Habar wakuu msaada wenu bint yangu wa mwaka mmoja anakohoa sana usiku tumejaribu kumpa dawa na kwenda hospital dawa hazijasaidia kitu...anakohoa Hadi inaogopesha ,,na mchana mara Chache hukohoa
Habari,
Vikohozi vinavyokazana/zidi usiku na kupungua mchana, vikiwa haviambatani na homa vinahusishwa zaidi na allergy/mzio.
1: Hatua ya kwanza ni kujua mfumo wa maisha wa wazazi.
Je wazazi kuna mwenye historia ya mzio, mfano: vumbi nk.
Hii husaidia ufatiliaji kwa mtoto pia.
2: Maisha ya mtoto binafsi.
Matumizi ya:
1: Vitu vinavyoambatana na hali husika ni kama: matumizi ya karanga/unga wa karanga, unga wa mbegu za maboga, blue band na maziwa yatokanayo na wanyama.
Ni vyema kuangalia kitu kipya kilichoanzishawa kwenye mlo wake kipindi anaanza kukohoa.
2: Wazazi kutumia manukato au mtoto kutumia mafuta au sabuni zenye manukato.
3: Matumizi ya feni au AC.
4: Kuishi eneo ambalo lina maua au mahindi au mimea ambayo inatoa mbelewele/pollen grain. Usiku ni muda ambao mazao husika huachia pollen grain kwenye hewa hasa kwa maua.
Haya yote hutoa uchaguzi wa aina ya dawa anayotakiwa kupewa mtoto.
NB: Haya ni maelezo ya jumla, ni vyema kumfikisha mtoto kwa daktari mwenye ujuzi hasa daktari bingwa wa watoto ili kufanya tathmini kwa mhusika zaidi kwa kuzingatia erefu wa muda, kiasi cha kikohozi na yanayoambatana pia ukaguzi wa mtoto.