Mtoto wa miaka mitatu awekwa unyumba na Baba yake mzazi

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
Kuna msemo unaosema ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya Firauni, tukio la Baba mzazi mkazi wa mtaa wa Mafisa, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kudaiwa kumuweka unyumba mtoto wake wa kike wa miaka mitatu limewachukiza wengi huku baadhi ya wananchi wakiiomba serikali kuchukua hatua kali zaidi kwa mtuhumiwa huyo ili iwe fundisho kwa wengine

Mtoto huyo wa miaka mitatu ambaye jina lake limehifadhiwa, inaelezwa ameanza kupitia maswaibu angali bado akiwa kinda (mdogo sana) ambapo majirani wanasema taratibu walianza kumuona Baba wa mtoto huyo akioga na mwanaye mara kwa mara na hatimaye kuanza kumfanyia ukatili, huku wakisema licha ya Mama kupenyezewa taarifa hizo lakini hakujali.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mafisa, Salum Hamadi amesema tayari wameshamfikisha Baba huyo mikononi mwa Jeshi la Polisi, ambapo Jeshi hilo mkoani Morogoro limekiri kumshikilia Baba wa mtoto huyo kwa uchunguzi zaidi.

Source - JamboTv
 
Ukiachana na laana, bado nawaza hivi hawa watu huwaga wanazo akili au na ushirikina sometimes 🤔🤔... Maana huku kwetu leo zinatembea za chinichini mwenyekiti wa jumuiya kambaka kichaa,, halafu ni mbaba mstaafu anaheshimika karibu na kila mtu na mke wake ni mrembo hatari
 
ushirikina(ndumba) offcoz,maanake haiingii akilini mtu timamu kufanya tendo la hivyo Kama hilo..
Ujinga wa kutafuta Mali kwa masharti ya mganga ndio huo,watanzania baadhi madish yameyumba,kupenda short cut tu !
 
ushirikina(ndumba) offcoz,maanake haiingii akilini mtu timamu kufanya tendo la hivyo Kama hilo..
Ujinga wa kutafuta Mali kwa masharti ya mganga ndio huo,watanzania baadhi madish yameyumba,kupenda short cut tu !
Inafikirisha sanaa na haileti majibu, em imagine mtoto kama huyo inapitaje 🤔
 
Mbona hangingii akilini sasa miaka mitatu apenyezewe dudu yani nawaza akili inagoma
 
Hamna unyumba hapo zaidi ya imani za kishirikina.

Sababu kiuhalisia mtoto wa miaka mitatu hana anachojua zaidi ya kufuata tu kile anachoambiwa au kulazimishwa afanye.
 
ushirikina(ndumba) offcoz,maanake haiingii akilini mtu timamu kufanya tendo la hivyo Kama hilo..
Ujinga wa kutafuta Mali kwa masharti ya mganga ndio huo,watanzania baadhi madish yameyumba,kupenda short cut tu !
Na kinachoshangaza saa ingine huyo aliyemshauri kwamba atapata hizo mali ni kapuku wa kutupwa.
 
Waganga wanatambuliwa na serikali. Waganga ndio wanaaoshauri watu kubaka ili kufanikiwa kibiashara. Waganga wanakingiwa kifua na wafanya biashara.
Angekuwa mchungaji ama shehe anaagiza mtu abake ingekuwa issue nyingine ila kwa mganga haguswi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mambo ya kishirikina.
 
Ajabu sana
 

Attachments

  • 20240217_062116.jpg
    202 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…