Mtoto wa Magufuli (Jesca) sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Mtoto wa Magufuli (Jesca) sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Inawezekana kweli alipita njia halali nimejaribu kuangalia majina ya wanafunzi wa hiyo school of humanity mwaka 2014 hilo jina halipo kwa hiyo ni kweli amechelewa mwaka mmoja kwa hiyo naombeni hizo shaka mzitoe
Chuo Kikuu Dodoma, waliodahiliwa shahada ya kwanza 2014/15
Yupo mwaka wa pili sasa... Lecturers wake wengi nafahamiana nao na ni rafiki zangu...

Au mnataka tuweke mpaka namba yake ya chuo??? Mnataka tuanze na kuweka course work zake humu muone ukilaza bado haujaisha..
 
Kuna huyu jamaa anaitwa rutashobolwa nataka nijue aliishia darasa gani maake najua ata certificate ya mapishi hana
Haya twambieni kama ni kweli kuwa hayo matokeo ya form four ndio yalitumika kama mtoa mada anavyo jaribu kuonesha!
2012/13 - Certificate...

2013/14-2014/15 - Diploma..

2015/16 - University of Dodoma..

Huu mwaka mtoto wake angetakiwa ndio awe mwaka wa kwanza... Ajabu ni kwamba yuko wa pili..

Wanadahiri diploma kwenda chuo kama una diploma unaomba NACTE Mhaya mshamba wewe.
 
Ni vichwa maji tuu hata kuangalia hiyo screen short vizuri hawajaangalia wamekimbilia kukomenti!

Yani watu wazima wanadanganywa kama watoto...kweli Magufuli kawachoma!
Mkuu unajivua nguo hadharani, tulia tu..Wanaomaliza diploma wote wanadahiliwa na NACTE na TCU ni kwa freshers tu. Kumbe humu wengine hata form four hamjafika halafu mnatamba!!!!
 
Diploma ni miaka miwili Chifu....
Miaka miwili ukiwa unacredit tatu yaani zikiwa zinakuruhusu kwenda advance ndo unaenda kusoma diploma lakini kwan matokeo ya jeska hana credit tatu so anatakiwa aanzie certificate na sio diploma hope utakua umeelewa
 
Haya twambieni kama ni kweli kuwa hayo matokeo ya form four ndio yalitumika kama mtoa mada anavyo jaribu kuonesha!
teh teh teh teh naona unahamisha magoli tu...

Haki bin haki ni angetakiwa kuwa mwaka wa kwanza...

Jamaa atuambie mtoto wake kasomaje somaje Certificate na Diploma ndani ya miaka miwili..

Atujibu hilo tu mkuu..
 
Wanadahiri diploma kwenda chuo kama una diploma unaomba NACTE Mhaya mshamba wewe.
Wao hawadahili mkuu...Bali wanakuunganisha na CAS ambayo inaendeshwa na TCU...

Ukigonga hapa chini penye NOAS|NACTE Online Admission System


Itakupeleka hapa...TCU
 

Attachments

  • IMG-20160603-WA0000.jpg
    IMG-20160603-WA0000.jpg
    69.8 KB · Views: 53
  • IMG-20160603-WA0001.jpg
    IMG-20160603-WA0001.jpg
    73.1 KB · Views: 51
Yupo mwaka wa pili sasa... Lecturers wake wengi nafahamiana nao na ni rafiki zangu...

Au mnataka tuweke mpaka namba yake ya chuo??? Mnataka tuanze na kuweka course work zake humu muone ukilaza bado haujaisha..
Kwani Magufuli kasema mtoto ni genius? Acheni unafiki. Ebu wekeni na yenu tuone
 
Bora mseme na nyinyi sasa. Like father like daughter. Huyu kilaza kama baba yake
kusomea ukarani hizo kozi za ukarani ili upate bahati ya mtende kupata credit za kuweza kukubaliwa UDSM imeanzishwa lini? Masomo haya ya ukarani ni ya muda gani? Muhula unaanza lini mpaka lini? Mpaka sasa hivi ni Wanafunzi wangapi waliopitia hii course ya ukarani na kufanikiwa kupata credits za kuwawezesha kuingia UDSM? Vilaza wengine ambao hawakufanya vizuri O'level wapi watume maombi yao ya course hii ya ukarani!?

Ok well... Sio NECTA ni NACTE.. NECTA na NACTE ni vitu viwili tofauti kabisa... Suala la pili, ni kweli kadahiliwa na NACTE maana Diploma wote wao wanapitishia maombi yao NACTE na sio TCU... Kinachounganisha TCU na NACTE ni mfumo unaoitwa CAS ambao ndio wote hutumia.. Yaani kama kwenda Arusha mmoja anapanda ndege anashuka KIA na mwingine anapanda basi ila wote mnatumia vyombo vya usafiri..

Pili, huyo binti alifeli.. hakuresit ila alienda kusoma Utumishi wa Umma... Huko alisomea ukarani.. Mimi nilichoshangaa pekee ni kutoka kwenye Ukarani mpaka kwenda kusoma Human Resource wakati hesabu alipata F na Commerce alipata F kwenye mitihani yake ya Form Four.. Kama huyo mtoto angekuwa amesoma Diploma ya HR wala nisingeshangaa..
 
Wao hawadahili mkuu...Bali wanakuunganisha na CAS ambayo inaendeshwa na TCU...

Ukigonga hapa chini penye NOAS|NACTE Online Admission System


Itakupeleka hapa...TCU
Sawa mkuu vyovyote iwavyo ni sawa... Iwekeni nyie mnavyotaka ni sawaa..

Ila Je, kasomaje Certificate na Diploma ndani ya miaka miwili pekee mpaka apate sifa ya kudahiliwa chuo kikuu??

Hapa ndipo kwenye base ya swali, sio TCU wala NACTE wala kufeli kwake Form Four.. Swali ni Cheti na Diploma inawezekana kusomewa kwa miaka miwili Tanzania hii??
 
Haya twambieni kama ni kweli kuwa hayo matokeo ya form four ndio yalitumika kama mtoa mada anavyo jaribu kuonesha!
Sasa unafkili yatakua yametumika yapi yaan ata kuchaguliwa chuo kikuu aliombea NACTE dats why kwenye matokeo yake kuchaguliwa kwake UDOM jina lake lipo kwenye copyright ya nacte mwaka 2014 [emoji767]NACTE 2014 sasa ndugu yangu kwa kumaliza form four 2011 bila credit alitakiwa akasome diploma kwan miaka mitatu yaani including na certificate probably angeanza mwaka wa kwanza 2015 lakini matokeo yanaonyesha kaanza mwaka 2014 something must be wrong ni hayo tuu mkuu
 
Hajasema ni genius, amesema ni 'kilaza' kwa tafsiri yake mwenyewe. Swali ni je, amefikaje chuo kikuu huku Kakiwa 'kilaza'?
Ndo maana anatumbua hajari mtu Muda ukifika lazima iwe tu
 
Bora mseme na nyinyi sasa. Like father like daughter. Huyu kilaza kama baba yake
kusomea ukarani hizo kozi za ukarani ili upate bahati ya mtende kupata credit za kuweza kukubaliwa UDSM imeanzishwa lini? Masomo haya ya ukarani ni ya muda gani? Muhula unaanza lini mpaka lini? Mpaka sasa hivi ni Wanafunzi wangapi waliopitia hii course ya ukarani na kufanikiwa kupata credits za kuwawezesha kuingia UDSM? Vilaza wengine ambao hawakufanya vizuri O'level wapi watume maombi yao ya course hii ya ukarani!?
teh teh teh teh Maswali yako magumu sana.. Haya ni mkulu mwenyewe ndio ataweza kuyajibu kwa ufasaha..

Sasahivi watoto wetu wakipata Division mbaya hivo (kumbuka tu Division 4 ya 30 hata Ualimu hawakuchukui) basi tunawapeleka kwenye ukarani kuwasubiria wenzao waliopata Division 1 na 2 wakiwa Form Five na Six alafu wanaenda kukutana tena Chuoni mwaka mmoja... Hakuna haja ya kuhangaisha watoto na PCM, PCB, EGM, HGE, ECA wakati Ukarani pele Utumishi wa Umma wa kuzugia upo..
 
What goes around comes around! Tujifunze kuwa na akiba ya maneno tuwapo mbele ya majukwaa ya siasa
 
Kwani ni ya uongo? Si ipo kwenye public domain?
ipo kwenye public domain sawa....mimi natilia mkazo ule ufukunyuzi wake.

sio kila kilichopo kwenye public domain ni cha kukileta JF na kukijengea habari.

vingine ni vya kupotezea tu ili visikuingize matatizoni.tukumbuke hii ni ya zama ya mtawala asiyependa kukosolewa.
 
Back
Top Bottom