I second this. Mara nyingi shida tunazopata ni matokeo ya kilichofanyika mwanzo. Iwe ni sisi wenyewe ama waliotutangulia. Katika kitabu cha Imani yangu kuna andiko linasema "Misingi ikiharibika mwenye haki atafanya nini?"
Sasa its either; Mtoto kapigwa zongo ama juju na mama hajui kumswalia mtoto (not sure kama nimepatia), Alimpataje mtoto? Kama alimbeba bwana wa mtu (ombe hiyoko), kama ni mume wake halali je mama ni mtumiaji wa madawa ya shirki. Ukiwa muumini wa uganga na mambo ya mfanano huo ni rahisi sana shetani kupata uhalali kwenye kizazi chako hatimae watoto wanazaliwa na matatizo mbalimbali, ama pia tatizo laweza kuwa kwenye damu nikimaanisha generational penalty from sins done by the past generation.
Kimtaani tunasikiaga watoto ni malaika na hawana dhambi. So kama ni kitu kibaya hata warushiwe vipi wanalindwa. Ukiona mtoto amefikia hapo, kuna tatizo kubwa, na shetani ana uhalali wa kum-own mtoto. Anyways hata niandikeje naweza nisieleweke maana tayari tuko kwenye imani na mienendo ama mafundisho tofauti. Mungu amsaidie aweze kulitatua.