Mtoto ana mwaka na miezi 7 na mama yake ana ujauzito ila afya ya mtoto kama inazorota

Mtoto ana mwaka na miezi 7 na mama yake ana ujauzito ila afya ya mtoto kama inazorota

Dogo Soma
It's usually perfectly safe to continue breastfeeding if you get pregnant and your pregnancy is normal and healthy.

Uione hapa
 
Mkuu kunyonya ashaacha mimba mama Ake amepata baada ya mtoto kuachishwa kunyonya na anatembea vizuri tu, hali yake imebadilika wiki moja hii
Mkuu hiki ndicho kinachomsumbua mwanangu. Miezi mitatu yote anaharisha tuu na Afya inazidi kuzorota. Hospital ya mwisho kwenda yule dr ndo aliyenifumbua akili la sivyo sijui ingekuwaje.
 
Mimba alipata baada ya kuacha kunyonya mkuu ,mtoto anatembea na alikuwa vizuri tu hali ime change hili wiki ,dogo analia Lia tu na kula hataki
Mtafutie dawa za asili ama sivyo kama unaweza mtenge na mama yake akae mbali ikiwezekana mpeleke kwa bibi yake akakae huko mpaka mkeo ajigungue.
 
Sisi wa imani potofu tunasema mtoto mnamuunguza kwa miili hapo kitandani mnapolala nae.
Timu imani potofu inaelekeza mtoto aoge maji ya mizizi ya miti shamba inayopigiwa kelele na matangazo ya wizara ya afya.
Mwambie nkeo aongee na wahenga (wanawake wa kabila lake) mechi itaisha dakika ya 3 tu
Hii nakubaliana na wewe mkuu.
 
Ujauzito wa mama hauna uhusiano wowote na afya ya mtoto. Kiufupi hakuna mambo ya kubemenda kama wengi wanavyosema na mtoto anaweza endelea kunyonya mpaka mama anavyokaribia kujifungua.

Mama azingatie sana usafi wake binafsi na wa mtoto katika kipindi hiki. Mtoto akiwa na umri huu ndio wakati wa kuokota kila kitu kuweka mdomoni, uchafu wote anakula mikono anagusa kila kitu na kuweka mdomoni.

Pia ajitahidi ampe dawa za minyoo kwa wakati, kumpa hamu ya kula ampe sana machungwa au pharmacy kuna dawa za vitamins atumie hizo.

Kila mtoto ana chakula chake anachokipenda natumai mpaka sasa mama kashajua mwanae anapenda nini so ajitahidi kumpikia hicho hata akila vijiko viwili anamwacha baada ya muda kidogo ampe tena.

Ampe sana maji na matunda, kama kuna uwezekano awe anamkatia matunda ambayo mtoto anaweza kula mwenyewe umri huu watoto hupenda kuokota na kula peke yao, amtandikie nguo safi hata akimwaga kiwe safe kuokota kula. Hata chakula pia ajaribu njia hii asimforce kula.

Mwisho afya yake mama aipe kipaumbele. Mungu amtangulie katika safari ya malezi.

NB: Nina unga wa lishe special kwa ajili ya watoto karibu sana huu ataupenda na afya itaimarika.
 
Uongo! Kitu hujui acha kukiongelea’ hakuna uhusiano na mimba na maziwa ya mama. Sema uangalizi wa mama kwa mtoto umepungua. Baba ashike hatamu kumnusulu
Walau wewe una akili uangalizi wa mama kwa mtoto umepungua isitoshe huyo mtoto mbona ni mkubwa kabisa watu wanabeba mimba mtoto akiwa na miezi 3-5 wanamnyonyesha mpaka mimba ikifikisha miezi nane kasoro na mtoto hadhuriki wala nini,,

Wataalam wa jf wengi waongo wengine wamekataa mimba na kuzitelekeza huko ila humu wamo wanajifanya baba ushauri,
 
Back
Top Bottom