Mtoto wa miezi 2 analia mpaka napata wasiwasi na maziwa hataki kunyonya na nipo mbali na hospitali tatizo linaweza kuwa ni kwa wenye udhoefu wa watoto

Msaada wa haraka mtoto wa miezi 2 analia mpaka napata wasiwasi tatizo linaweza kuwa nini mbaya zaidi maziwa hataki kunyonya
Tatizo kama hili lilimpata mwanangu wa miezi2 mwezi uliopita dogo hataki kunyonya analia mfululizo, hospital wakampa panadol, nikaanza kumpa maziwa ya LACTOGEN-1 saivi fresh tu.
 
Kwa taaluma ya "Nyungu" inaitwaje?
 
Mresho naona ni tumbo maana nimempa maji ya uvuguvugu yalichangwanya na chumvi na sukari kama memba alishauri kanyamaza na usingizi juu
Yawezekana tumbo ila yawezekana pia njaa.

Epuka kumpa mtoto chumvi au sukari maana ini lake na kongosho haliwezi kumudu ipasavyo. Unaweza kuuliza wataalam ila watoto wadogo si vema wapewe added salt au sugar.

Jitahidi mama awe na maziwa ya kutosha na anyonye hadi ashibe na acheulishwe kwa kuweka begani. Gesi nyingine hujikusanya wakati umemlaza chali hivyo mama awe anamlaza kwa tumbo ( ila awe anamwangalia asilalie pua akaji suffocate) .

Pia chakula anachokula mama kinaweza kumletea mtoto constipation na gesi.

Vyote hivi usisite kuwaleza madaktari ukienda clinic.
 
Acha upotoshaji. Maziwa ya mama yanajitosheleza kwa miezi sita ya mwanzo Yana Maji na virutubisho vyote vinavyotakiwa kwenye ukuaji wa mtoto.
Umekariri kweli kweli wewe, hebu linganisha hicho ulichokariri na tatizo aliloliainisha mtoa mada.... utaelewa tu!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…