Pre GE2025 Mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli amwaga Pikipiki kwa UVCCM Mkoa mzima wa Geita

Pre GE2025 Mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli amwaga Pikipiki kwa UVCCM Mkoa mzima wa Geita

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndugu zangu Watanzania,

Mtoto Wa Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Joseph Magufuli Rais Wa awamu ya Tano Ndugu Jesca John Magufuli Amemwaga Pikipiki kwa makatibu wote wa UVCCM Mkoa wa Geita.

Binti huyu mdogo ametoa msaada huo wa pikipiki kwa makatibu hao wa UVCCM ili ziweze kuwasaidia watendaji hao wa vijana ngazi ya wilaya katika shughuli zao.hii ni kwa kutambua kuwa jumuiya hiyo ndiyo injini na moyo wa chama na tanuri la kuwapika viongozi mbalimbali wazalendo, wachapakazi, waadilifu na wenye moyo wa kujitoa na kujitolea kwa chama na serikali.

Ndio maana binti huyu Mbichi ameamua kuwa sehemu ya kuijenga na kuipa nguvu UVCCM.ikumbukwe UVCCM itajengwa na wenye moyo na siyo wenye tamaa na uroho wa madaraka na vyeoView attachment 3136209View attachment 3136210View attachment 3136211

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
fisadi kama babake hafai
 
Sema huyu katoa pikipiki kali..sio yale SSH..😂
 
Kwa mtu mwenye akili timamu, anaejitambua, na mwenye familia hawezi kushangilia huu ujinga. Huyo anarudisha pesa za walipa kodi zilizokwapuliwa na mwenda zake enzi za uhai wake. Km unabisha, eleza chanzo cha fedha alizonunilia hizo pikipiki. Tusifurahie pale manyang'au yanaporejesha pesa za wanyonge kwa mkono wa nyuma.

Tatizo wapumbavu ni wengi sana Tz kuliko wajinga. Yani mtu unafrahia kupewa zawadi yenye thamani ya mamilion ya pesa wakati mtu huyo hana kazi ya kumpatia pesa hiyo. Ukiwa mwanaume unatakiwa ufikiri kabla ya kuongea, vinginevyo utakuwa hauna utofauti na mchepuko.
Kama umeumia basi kunywa hata sumu UFE tu maana huna faida yoyote ile hapa Duniani
 
Hizi hela wanazitoa wapi? Au ndio pikipiki anazogawa Mama? Hakika hii Nchi itatafunwa hadi wenyewe watakapozinduka usingizini.
 
Back
Top Bottom