Lakini raia wake waliishi maisha matamu sana...sasa hivi je? Hakuna rangi wanaacha ona
Hawakuishi maisha matamu wala nini. Wewe unasema siasa uchwara za kulipiwa mahari. Huwazi ni watu wangapi wanaoa kwa mwaka Nchini na Nchi ina watu wangapi. Na huwazi mtu akishaoa familia atailisha nini.
Kumbuka Libya haikuwa na Uchaguzi, Mahakama, wala Shule za kueleweka. Kwani Wanafunzi walifundishwa Kiarabu tu..
Na ukitokea kumpiga japo kwa kuongea tu unafungwa.. Na allikuwwa anamuandaa mwanae kuwa Rais kwani 70% ya Viongozi walikuwwa wanafamilia wa Ghadaffi.
Watu wallikuwa wanadai Democrasia. Ndo chanzo cha maandamano.. Akaamuru watu watoke barabarani wakagoma, akaagiza Polisi waue kila mtu atakaye andamana.. Watu walikufa sana, ndo Jeshi likaingilia kati kusaidia wananchi wasiuawe na Polisi. Hapo ndo Jeshi likagawanyika.. Wanaounga mkono Ghadaffi na Wanaounga Mkono Wananchi. Ndo chanzo cha Vita yao. Wanajeshi wanaounga Mkono Wananchi wakaitwa Waasi.
Katika kudhibiti Waasi, kuna mji wa Pili kwa ukubwa Libya unaitwa Bhangazi, Wanajeshi wa Ghadaffi walizidiwa Nguvu, ukaangukia mkononi mwa Waasi.. Wananchi wakagaiwa siraha zote zilizokuwa Bhangazi, wakajiunga na Waasi kulinda mji wao.
Kama baada ya Wiki baraza la usalama la Libya likaamua mji wote wauteketeze, Yaani Majeshi yote Kutoka Mkoa waelekee Bhangazi, asiingia mtu wala kutoka Mtu.
Vifaru na ndege zikaelekezwa Bhangazi,
Ila kumbuka hata hao wanajeshi wa Ghadaffi wapo wanaotokea Bhangazi..
Hivyo ndege nyingi zilikuwa zinaangisha mabomu nje ya target wanakea makusudi kwani wallikuwa wakikuta wananchi wapo wanashangilia ushindi hata hawapambani, wengine wa kwenye ndege za Vita hawakurusha Bomu hata moja bali walitoroka na ndege na kwenda nazo nchi jirani kama wakimbizi.
Sema vifaru ndo vilikuwa vinafyeka sana watu.. Wale waansi wanaomba msaada wa kimataifa kwani risasi na siraha ziliwaishia.. Ndipo Ufaransa ikatoa msaada wa haraka wa kuangamiza kama robo tatu ya Vifaru vilivyokuwa vinaelekea Bhangazi.
Marekani ikaleta ndege ya Silaha ikazidondosha Bhangazi.
Vita ikaanza upya.. Makamanda wakaanza kusonga mbele kuelekea..
Baada ya kupokea Siraha, ndo kwa muda mfupi sana wakauteka mji wa Al-Bayda na hapo hapo mji tajiri wa mafuta Tobruk..
Ndipo Waasi wakaanza kupata hela.. Waliishikilia hiyo miji kufa kupona.. Wwakaanza kuwauzia Marekani mafuta.. Wakaletea Magari ya Kivita na Pickup nyingi pamoja na silaha nyingi..
Vita ikanoga..
Hili ndo handaki alilojificha akijifanya komando na kubadilisha nguo. Kutoka kuishi kifalme hadi hapa🤣. Hii ni baada ya msafara wake kushambuliwa.
Hii vita ndo vita najua vizuri ambayo nilifuatilia mwanzo mwisho. Hata Gaddafi alipodakwa kama kuku niliweka thread hadi moderator wakawa haamini kila nikiweka wanatoa.🤣🤣.
Gaddafi aliongoza miaka 42, lakini ilituchukua miezi 9 tu kumshikisha adabu.
Hadii Mwili wa ghadaffi unaagwa akiwa kifua wazi. Hadi ghadaffi hujambo anaburuzwa barabarani kwenye gari.. Ghadaffi alidakwa na vijana wadogo wala sio wanajeshi. Hata walipotoa taarifa kwa Jeshi la waasi kwamba tumemkamata Ghadaffi hawakuamini kwani ilikuwa nje ya mji. Hadi wanajeshi wanafika wakakuta wanshamuaa na kugawanagawana nguo zake. Ndo mwili wake kubebwa.
Ghadaffi alikuwa na Vifaru, Mizinga na zana zote za kivita, lakini haya Magari/Pickup ndo zilimtoa Madarakani.