Mimi kwenye kupambana na mafisadi wala simwamini na wala sio muumini wa vita vya kukomoana...
Ajenge uchumi tuuone unajengeka... 7 months zimepita zaidi ya lile dili la bomba la mafuta ambalo nalo ni kwa msaada wa Al Shabab ndio tumelipata sijaona kingine kilichofanyika.. Mtaani pesa imekuwa ngumu, watu wameshaanza kuchomana moto kwa uwizi kitu ambacho tulishakisahau kwa miaka mingi tu..
Fiscal and Monetary Policies awamu hii hawazijui kabisa, ndio maana wanatoa pesa kwenye mabenki ya biashara na kwenda kujifungia nazo ndani alafu wanaamua na kubaka kabisa government expenditure ili sijui pesa izaane yenyewe huko Ikulu... Leo hii pita benki zote kitengo cha Mikopo uone wafanyabiashara wanavyoshindwa kurejesha marejesho yao.. Juzi nimesoma gazeti la Mwananchi lina Public Notice kutoka kwa benki kama nne tofauti zikitangaza kufulisi watu.. Hali ni mbaya mkuu... Tusubiri labda bajeti ikipita wataiachia hiyo pesa inayozaana yenyewe huko Hazina..