Ujauzito wa mama hauna uhusiano wowote na afya ya mtoto. Kiufupi hakuna mambo ya kubemenda kama wengi wanavyosema na mtoto anaweza endelea kunyonya mpaka mama anavyokaribia kujifungua.
Mama azingatie sana usafi wake binafsi na wa mtoto katika kipindi hiki. Mtoto akiwa na umri huu ndio wakati wa kuokota kila kitu kuweka mdomoni, uchafu wote anakula mikono anagusa kila kitu na kuweka mdomoni.
Pia ajitahidi ampe dawa za minyoo kwa wakati, kumpa hamu ya kula ampe sana machungwa au pharmacy kuna dawa za vitamins atumie hizo.
Kila mtoto ana chakula chake anachokipenda natumai mpaka sasa mama kashajua mwanae anapenda nini so ajitahidi kumpikia hicho hata akila vijiko viwili anamwacha baada ya muda kidogo ampe tena.
Ampe sana maji na matunda, kama kuna uwezekano awe anamkatia matunda ambayo mtoto anaweza kula mwenyewe umri huu watoto hupenda kuokota na kula peke yao, amtandikie nguo safi hata akimwaga kiwe safe kuokota kula. Hata chakula pia ajaribu njia hii asimforce kula.
Mwisho afya yake mama aipe kipaumbele. Mungu amtangulie katika safari ya malezi.
NB: Nina unga wa lishe special kwa ajili ya watoto karibu sana huu ataupenda na afya itaimarika.