LA7
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 655
- 2,369
Habari za humu wandugu, natumai wengi wenu hamjambo,
Mimi ni yule yule ndugu yenu niliyekimbia umande kusoma sikuona dili,
Kuna Uzi niliuletaga humu nikijisifia kuwa nimeweza kumlea mwanangu au kumfundiasha kuwa na tabia nzuri akiwa tu na Miaka miwili,
Sasa kuanzia mwezi wa 11. 2023 tulibahatika kutarajia kupata mtoto wa pili hivo kutokana na mambo kubana ili bidi nimsafirishe mke wangu mkoani kwao Kilimanjaro,
Sikumpeleka kwetu kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, tokea mwezi wa 11 2023 nilimfuata baada ya kujifungua mwaka huu mwezi wa tatu ili bidi niwafuate,
Sasa kinachoniumiza kichwa kwa Sasa ni huyu mtoto wangu wa miaka miwili ni wa kiume, tabia yake imekuwa mbaya, mwanzoni hakuwa na hizo tabia,
Ukimpiga labda tu kakofi anakurudishia hasa mama yake
Kipindi cha nyuma hata nikija na zawadi anapokea na kuweka mezani halafu anarudi kwangu, sasa hivi ni anafungua hapo hapo na kama kinafaa kuliwa anaanza kula.
Siku hizi analia bila sababu hata akiomba kitu ukimwambia subiri anaanza kulilia mwanzoni hakuwa hivo,
Amekuwa mchoyo ukimpa kitu halafu ukaamua kukata anaanza kula mwanzoni hakuwa hivo,
Hata mchana nilikuwa nikimwambia alale alikuwa hamalizi dk15 anakuwa amesinzia lakini Sasa anajifunika shuka na kuanzia kukuchungulia,
Nilikuwa nikimpa kitu anasema Asante baba lakini kwa Sasa sioni tena akifanya hivo
Yaani kiujumla amekuwa mbishi, mama yake amekiri kuwa ni kweli mtoto amebadilika,
Hivo mm nimeamua kukaa na kiboko ndani nikimwambia kitu maramoja nikiona anajivutavuta, namtandika ya makalio au miguuni,
Je? Nipo sahihi au ni mbinu gani nitumie ili niweze kumrejesha kama mwanzoni hata kama itachukua muda mrefu, maana hakuna namna.
Nawasilisha.