Mtoto miaka 4 apasua kioo cha basi la Shabiby kwa manati

Huyo mtoto ni JAMBAZIi mtarajiwa.


Kuna msemo usemao MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUWAVYO.
 
Yaani mambo ya viboko watamalizana wenyewe huko nyumbani...

Ila kwa kuwa walitoa 170k hyo inatosha kabisa kujifikilia kuanzia bibi na wote wanaomlea huyo mtoto
Siku moja tulikuwa tunasafiri kuelekea wilaya ya Kwimba, basi njiani kijana mdogo alirusha dongo kubwa kwenye kioo. Bahati nzuri mimi nilikuwa seat ya mbele nilifunga kioo kwa hivyo liligonga kioo. Tuliposimamisha gari yule kijana na wenzake wawili walikimbia. Wenzangu walishuka na kuwafukuza mpaka kwao, na wakakuta akina mama wamekaa wanasukana nywele. Waliuliza nani mwenye mtoto wao wakakataa kujibu, wenzangu wakawaambia tunampeleka polisi kama hamutaki kujibu, na hapo siyo chini ya kilomita 60 kutoka hapo kijijini. Mama yake ilibidi alijibu haraka maana aliogopa ni gari ya serikali.

Yule mama aliambiwa kama anataka mwanawe asipelekwe kituoni basi akate fimbo amchape mpaka bakora zimkolee. Masikini yule mama alikata fimbo na kumchapa kisawasawa yule mtoto wake, lakini nadhani ilkuwa adabu stahiki kwa yule kijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…