Mtoto wa Mbowe, Dudley Mbowe aanguka akiwa Yatch Club, alazwa ICU

Mtoto wa Mbowe, Dudley Mbowe aanguka akiwa Yatch Club, alazwa ICU

Dudley Mbowe, mtoto wa kiume wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman A. Mbowe amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospital ya Aga Khan, Dar es Salaam baada ya kuumia vibaya kichwani.

Kijana huyo jana alifanyiwa operesheni ya kichwa na inaelezwa hali yake ni mbaya.

Sababu za kulazwa kwa Dudley inaelezwa kuwa ni baada ya kuanguka na kukigonga kichwa chake vibaya wakati akiwa Yatch Club, iliyoko Leopard’s Cove, Msasani Bay jijini Dar es Salaam.

Club hiyo ni sehemu ya starehe ambayo inaruhusu wanachama tu kuingia na kustarehe. Gharama ya kuwa mwanachama ni dola 500 (zaidi ya Sh milioni 1) inayolipwa kila mwaka. Kiasi hiki hakihusishi gharama za vinywaji, vyakula, boti za kifahari na huduma nyingine za kiwango cha kimataifa.

Hili linakuja ikiwa ni siku chache tangu Freeman Mbowe adaiwe kuumizwa na kuvunjwa mguu akiwa jijini Dodoma ambapo baadaye alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar.

Chanzo: Mtoto wa Mbowe aanguka, alazwa ICU
Habari imekaa kidemu demu tu
 
Hapo imekuuma hii habari kuletwa humu!
Hahaha wewe ni muandishi wa habari za Afya?! Mbona habari za wagonjwa wengine huleti humu?!

Halafu habari za membership ya Yatch Club, gharama za kujiunga na gharama za kula na kunywa, zina uhusiano gani na ajali au matibabu ya ajali aliyopata?!

Hahaha this is crazy people.
 
Jini mkata kamba anaimendea familia ya Mwenyekiti.
 
Ruzuku za chama zinapukutishwa kila siku ,huku wanachama wakipato cha chini hatuoni matumizi sahihi ya pesa za chama .zaidi ni baba na mwana kuangamizwa kwa ulevi.

Pole kwa mgonjwa,Mungu akusaidie upone na urejee tena kwenye kupukutisha ruzuku ya chama

JamiiForums-726394381.jpg
JamiiForums1858942893.jpg


Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Nisiposema pole pengine nikaonekana nna wivu wa dola 500,.lol lakini kuna majanga mengine ni ya kujitakia tuu...ulevi???🙄🙄
Kwa nini unafanya conclusion kuwa ni ulevi wakati ambapo hakuna sehemu wamesema alikuwa mlevi? Hata kuanguka hapo inawezekana alikwenda kwa shughuli nyingine kabisa na siyo kustarehe.
 
Back
Top Bottom