Mtoto ni baraka, kwanini wazazi mnawafungia watoto wenye ulemavu ndani?

gearbox

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
563
Reaction score
1,768

Kitu chenye baraka wengi hukiombea wakipate, kinyume chake watu huomba kiwaepuke

Kwa imani zetu huwa tunaamini Mungu anahusika kwenye uumbaji hivyo hata mlemavu ni kazi yake, akipanga uwe na mtoto mlemavu kuna tatizo ?

Naleta hii mada sababu inafikia kipindi wazazi wanafungia watoto wao wenye ulemavu, hawapendi watu wajue, wanahisi mtoto karogwa wanazunguka kwa wachungaji, maustadh, waganga.
 
Unaelewa maana ya ulemavu? Ni kuwa na kiungo ambacho hakiko kawaida au hakifanyi kazi kama inavyotarajiwa.

Swali la kijinga, ni sawa na kusema kwanini watu hawombi maradhi, no one need a misery life, but we accept it when no way out.
 
kwa maelezo yako kupata mtoto mlemavu ni laana ?
 
View attachment 2992733

kitu chenye baraka wengi hukiombea wakipate, kinyume chake watu huomba kiwaepuke

kama watoto ni baraka kwanini watu hawaombei kupata watoto wenye usonji, vipofu, bubu, viziwi, vilema wa viungo, n.k. ?
Kwa nini uombe mlemavu? Kwani yeye anataka kuzaliwa hivyo?
 
Kwa nini uombe mlemavu? Kwani yeye anataka kuzaliwa hivyo?
Kwa imani zetu huwa tunaamini Mungu anahusika kwenye uumbaji hivyo hata mlemavu ni kazi yake, akipanga uwe na mtoto mlemavu kuna tatizo ?
 
Ulemavu wa kuzaliwa husababishwa kwa kiasi kikubwa na makosa ya kibinadamu, wala sio mpango wa Mungu..... ndiyo maana kuna hadi chanjo ili kupunguza kama sio kuzuia uwezekano huo.
 
Tunapata watoto ili tuendeleze jamii(species) yetu ya homo sapiens.

Ni lengo mahususi kabisa la mageuzi(evolution) limepachikwa kwenye ubongo wako na viungo vyako vitashirikiana kutekeleza hilo punde tu utakapopevuka.

Maelezo ya dini ni uongo tu kwangu mimi

Kwa mantiki hiyo kuzaa mtoto mlemavu ni bahati mbaya, lakini kwa vile kila binadamu ana haki ya msingi ya kuishi, na nyanja mbalimbali zimewekwa kusaidia walemavu kuishi, basi utamlea....

Njia rahisi ya kushughulika na mambo yaliyo nje ya uwezo wako ni kuyakubali tu
 
Hata Ustadhi / mchungaji kipelekewa mtoto mwenye ulemavu haoni baraka, anasema kuna pepo inabidi alikemee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…