Mtoto wa mwaka 1 anakohoa sana usiku

Mtoto wa mwaka 1 anakohoa sana usiku

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,266
Reaction score
3,698
Habar wakuu msaada wenu bint yangu wa mwaka mmoja anakohoa sana usiku tumejaribu kumpa dawa na kwenda hospital dawa hazijasaidia kitu...anakohoa Hadi inaogopesha ,,na mchana mara Chache hukohoa
 
amepungua uzito?
hachezi sana na wenzie kabla hajaanza kukohoa sana
hapendi kula
kama yote anayo hapo juu,mtoto anaweza kua na maambukizi ya kifua kikuuu.
 
Kuna kitu kinaitwa "kimeo" kama sikosei, jaribu kucheki hicho
 
Habar wakuu msaada wenu bint yangu wa mwaka mmoja anakohoa sana usiku tumejaribu kumpa dawa na kwenda hospital dawa hazijasaidia kitu...anakohoa Hadi inaogopesha ,,na mchana mara Chache hukohoa
Ni kwasababu ya baridi angalia unapo ishi sio bondeni au swamp jotahidi kulala na nguo nzito isio pitisha baridi mpaka shingoni.......nimonia pia inasumbua watoto wadogo siku hizi.
 
amepungua uzito?
hachezi sana na wenzie kabla hajaanza kukohoa sana
hapendi kula
kama yote anayo hapo juu,mtoto anaweza kua na maambukizi ya kifua kikuuu.
Hajapungua uzito,anacheza sana tu na anakula vizur
 
Ni kwasababu ya baridi angalia unapo ishi sio bondeni au swamp jotahidi kulala na nguo nzito isio pitisha baridi mpaka shingoni.......nimonia pia inasumbua watoto wadogo siku hizi.
Hatuishi mabondeni na hakuna barid
 
Habar wakuu msaada wenu bint yangu wa mwaka mmoja anakohoa sana usiku tumejaribu kumpa dawa na kwenda hospital dawa hazijasaidia kitu...anakohoa Hadi inaogopesha ,,na mchana mara Chache hukohoa

Pole sana.

Mpeleke hospital ili akafanyiwe vipimo vya kifua na makohozi.

Kila la kheri.
 
Habar wakuu msaada wenu bint yangu wa mwaka mmoja anakohoa sana usiku tumejaribu kumpa dawa na kwenda hospital dawa hazijasaidia kitu...anakohoa Hadi inaogopesha ,,na mchana mara Chache hukohoa

Habari,

Vikohozi vinavyokazana/zidi usiku na kupungua mchana, vikiwa haviambatani na homa vinahusishwa zaidi na allergy/mzio.

1: Hatua ya kwanza ni kujua mfumo wa maisha wa wazazi.
Je wazazi kuna mwenye historia ya mzio, mfano: vumbi nk.
Hii husaidia ufatiliaji kwa mtoto pia.

2: Maisha ya mtoto binafsi.
Matumizi ya:

1: Vitu vinavyoambatana na hali husika ni kama: matumizi ya karanga/unga wa karanga, unga wa mbegu za maboga, blue band na maziwa yatokanayo na wanyama.
Ni vyema kuangalia kitu kipya kilichoanzishawa kwenye mlo wake kipindi anaanza kukohoa.

2: Wazazi kutumia manukato au mtoto kutumia mafuta au sabuni zenye manukato.

3: Matumizi ya feni au AC.

4: Kuishi eneo ambalo lina maua au mahindi au mimea ambayo inatoa mbelewele/pollen grain. Usiku ni muda ambao mazao husika huachia pollen grain kwenye hewa hasa kwa maua.

Haya yote hutoa uchaguzi wa aina ya dawa anayotakiwa kupewa mtoto.

NB: Haya ni maelezo ya jumla, ni vyema kumfikisha mtoto kwa daktari mwenye ujuzi hasa daktari bingwa wa watoto ili kufanya tathmini kwa mhusika zaidi kwa kuzingatia erefu wa muda, kiasi cha kikohozi na yanayoambatana pia ukaguzi wa mtoto.
 
amepungua uzito?
hachezi sana na wenzie kabla hajaanza kukohoa sana
hapendi kula
kama yote anayo hapo juu,mtoto anaweza kua na maambukizi ya kifua kikuuu.
Duuh kirahisi rahisi tu ushahitimisha hivyo, mtakuja kuua watu Kwa presha nyie ma bush Dr .
 
Habari,

Vikohozi vinavyokazana/zidi usiku na kupungua mchana, vikiwa haviambatani na homa vinahusishwa zaidi na allergy/mzio.

1: Hatua ya kwanza ni kujua mfumo wa maisha wa wazazi.
Je wazazi kuna mwenye historia ya mzio, mfano: vumbi nk.
Hii husaidia ufatiliaji kwa mtoto pia.

2: Maisha ya mtoto binafsi.
Matumizi ya:

1: Vitu vinavyoambatana na hali husika ni kama: matumizi ya karanga/unga wa karanga, unga wa mbegu za maboga, blue band na maziwa yatokanayo na wanyama.
Ni vyema kuangalia kitu kipya kilichoanzishawa kwenye mlo wake kipindi anaanza kukohoa.

2: Wazazi kutumia manukato au mtoto kutumia mafuta au sabuni zenye manukato.

3: Matumizi ya feni au AC.

4: Kuishi eneo ambalo lina maua au mahindi au mimea ambayo inatoa mbelewele/pollen grain. Usiku ni muda ambao mazao husika huachia pollen grain kwenye hewa hasa kwa maua.

Haya yote hutoa uchaguzi wa aina ya dawa anayotakiwa kupewa mtoto.

NB: Haya ni maelezo ya jumla, ni vyema kumfikisha mtoto kwa daktari mwenye ujuzi hasa daktari bingwa wa watoto ili kufanya tathmini kwa mhusika zaidi kwa kuzingatia erefu wa muda, kiasi cha kikohozi na yanayoambatana pia ukaguzi wa mtoto.
Mleta uzi fuata huu ushauri hao wengine watakuingiza chaka uishie kumuumiza tu huyo mtoto .
 
Habar wakuu msaada wenu bint yangu wa mwaka mmoja anakohoa sana usiku tumejaribu kumpa dawa na kwenda hospital dawa hazijasaidia kitu...anakohoa Hadi inaogopesha ,,na mchana mara Chache hukohoa
1. Epuka neno kilimi...usije kujaribu kumkata.
2. Msaada wa uhakika tafuta SPECIALIST WA ENT (E=Ear, N=Nose, T=Throat. Hapa utasaidika haraka)
 
Habar wakuu msaada wenu bint yangu wa mwaka mmoja anakohoa sana usiku tumejaribu kumpa dawa na kwenda hospital dawa hazijasaidia kitu...anakohoa Hadi inaogopesha ,,na mchana mara Chache hukohoa
Usifanye uzembe utapoteza mtoto huyo hamia hospitali kubwa zaidi umuone pediatrician
 
Back
Top Bottom