wenzangu naombeni msaada hapo niweze kuvuka kama Kuna sayansi yoyote nisaidieni nitumie

Mtoto anaharisha, nimeenda hospital wamempa oral lakini naona hali yake kiafya inaporomoka, kula amepoteza hamu ya kula hali, muda mwingine unakuwa unashindwa ununue nini Ili ale

Nitumie mbinu gani mtoto arudi hali yake ya mwanzo
Mkuu mtoto anaharisha mnampa dawa hiyo pekee??
Si unaizungumzia ors ya kuchanganya na maji?
Kama ni hiyo kazi yake ni kurudisha madini yaliyopotea mwilini tu.
*Mpeleke apimwe choo,damu,mkojo ili ijulikane tatizo ni nini.
Itapendeza ukienda kumuona pediatrician/daktari wa watoto.
Ukienda kwake utapata majibu sahihi.
Ushauri wa humu usiuzingatie sana.
 
Sisi wa imani potofu tunasema mtoto mnamuunguza kwa miili hapo kitandani mnapolala nae.
Timu imani potofu inaelekeza mtoto aoge maji ya mizizi ya miti shamba inayopigiwa kelele na matangazo ya wizara ya afya.
Mwambie nkeo aongee na wahenga (wanawake wa kabila lake) mechi itaisha dakika ya 3 tu
 
Mnaharaka mno, mwambie akijifungua aweke kitanzi,asifikiri sifa kizaazaa, sikuhizi uzazi ni kifo....atakufa
Hiyo haihusiani madam na uzazi wake kufuatana.
Miaka miwili inatosha mwanamke kupumzika na kubeba mimba nyingine.
Ila kwa anavyolalamika yeye mtoto ndio anayeumwa sana.
 
Pole sana, uyo mtoto anaharisha kwa sababu ya joto la mama yake ilo ni joto ni la mimba kama ungeweza ungetafuta wabibi huwa wanakuwa na tudawa dawa huweza kumaliza tatizo lote ilo. Mimi wife wangu nae yupo na hari kama yako tena mtoto wangu ana mwaka na kama miaka motatu mtoto alianza kiharisha pia alipoteza amu ya kula kabisa lakini nilijiongeza nikatafute tudawa twa mitishamba kwa sasa mtoto anakula uyo mpka anakera ana afya tele.
Ushauri wangu kama utashindwa kupata mitishamba basi mwachishe mtoto kunyonya.
 
Back
Top Bottom