Mtoto wa kiume anakojoa damu umri maiaka10

Mtoto wa kiume anakojoa damu umri maiaka10

Ndio ikoje
Mpeleke hospital kaka achana na kuchat

Mimi siku niko machungani nikanywa maji ya kisima baada ya kubanwa na kiu kikali sana kumbe kile kisiwa kilikuwa ni kichafu pasipo mimi kujua na maji yake huwa si ya kunywa, baada ya kama masaa kadhaa ikanitokea hiyo hali jion nikarudi home nikamtonya mshua hiyo changamoto

Hakukawia wala hakuchati na mtu Bali dakika hiyo hiyo akanipeleka hospital usiku majibu yakaja ni kichocho

Ni dozi kwa kwenda mbele
 
Kwanini huwa mnakimbilia humu kwa mambo serious kama hayo?

Ninavyoamini mimi ni kuwa kwenye mitandao huwa tunakuja kuomba ushauri baada ya tiba au diagnosis za awali kushindikana.

Yani kutafuta tiba mbadala au kama kuna mtu aliwahi kupata changamoto ya hivyo na ikawa solved.

Ilitakiwa uwahi hospitali ikishindikana ndio unakuja humu kutafuta suluhisho.
Sijakuja kutafuta suluhu nimekuja kushare tu,nalengo mim asubuh niamkie hospital ya mkoa kabisa,maana hapa wilayani kiuweli usiku huu huduma mtu anayopewa sana nikitanda na dripu hakuna kipimo unaweza fanyiwa usiku huu nahata hiyo mda wakazi yaan saa,ndio maana nawaza kwenda mkoani
 
Pole sana mkuu

Yah muhimu kucheki na Kichocho (urinary Schistosomiasis). hasa kama maeneo mnayokaa ni karibu na Ziwa au mito au mashamba ya mipunga au madimbwi ya maji wanakocheza watoto na kama kuna historia au kipo kichocho maeneo hayo.
Kama hamna ...check pia travelling history ya miez ya karibuni kama alisafiri kwenda maeneo hayo.

Mwenyezi Mungu amponye dogo akae fresh.

Ikiwa positive.
Praziquantel drug of choice.
Nikweli acha nifike wacheck,Sasa ngazi ipi ya hospital nibora Zaid kwa matibabu kama hayo yakichocho
 
Huo muda wa kushinda hapa kwenye hii mada, ilitakiwa uwe ushafika hosp, au ww n mzazi uliyezaliwa miaka ya 2000.?
 
Sijakuja kutafuta suluhu nimekuja kushare tu,nalengo mim asubuh niamkie hospital ya mkoa kabisa,maana hapa wilayani kiuweli usiku huu huduma mtu anayopewa sana nikitanda na dripu hakuna kipimo unaweza fanyiwa usiku huu nahata hiyo mda wakazi yaan saa,ndio maana nawaza kwenda mkoani
Usiwapuuze wa Wilayani maana Inaweza ikaja siku Ukawahitaji.
 
Mnawaza kichocho tu'

Hamuwazi inflammation zozote za kwenye kidney au bladder... Ni kichocho tu' siyo?

Peleka mtoto hospital
Ndo akili yangu inawaza huko inaweza kuwa Zaid ya hiyo kichocho ndio maana nataka kwenda hospital ya mkoa
 
Sijakuja kutafuta suluhu nimekuja kushare tu,nalengo mim asubuh niamkie hospital ya mkoa kabisa,maana hapa wilayani kiuweli usiku huu huduma mtu anayopewa sana nikitanda na dripu hakuna kipimo unaweza fanyiwa usiku huu nahata hiyo mda wakazi yaan saa,ndio maana nawaza kwenda mkoani
Sawa mkuu wahi hospitalini mapema kijana afanyiwe uchunguzi apewe matibabu
 
Nikweli acha nifike wacheck,Sasa ngazi ipi ya hospital nibora Zaid kwa matibabu kama hayo yakichocho
Kiongozi
Hicho kipimo kituo cha afya/hospitali ya wilaya uhakika unapata kupimwa huo mkojo.
Kama ni KICHOCHO , MTAALAMU AKIWA MAKINI/ MTAALAMU MAKINI kuangalia "sediments za chini" baada ya kuuacha mkojo utulie kama dakika 20 tu mayai hushuka chini then akichek anaona mayai ya Mdudu wa kichocho. So hapo ni microscope tu inahitajika basi.

Nje ya hapo wahi kwa wataalamu ngazi ya juu ,mkoani nk dogo apate huduma sahihi.
 
Ngazi ipi ya hospital wanaweza baini hii tatizo na kutibu namaanisha kituo Cha afya,hospital ya wilaya au hospital ya mkoa ya rufaa
Ngazi zote hizo wanauwezo wa kubaini tatizo. Pale watakaposhindwa watakuelekeza ngazi ya juu. (Referal). e.g. Kama ni kichocho (Blood flukes) wanaonekana kwa darubini ya kawaida; na darubini hizo zipo kila zahanati kijijini.
 
Ndo akili yangu inawaza huko inaweza kuwa Zaid ya hiyo kichocho ndio maana nataka kwenda hospital ya mkoa
Mostly kwenye matibabu, siyo aina ya hospital Bali ni aina Daktari unayekutana naye... Pia usisahau kuwa friendly kwa anayekuhudumia ili upate wasaa wa kumuuliza au kuuliza maswali meengi kuhusu changamoto ya mwanao

All the best
 
Kiongozi
Hicho kipimo kituo cha afya/hospitali ya wilaya uhakika unapata kupimwa huo mkojo.
Kama ni KICHOCHO , MTAALAMU AKIWA MAKINI/ MTAALAMU MAKINI kuangalia "sediments za chini" baada ya kuuacha mkojo utulie kama dakika 20 tu mayai hushuka chini then akichek anaona mayai ya Mdudu wa kichocho. So hapo ni microscope tu inahitajika basi.

Nje ya hapo wahi kwa wataalamu ngazi ya juu ,mkoani nk dogo apate huduma sahihi.
ALAA kumbe ni hivo
 
Mostly kwenye matibabu, siyo aina ya hospital Bali ni aina Daktari unayekutana naye... Pia usisahau kuwa friendly kwa anayekuhudumia ili upate wasaa wa kumuuliza au kuuliza maswali meengi kuhusu changamoto ya mwanao

All the best
Namim huwa nakuwa friendly nkakuuliza vitu vingi mara nyingi nimejikuta madaktari wengi wananipa muda wakunisiliza nakunipa elimu kwa udani Zaid,maana navokua naulizaga wananiona ni mtu nae jali sana afya Hadi wananambia upo tofaut nawagonjwa wengi wanaokutana nao
 
Mkuu amka kesho asubuhi mapema sana hosptal maana angekuwa ni 18+ tungeliumga tela la zile sindano za wiki Hadi tako linakufa ganzi kisa kuokota mademu wa sinza
 
Mostly kwenye matibabu, siyo aina ya hospital Bali ni aina Daktari unayekutana naye... Pia usisahau kuwa friendly kwa anayekuhudumia ili upate wasaa wa kumuuliza au kuuliza maswali meengi kuhusu changamoto ya mwanao

All the best
Exactly yes. Watoto wanaweza ku-overdue katika michezo yao au mwenzake akampiga e.g. teke eneo la kinena au akaanguka vibayana kusababisha mchubuko kwenye kibofu cha mkojo. Lakini cha msingi Ampeleke dogo Hosp.
 
La mwisho unapoenda kwa Daktari epuka kuwa limbukeni wa kutaja magonjwa (Diagnosis) kisa tu' una uelewa au uli gugo huko....

Taja dalili na jibu unavyoulizwa..

Wabongo mnazingua ndio maana unaweza kuona hospital Fulani haina maana kumbe ukienda tu, unapoulizwa kinachokusibu usharopoka Naumwa YUTIAI au MALERIA

😂😂😂

Sasa umemtajia Daktari diagnosis (ugonjwa) unataka akupe dawa tofauti na unazozitaka...? Eti nyie Genz wazee wa AZUMA?
 
Back
Top Bottom