Mtoto wa mkeo asipokupenda unafanyaje?

Mtoto wa mkeo asipokupenda unafanyaje?

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Imetokea na huwa inatokea mtoto wa mkeo hakupendi. Umeamua kuishi au kuoa mke ambaye hana kazi ana mtoto mmoja wa kike au wa kiume mwenye umri wa miaka 4 sasa mkeo anajaribu kumwambia mtoto kuwa wewe ndiye baba yake au baba wa kambo mtoto hataki na ukijaribu kuwa karibu na yeye hakubali, unamletea juice, pipi, biscuit mara kwa mara kama zawadi hataki, siku moja mkiwa wawili wewe na mkeo mama anamuuliza mbele yako huyu nani anasema hajui

Wenye uzoefu na haya mambo unafanyaje, kwanza mama hajisikii vizuri mtoto kutokuwa karibu na wewe na hataki kukusogelea ukizingatia kuwa mkeo alikwambia kuishi na mimi lazima umkubali mwanaye. Zingatia kwamba mkeo hana tena wazazi kwamba angempeleka mtoto kwa bibi yake.

Tunafanyaje kwa mfano huu.
 
Mkuu anza nae taratibu atakuzoea, bado mdogo huyo ila mama ake anatakiwa akazanie ukaribu Kati yako na huyo mtoto mfano awe muda wote kila anapomtuma awe anakazania wewe ni babaake atabadilika
 
NI UTOTO UNMSUMBUA ataacha alikua.........endelea kum care. ...ingawa anaonekana ana kbur cha kichaw......

Anyway

MWANAMKE WA KUOLEWA AWE.....BIKRA TU ...
What? Mtoto kama huyo atakuwa na kiburi cha kichawi, baada ya muda gani ataacha maana kila ukifikiria kumnunulia uniform na mahitaji mengine unaona kama hayuko upande wako
 
Mkuu anza nae taratibu atakuzoea, bado mdogo huyo ila mama ake anatakiwa akazanie ukaribu Kati yako na huyo mtoto mfano awe muda wote kila anapomtuma awe anakazania wewe ni babaake atabadilika
Upo na mama yake mwaka wa 2 sasa maana ulimchukua akiwa na mwaka 1, tazoeaje mfano
 
Mapenzi hayalazimishwi!!

Tatizo mnamlazimisha huyo mtoto kukupenda badala ya kumpa nafasi ya yeye kukupenda mwenyewe naturally. Sijui kwanini ila nahisi kama wewe (or who ever that is) mlikuwa na haraka sana ya kutambulishana kwa mtoto. Mlipaswa kuacha mahuasiano yenu kuwa yenu kwanza, wakati unaanzisha urafiki na mtoto bila pressure yoyote mpaka hapo baadae.

Kama mko serious na mahusiano yenu kweli, cha msingi acheni kum-force huyo mtoto kukupenda/kukukubali mara moja. Na wala usijipendekeze nae sana. Just be there as a friend & a father figure. Akionyesha kukuhitaji kwa lolote sawa, asipoonyesha pia sawa....mwishowe atakuzoea na bond itaanzia hapo. Huyo mtoto bado mdogo sana....angekuwa mkubwa ndio ingekuwa changamoto.

Swali la kizushi.....
Usikute una nia mbaya nao na mtoto can sense that alafu unatuchosha na ushauri? 😬😬
 
Ushauri huu
 
Mama kumuelekeza mtoto akuamkie sio kosa na sio ku force, mama kumwambia mtoto huyo ndio baba yako ili akitaka kufanya kitu ajue huyo ndiye baba sio kosa, mwanaume hata muda wa kutaka kuongea na mtoto ila kama mtoto wake akitoka kazini au sehem anakuja na zawadi bado mtoto hataki hizo zawadi. Nia mbaya kwa huyo mtoto ni kama ipi mfano maana hakuna mpango wa kumuumiza au kumfanyia mtoto kitu kibaya.
 
Duuu kuna vitu kweli kibinadamu kuvibadilisha ni kazi aisee.

Ushauri wangu mimi ni jitahidi usisubutu kumfokea mtoto wala mama yake (wife).

Pili jitahidi kuchunguza anapenda michezo gani huyo mtoto, yani hata kama anapenda kuchezea simu unakua unampa achezee.

Yani mimi huwa nina chemistry nzuri na watoto automatically tu.
Kuna mtoto wa best yangu ni ananipenda balaa nikienda kwao kisha nikiwa naondoka huwa kanasikitika sana, kanatamani hadi kunifata.
 
Duuu kuna vitu kweli kibinadamu kuvibadirisha ni kazi aisee.

Ushauri wangu mimi ni jitahidi usisubutu kumfokea mtoto wala mama yake (wife).

Pili jitahidi kuchunguza anapenda michezo gani huyo mtoto, yani hata kama anapenda kuchezea simu unakua unampa achezee.

Yani mimi huwa nina chemistry nzuri na watoto automatically tu.
Kuna mtoto wa best yangu ni ananipenda balaa nikienda kwao kisha nikiwa naondoka huwa kanasikitika sana, kanatamani hadi kunifata.
Nadhani mama mtoto alitakiwa kwanza amzoeshe mwanaye kumfahamu mtu aliye naye kimapenzi kabla hawajakubaliana ili mtoto amjue baba mdogo au baba wa kambo labda, mtoto hafokewi wala mama yake hafokewi ni amani kabisa, hilo la michezo nilijua anacheza gemu kwenye simu ya mama yake nikamletea ki machine kidogo cha gemu amekikataa nikampa simu yangu akakataa nikanunua simu flani ili asisumbue ya mama yake akakataa
 
Back
Top Bottom