Mtoto wa kike wa miaka 9 kulala na babake

Vipi hajawahi kukutembelea akiwa bila baba'ke na akalala kwako? Kama amewahi alilala na nani? Na vipi baba'ke akisafiri mtoto huwa analala na nani kama hawezi kulala bila baba'ke? Naimani suluhisho mnalo nyie wenyewe
Kwao ana chumba chake. Na pia nimempa chumba cha wageni akiwa kwangu na pia nimempa uhuru wa kulala chumbani kwa mwenzie. Anaweza kushinda huko wakifanya yao, tatizo ni usiku wakati wa kulala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama umeielewa mada vizuri... kuna mtu kazungumzia mawasiliano na ex wake hapa?
Mama amezaa mtoto na jamaa wakahitilafiana. Baba akachukua mtoto kulea to 9 yrs, mama huko aliko ameolewa ana mji wake ameamua kuganga yajayo na mume mpya sasa unapataje guts za kumuita huyo mama muuaji boss?

Ina maana alitakiwa aendeleze connections na huyu jamaa kisa mtoto! Huoni angehatarisha uhusiano mpya.
 
ha ha ha kama vile umenisema mimi kabinti kangu kana miaka mi nne mda wa kulala utasikia ''baba njoo tulalele wote'' na mimi nnavo kadekeza siku nyingine hua naenda nalala chumbani kwake... ila miaka tisa mkubwa mnoo pia si jambo jema japo watoto wa kike wanapenda saana baba zao...
 
Umeenda shule kwa maswala ya mwanao huko huko ukapata mme!!

Kwa maana moja au nyingine kila uhudhuriapo shughuli fulani unaibuka na kifaa kipya!!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuacha mtoto wa miezi sita... anayehitaji zaidi maziwa ya mama kuliko kitu kingine chochote huu ni sawa na ukatili unaofanywa na watu wasiojulikana. Ni ushetani uliopitiliza.
 

Mimi naona kama tunapima lifestyle ya mleta mada kama vile tunamfahamu sana, Inaweza kutokea yeye na huyo baba wa motto wnanaishi kwenye nyumba yenye chumba kimoja na sebule, kwa sababu hajatuambia, sasa mnavyoshauri wamtengee chumba chake huyo mtoto halafu sijui wamuwekee na TV na midori, watoto wengine hawana hivyo vitu na wanalala peke yao.
 
Nisawa mkuu ila mtoto kama unaona maelekezo yamekuwa magumu kuyafuata viboko viwili vitatu huwa vinasaidia
 
Cha kufanya kwa haraka haraka kwa kua una kwako na kama haitaathiri masomo yake basi mchukue ukaishi nae kwako kwa muda wa hata mwezi awe analala mbali na baba yake na akiwa kwako kama una vyumba vya kutosha basi anzisha competition ya utani utani ya watoto kulala peke yao
Waweza kurudi jioni ukawauliza "nani anaweza kulala peke yake?" Wakikujibu basi unawaambia nataka nione atayeweza kulala peke yake kutandika kitanda na kufanya usafi wa chumba chake kisha atayeweza kwa siku 5 tu nitampa zawadi ,vitu kama outing n.k vitumike kuwa inspire
Kwa kupitia hayo atajifunza taratibu ili apate hizo zawadi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo linaanzia kwa huyo baba. Alitakiwa yeye awe ameshamzoesha kulala chumba kingine tangu yupo mdogo kwani anafahamu kuwa ndio inafaa. Na yeye miaka 9 yote hajaoa wala haishi na mke ni kwamba alikuwa anamtumia huyo mtoto kama substitute ya patner hapo chumbani hata kama sio kimapenzi. Ina maana usingetokea wewe angeendelea tu mpaka miaka mingine mingi tu.

Kwahiyo yeye mwenyewe inabidi ampe darasa mtoto taratibu kuhusu kwa nini inabidi aanze kujitegemea kufanya mambo yake. Ukifanya wewe atakuchukia na katika umri huo hatoacha kukuchukia.

Odhawaizi sepa kama walivyosepa wengine kabla yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…