Tetesi: Mtoto pendwa kapatwa na nini? Yuko hoi kwa Madiba, inadaiwa ni sumu
Kuna kesi moja Mbunge alipakia nyara za Serikali kwenye gari yake. (Meno)
Kwenye gari alikuwa yeye (mbunge)
Dereva wake na aliyemwuzia meno ambaye anaenda naye mjini kumlipa pesa yake.
Mwendesha mashtaka aliulizwa na wakili.

Hivi wewe ukiwa kama dereva wa Bosi wako.
Unaweza kumkatalia kupakia mizigo yake kwenye gari yake ?

Mwendesha mashtaka akaulizwa tena.
Hivi ukiomba lifti kwenye gari ya mbunge wako.
Akikukubalia utaanza kukagua alichokipakia ?
Dereva na muuza (meno) wakawa hawana hatia na kuachiwa huru.

Mbunge Akala miaka Saba gerezani akakata rufaa Akala miaka 12. Katoka kakuta mkewe keshaolewa na mtu mwingine.

Je wewe unaweza kumkatalia Bosi wako anapo kutuma?
Namaanisha Mkuu wa nchi.
 
JF imeingiliwa saivi wamefuta thread yangu kuwashauri TISS kusimamia mabadiliko ya Katiba ili nchi yetu iwe na mifumo imara kwa mustakabali mzuri. Ila wameacha thread inayowaomba hao hao TISS kumuandaa Makonda kuwa Rais. Siku hizi ni censorship humu. Wanaamua kipi cha kwenda hewani na kipi cha kutokwenda. Hili sio lile jukwaa la Maxense Mello tuliyemjua zamani!

@maxence mmelo JamiiForums mmekuwaje?
 
"Mtoto mpendwa"?

Nani anampenda huyo mtoto. Baadhi yenu watu wa JF huwa mnajisahaulisha sana. Lakini yote haya inajulikana sababu yake ni nini...; kujikomba; uchawa, n.k..
Baadhi ya watu humu hata wakiona nyoka wao watamwita ni mnyoo, ili mradi tu waonekane wanapigania chama cha mapinduzi
Huyo wewe unaye mpachika "utoto mpendwa", ni misingi ipi inayokufanya wewe uone ni "mtoto mpendwa"?

Mtu kutumiwa kama kikaratasi cha chooni, ndiko kupendwa huko?
Huyo hapendwi, ila inamlazimu mteuzi kumleta karibu kwake kwa sababu inalazimu afanye hivyo, siyo kwa sababu ya mapenzi yake.

Mara nyingi unafiki unaoonyeshwa katika maandishi humu ndani ya JF, kwa sababu tu za uchama zinawaondolea heshima wenye tabia hizo.

Long-useless comment
 
Back
Top Bottom