Mtoto wa kike wa miaka 9 kulala na babake

Mtoto wa kike wa miaka 9 kulala na babake

Vipi hajawahi kukutembelea akiwa bila baba'ke na akalala kwako? Kama amewahi alilala na nani? Na vipi baba'ke akisafiri mtoto huwa analala na nani kama hawezi kulala bila baba'ke? Naimani suluhisho mnalo nyie wenyewe
Kwao ana chumba chake. Na pia nimempa chumba cha wageni akiwa kwangu na pia nimempa uhuru wa kulala chumbani kwa mwenzie. Anaweza kushinda huko wakifanya yao, tatizo ni usiku wakati wa kulala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama umeielewa mada vizuri... kuna mtu kazungumzia mawasiliano na ex wake hapa?
Mama amezaa mtoto na jamaa wakahitilafiana. Baba akachukua mtoto kulea to 9 yrs, mama huko aliko ameolewa ana mji wake ameamua kuganga yajayo na mume mpya sasa unapataje guts za kumuita huyo mama muuaji boss?

Ina maana alitakiwa aendeleze connections na huyu jamaa kisa mtoto! Huoni angehatarisha uhusiano mpya.
 
Mimi ni single mother wa mtoto wa kike wa miaka 10. Nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi na single father mwenye binti wa miaka 9.

Watoto wetu wanasoma shule moja madarasa tofauti. Tulikutana kwenye mkutano wa wazazi shuleni. Hali ya kuwa single parent ilituunganisha, tukajikuta tupo mapenzini. Tumekuwa msaada kwa kila mmoja wetu kwenye malezi.

Hatuishi pamoja officially ila tunatembeleana na sleepovers za mara kwa mara.

Tatizo ni huyu mtoto wangu kupitia mpenzi wangu, anapenda kulala na babake. Babake anasema ndio yuko hivyo kwani ameanza kumlea toka ana miezi 6 na hivyo kubidi kulala nae toka umri huo. Ameshindwa kum'wean'.

Akilala peke yake au na mwanangu hapati usingizi, inabidi aje chumbani kwetu tulale nae, either hadi asubuhi au tumhamishe kwa kumbeba akiwa ameshalala.

Naomba ushauri nifanye nini kumsaidia huyu mtoto aweze kujitegemea.

Natanguliza shukran wapendwa.
ha ha ha kama vile umenisema mimi kabinti kangu kana miaka mi nne mda wa kulala utasikia ''baba njoo tulalele wote'' na mimi nnavo kadekeza siku nyingine hua naenda nalala chumbani kwake... ila miaka tisa mkubwa mnoo pia si jambo jema japo watoto wa kike wanapenda saana baba zao...
 
Mimi ni single mother wa mtoto wa kike wa miaka 10. Nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi na single father mwenye binti wa miaka 9.

Watoto wetu wanasoma shule moja madarasa tofauti. Tulikutana kwenye mkutano wa wazazi shuleni. Hali ya kuwa single parent ilituunganisha, tukajikuta tupo mapenzini. Tumekuwa msaada kwa kila mmoja wetu kwenye malezi.

Hatuishi pamoja officially ila tunatembeleana na sleepovers za mara kwa mara.

Tatizo ni huyu mtoto wangu kupitia mpenzi wangu, anapenda kulala na babake. Babake anasema ndio yuko hivyo kwani ameanza kumlea toka ana miezi 6 na hivyo kubidi kulala nae toka umri huo. Ameshindwa kum'wean'.

Akilala peke yake au na mwanangu hapati usingizi, inabidi aje chumbani kwetu tulale nae, either hadi asubuhi au tumhamishe kwa kumbeba akiwa ameshalala.

Naomba ushauri nifanye nini kumsaidia huyu mtoto aweze kujitegemea.

Natanguliza shukran wapendwa.
Umeenda shule kwa maswala ya mwanao huko huko ukapata mme!!

Kwa maana moja au nyingine kila uhudhuriapo shughuli fulani unaibuka na kifaa kipya!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama amezaa mtoto na jamaa wakahitilafiana. Baba akachukua mtoto kulea to 9 yrs, mama huko aliko ameolewa ana mji wake ameamua kuganga yajayo na mume mpya sasa unapataje guts za kumuita huyo mama muuaji boss?

Ina maana alitakiwa aendeleze connections na huyu jamaa kisa mtoto! Huoni angehatarisha uhusiano mpya.
Kuacha mtoto wa miezi sita... anayehitaji zaidi maziwa ya mama kuliko kitu kingine chochote huu ni sawa na ukatili unaofanywa na watu wasiojulikana. Ni ushetani uliopitiliza.
 
Mleta mada kuweni waangalifu namna mtakavyo tatua shida hiyo.

Mikikosea ama kwa kutumia nguvu au kuharakisha mambo basi utajikuta wewe unageuka kama adui wa mapenzi ya mtoto kwa baba yake.

Mtoto atakuchukia na hata mkiowana na huyo jamaa hautafurahia ndoa yenu sababu ya huyo mtoto.

Kwanza mgeuze kuwa rafiki yako huyo mtoto. Pili anza utaratibu wa kwenda kumsimulia hadithi au kumsaidia homework au kuangalia wote Movie au Catoon chumbani kwa mtoto hadi anapata usingizi analala. Wakati huo unamsisitiza watoto wakiwa wakubwa wanatakiwa wawe na chumba chao.

Unamuonesha mfano ktk movie mnazo angalia watoto wengi wana vyumba vyao na hawapendi kero. Muwekeeni vitu na mapambo mbalimbali chumbani.

Mimi naona kama tunapima lifestyle ya mleta mada kama vile tunamfahamu sana, Inaweza kutokea yeye na huyo baba wa motto wnanaishi kwenye nyumba yenye chumba kimoja na sebule, kwa sababu hajatuambia, sasa mnavyoshauri wamtengee chumba chake huyo mtoto halafu sijui wamuwekee na TV na midori, watoto wengine hawana hivyo vitu na wanalala peke yao.
 
Mkuu unakuta wewe ni kati ya wanaolalamikia ukatili wa baba J, huku upande mwingine unashabikia malezi ya bakora na ukatili kama utumwani Babylon dhidi ya watoto wetu.

Huwezi jua historia ya bond ya huyo mtoto na baba yake. Huenda waliachwa ktk kipindi kigumu sana na mama wa mtoto au changamoto zingine zozote.

Jambo la msingi taratibu afundishwe sasa amekuwa mkubwa hatakiwi hata kuingia ovyo chumbani kwa wazazi.
Nisawa mkuu ila mtoto kama unaona maelekezo yamekuwa magumu kuyafuata viboko viwili vitatu huwa vinasaidia
 
Cha kufanya kwa haraka haraka kwa kua una kwako na kama haitaathiri masomo yake basi mchukue ukaishi nae kwako kwa muda wa hata mwezi awe analala mbali na baba yake na akiwa kwako kama una vyumba vya kutosha basi anzisha competition ya utani utani ya watoto kulala peke yao
Waweza kurudi jioni ukawauliza "nani anaweza kulala peke yake?" Wakikujibu basi unawaambia nataka nione atayeweza kulala peke yake kutandika kitanda na kufanya usafi wa chumba chake kisha atayeweza kwa siku 5 tu nitampa zawadi ,vitu kama outing n.k vitumike kuwa inspire
Kwa kupitia hayo atajifunza taratibu ili apate hizo zawadi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo linaanzia kwa huyo baba. Alitakiwa yeye awe ameshamzoesha kulala chumba kingine tangu yupo mdogo kwani anafahamu kuwa ndio inafaa. Na yeye miaka 9 yote hajaoa wala haishi na mke ni kwamba alikuwa anamtumia huyo mtoto kama substitute ya patner hapo chumbani hata kama sio kimapenzi. Ina maana usingetokea wewe angeendelea tu mpaka miaka mingine mingi tu.

Kwahiyo yeye mwenyewe inabidi ampe darasa mtoto taratibu kuhusu kwa nini inabidi aanze kujitegemea kufanya mambo yake. Ukifanya wewe atakuchukia na katika umri huo hatoacha kukuchukia.

Odhawaizi sepa kama walivyosepa wengine kabla yako.
 
Back
Top Bottom