Mtoto wa miezi 6.5 takriban masaa mawili analia bila kunyamanza shida inaweza kuwa nini?

Mtoto wa miezi 6.5 takriban masaa mawili analia bila kunyamanza shida inaweza kuwa nini?

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,266
Reaction score
3,698
Habai wakuu mtoto gafla mda huu takriban masaa mawili na zaid analia bila kunyamanza..mama yake alikua katoka nyumbani kwenda kusalimia sehemu baada yakurudi jioni mtoto kaanza kuia bila kunyamanza.

Hii inaweza kuwa shida gani?
 
Mpe Panadol ya maji Yaezekana ni Meno yanaanza toka hivyo fizi zinaanza kuuma..
Ila wakati umempa panadol ya ki mtoto mpeleke hospital aangaliwe na dokta wa watoto.

Watoto hawaezi sema wapi panapouma au kuumia hivyo njia yake ya kutafuta msaada ni kulia.

Ila vitu ambavyo watoto hupelekea kulia ni

Njaa

Joto(Hapa kwenye joto ki ukwel familia nyingi zimefeli yaani tuna utamaduni wa kumjaza mtoto manguo mengi na kuishi vyumba ambavyo haviingizi hewa ya kutosha)

Maumivi kama ya Tumbo kujaa gesi, meno kuota

Kuumwa.
 
Mkuu Huku hospital yakutibu usiku hakuna zaid ya dripu tu na NES wazamu

Ukiwa na mtoto ndani hakikisha unayo panadol ya maji na ile dawa ya kutoa gesi. Na hakikisha unayo akiba ya kutosha ya pale aumwapo itakayokusaidia katibabu yake na usafiri.

Ukishaona hospitali iliyoko karibu haiwezi saidia mtoto basi funga safari kwenda hospitali zenye huduma ya kumkidhi mtoto.
 
Mpe Panadol ya maji Yaezekana ni Meno yanaanza toka hivyo vizi zinaanza kuuma..
Ila wakati umempa panadol ya ki mtoto mpeleke hospital aangaliwa na dokta wa watoto.

Watoto hawaezi sema wapi panapouma au kuumia hivyo njia yake ya kuotafuta msaada ni kulia.

Ila vitu ambavyo watoto hupelekea kulia ni

Njaa

Joto(Hapa kwenye joto ki ukwel familia nyingi zimefeli yaaani tunautamaduni kumjaza mtoto manguo mengi na kuishi vyumba ambavyo haviingizi hewa ya kutosha)

Maumivi kama ya Tumbo kujaa gesi, meno kuota

Kuumwa.
Ni ukweli
 
Habai wakuu mtoto gafla mda huu takriban masaa mawili na zaid analia bila kunyamanza..mama yake alikua katoka nyumbani kwenda kusalimia sehemu baada yakurudi jioni mtoto kaanza kuia bila kunyamanza.

Hii inaweza kuwa shida gani?
Pole sana!
Mpeleke hospital akaonwe na daktari, usipoteze muda kusubiri ushauri mtandaoni wakati mtoto yupo hoi analia kwa saa 2.
 
Habai wakuu mtoto gafla mda huu takriban masaa mawili na zaid analia bila kunyamanza..mama yake alikua katoka nyumbani kwenda kusalimia sehemu baada yakurudi jioni mtoto kaanza kuia bila kunyamanza.

Hii inaweza kuwa shida gani?
Dege dege hiyo nahisi mkuu
 
pole mkuu..japo sijaelewa maelezo ya mama yake kutoka kwenda kusalimia kisha kurud mtoto analia ghafla..je yanahusiana nin?? au ulikuwa na ulazima gani kuyaweka?? ingetosha kusema mtoto ameanza kulia ghafla .au unafkiri ni nin shida?? maana mie hapa naweza kusema LABDA mama yake alienda kuchepuka na amerud na janaba hivyo mizimu ya mtoto inagoma kukaa na mama hadi aoge hilo janaba....kama unanielewa bas ushanielewa.....naweka mic chini bwana mc🥹🥹😀😀
 
Habai wakuu mtoto gafla mda huu takriban masaa mawili na zaid analia bila kunyamanza..mama yake alikua katoka nyumbani kwenda kusalimia sehemu baada yakurudi jioni mtoto kaanza kuia bila kunyamanza.

Hii inaweza kuwa shida gani?
Wahi hospital, hata kama ni nurse ndio yupo,,,,,mtoto kulia hata kubembeleza hataki (inconsolable) ina maana kuna kitu serious inayohitaji uchunguzi na sio hisia tu na kuanza kutoa Panadol. Kila dawa hutolewa kwa sababu maalumu, sasa huku mtandaoni utashauriwa sijui mpe dawa fulani lakini jiulize hiyo dawa unampa mtoto kutibu nini?

Muwahishe mtoto kituo cha afya kilichoko karibu, hata kama ni nurse ndio yupo anajua dalili za dharura (emergency and urgency signs and symptoms )
na pia anajua namna ya kumchunguza mgonjwa,,,kwa hiyo usiache kumpeleka hospital eti kwa sababu kituo kilichopo watatoa sijui dripu tu,,,,
Kila lakheri
 
pole mkuu..japo sijaelewa maelezo ya mama yake kutoka kwenda kusalimia kisha kurud mtoto analia ghafla..je yanahusiana nin?? au ulikuwa na ulazima gani kuyaweka?? ingetosha kusema mtoto ameanza kulia ghafla .au unafkiri ni nin shida?? maana mie hapa naweza kusema LABDA mama yake alienda kuchepuka na amerud na janaba hivyo mizimu ya mtoto inagoma kukaa na mama hadi aoge hilo janaba....kama unanielewa bas ushanielewa.....naweka mic chini bwana mc🥹🥹😀😀
Haaaa kumbe hii inawezekana
 
Mpeleke hospitali hapa tutakisia tu, labda meno yanaanza kuota, tumbo limejaa gesi au tatizo lolote la kiafya....mimi niliambiwa nilivyokuwa mdogo nikisumbua kwa kulia nilikuwa nanyweshwa konyagi kidogo nasinzia ila sishauri hiyo tiba, nafikiri ndio maana akili zangu hazijakaa sawa
 
Back
Top Bottom